- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

Togo: Muhubiri Asafirisha Kilo 4.2 za Madawa ya Kulevya Yaliyofichwa kwenye Pipi ‘k Build Church

Mada za Habari: Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara, Brazil, Ghana, Togo, Mahusiano ya Kimataifa, Sheria, Uandishi wa Habari za Kiraia

Muhubiri wa Injili raia wa Togo, Woegna Yao Koufoualesse alikamatwa katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Accra akiwa na kiasi cha kilo 4.2 za madawa ya kulevya aina ya Cocaine akiwa kwenye safarini kutokea Sao Paulo, chapisho la Afrique Infos linaripoti [1] [fr]. Madawa hayo yalikuwa yamefichwa ndani ya peremende za kijiti; Koufoualesse alijitetea kwamba hakujua kuhusu madawa hayo na kwamba piremende hizo zilikuwa ziuzwe kwa ajili ya kusaidia kupata fedha za kujengea kanisa.