Julai, 2012

Habari kutoka Julai, 2012

Hispania: Maandamano ya Wachimbaji Madini Yaungwa Mkono na Wananchi

  16 Julai 2012

Maelfu ya wananchi wa Uhispania wameungana na maandamano ya wachimbaji wa madini nchini humo, wakati waandamanaji hao walipowasili nchini Madrid baada ya kutembea kilometa 400 wakitokea kaskazini mwa nchi hiyo. Wachimbaji hao walishangazwa na kiwango cha hamasa kilichoonyeshwa, ambacho kiliongeza chachu ya kile ambacho sasa chaitwa 'usiku wa wachimbaji madini'

Msumbiji: Je, Zana za Uandishi wa Kiraia Zimeua Blogu?

Katika mfululizo mfupi wa makala zake, Profesa Carlos Serra anabainisha baadhi ya sababu zinazoeleza kwa nini blogu za Msumbiji zinaendelea kupungua siku hadi siku. Msomaji mmoja anatoa maoni akidhani kwamba kublogu kunahitaji kazi kubwa katika kuhakikisha kuwa habari mpya zinaendelea kuwepo sambamba na kiwango cha habari hizo. Wakati Serra anasema...

Wananchi wa Mexico Wanamchagua Rais Mpya

  12 Julai 2012

Mnamo tarehe 1 Julai, Wa-Mexico walipiga kura kumchagua rais wao mpya. Punde tu kura zilipoanza kupigwa, watumiaji wa mtandao wa intaneti walianza kutoa mawazo na uzoefu wao. Walipanga pia namna tovuti na alama ishara za mtandao wa twita zitakavyotumika kukusanya taarifa juu ya udanganyifu na nyendo zilizo kinyume cha sheria wakati wa uchaguzi huo.

Uganda: Kuvunja Utamaduni wa Ukimya Kuhusu Haki za Afya.

A video produced by Results for Development, an international non-profit organisation whose mission is to unlock solutions to tough development challenges, was released online recently to encourage Ugandans to break the culture of silence and take control of their health rights.A video produced by Results for Development, an international non-profit organisation whose mission is to unlock solutions to tough development challenges, was released online recently to encourage Ugandans to break the culture of silence and take control of their health rights.

Somalia: Migawanyiko Mikubwa Kuhusu Katiba Mpya

Somalia, ambayo haijawahi kuwa na serikali kuu inayotawala nchi nzima tangu mwaka 1991, inaandika rasimu ya katiba mpya ambayo inatarajiwa kuhitimisha muda wa utawala wa serikali ya mpito iliyopo madarakani na kumchagua rais mpya. Hapa tumekusanya mijadala na mazungumzo ynayoendelea mtandaoni kuhusu rasimu hiyo ya katiba.