- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

Misri: Waandamanaji Watuma Ujumbe Dhidi ya Udhalilishaji wa Kijinsia.

Mada za Habari: Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini, Misri, Haki za Binadamu, Maandamano, Uandishi wa Habari za Kiraia, Wanawake na Jinsia

Nchini Misri, udhalilishaji wa kijinsia ni tatizo kubwa [1], na ndilo jambo linaloongozwa kupingwa na Wamisri. Maandamano yalifanywa na vijana wadogo wa Misri, wasichana kwa wavulana katika mji mdogo wa Nasr jijini Cairo mnamo tarehe 4 Julai kwa lengo la kutuma ujumbe kupinga udhalilishaji wa kijinsia.

Tangu mapinduzi yalipofanyika, Wamisri wanaotumia mtandao wa intaneti [2] na wasiotumia mtandao wa intaneti wamekuwa wakisimama imara kupinga udhalilishaji wa kijinsia pamoja na machafuko yatokanayo na kutokujali usawa wa binadamu. Mwezi Juni matembezi [3] ya kupinga udhalilishaji wa kijinsia yalishambuliwa [4]. Haikujalisha, harakati za kukabiliana na udhalilishaji huo zinaendelea.

Malengo ya maandamano ya Julai 4 yalilenga kuweka msimamo kuhusu kupinga udhalilishaji wa kijinsia na kudai usalama wa mitaa kwa wote. Maged Tawfiles [5] alikuwepo kwenye tukio na alipiga picha [6] zifuatazo (picha zote zimetumika kwa ruhusa):

[7]


“Uhuru wangu ni utu wangu”

[7]


“Mwanamke yeyote wa Misri ana haki ya kutembea kwa uhuru”

[7]


“Sihitaji kuchukia kwa mimi kuwa msichana”

[7]


“Natamani kama ungeacha kuangalia mwili wangu”

[7]


“Nahitaji kuendesha baiskeli bila kudhalilishwa”

[7]


“Sidhalilishi ili na dada yangu asidhalilishwe”

[7]


“Jitambue mwenyewe, sio mavazi yangu”

[7]


“Mtaa siyo wako, uhuru wangu siyo wako”