Hii ni sehemu ya makala zetu maalumu kuhusu mashindano ya Olympiki ya 2012 jijini London .
Pongezi nyingi zimekuwa zikimimika kwa muogeleaji wa Afrika Kusini Cameron van der Burgh ambaye amechukua medali ya kwanza ya dhahabu baada ya nchi hiyo kupata matokeo mabaya katika mashindano ya Olimpiki ya mwaka 2008 yaliyofanyika jijini Beijing. Alishinda medali hii ya dhahabu siku ya jumapili baada ya kuibuka mshindi katika uogeleaji wa mita 100 kwa kuweka rekodi ya dunia kwa kuogelea kwa muda wa sekunde 58.46. Pia, yeye ndiye muogeleaji wa kwanza mwanaume kutoka Afrika ya kusini kushinda medali ya dhahabu katika mashindano ya Olimpiki. Hii imemfanya Cameron van der Burgh, kupewa jina la utani ‘Golden Boy’ na pia ushindi wake kutawala majadiliano katika mtandao wa Twita.
Redio ya Voice of the Cape inauelezea ushindi wake :
Kulikuwa na furaha katika maeneo yote ya Afrika ya Kusini siku ya Jumapili Usiku wakati muogeleaji Cameron van der Burgh alipofanikiwa kunyakua medali ya kwanza ya dhahabu kwa nchi ya Afrika ya Kusini katika mashindano ya Olimpiki ya mwaka 2012 mjini London, sio tu kwamba amekuwa mshindi katika upigaji mbizi wa mita 100, lakini pia ameweka rekodi mpya ya dunia.
Cameron katika mtandao wake wa Twita, alionesha furaha yake:
@Cameronvdburgh: mimi ni bingwa wa olimpiki:) kama mlivyosema katika kurasa zenu za twita. Hisia zilizopitiliza! Kama tu jinsi maisha yangu yalivyokuwa, lakini http://instagr.am/p/Nsg12grbC3/
Magazeti mengi ya Afrika ya Kusini yaliuza sana kwa habari hii kugonga vichwa vya habari:
Miitikio kutoka kwa wanablogu wa Afrika Kusini:
:
Jason Von Berg anaelezea kipindi ambacho alifanya naye kazi:
Niliwahi kupata bahati ya kukutana na Cameron na kufanya nae kazi katika miradi kadhaa yeye akiwa kama balozi wa Audi, na ninachoweza kukuambia ni kuwa, Cameron ni miongoni mwa watu wazuri sana. Hivyo usiku wa jana kumuona Cameron akishinda taji la Olimpiki inamuelezea vizuri zaidi. SAFI SANA Cammy unayeogelea kama samaki!
HURRICANEVANESSA alijisikia kuweka hadharani picha ya Cameron:
Tulitambua mapema kipaji cha ndugu Cameron Van der Burgh. Hapa, yeye ni mshindi wa medali ya dhahabu kwa kukaa utupu katika suala lile la Marie Claire la utupu la mwaka 2011.
Ilikuwa na lengo la kuwasaidia mbwa wadogo wanaotangatanga, makinda.
Maoni ya watumiaji wa Twita wa Afrika Kusini::
@PebblesProject: @Cameronvdburgh Wewe ni shujaa wetu. Umeifanya nchi nzima kujisikia fahari sana.
@swanniem: @Cameronvdburgh ulitufanya tujisikie fahari sana usiku wa jana na hakika rangi yako ni kama ya dhahabu
@verashni: ningependa kuweka wazi kuwa Cameron van der Burgh anatokea Pretoria. Huu ndio ukweli, ni jiji ninalotokea. Ni jiji ambalo watu wengi wa Afrika Kusini huwa wanalidharau….
@Abramjee: umefanya vizuri Cameron, umefanya Afrika ya Kusini ijivunie. Medali yetu ya kwanza! Tumeshinda dhahabu. @Team_SA_2012 @OlympicsSA @lead_sa @rykneethling
@djcleo1: Afrika ya Kusini imeshinda medali ya dhahabu katika mashindano ya Olimpiki kupitia kwa CAMERON VAN DER BURGH na kuweka rekodi mpya ya dunia #JivunieMwafirkayakusini
Hii ni sehemu ya makala zetu maalumu kuhusu mashindano ya Olympiki ya 2012 jijini London .
2 maoni