- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

Basi la Watalii Raia wa Israeli Lashambuliwa Nchini Bulgaria

Mada za Habari: Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini, Ulaya Mashariki na Kati, Bulgaria, Israel, Habari za Hivi Punde, Uandishi wa Habari za Kiraia

Watu wapatao saba wameuawa katika shambulio lililofanywa dhidi ya kijana raia wa Israeli [1] katika basi lililokuwa limebeba watalii karibu na uwanja wa ndege wa Burgus nchini Bulgaria.

Ripoti zinadai kuwa shambulio hilo inawezekana lilifanywa na kijana aliyekuwa amevaa bomu la kujitoa muhanga, ambaye huenda alikuwa kando ya basi  ama aliingia ndani ya basi. Kwa mujibu wa nrg [2], mwanamke huyo aliyejitoa muhanga alisimama mbele ya mojawapo ya mabasi hayo na kulilipua bomu hilo.

HABARI MPYA:
@BarakRavid [3]:

Waziri wa Mambo ya Nje wa Bulgaria alizungumza na Waziri wa Mambo ya Nje Lieberman na kumwambia kuwa uchunguzi uligundua kwamba mlipuko huo ulisababishwa na bomu lililokuwa limefichwa kwenye buti la basi.

Waziri Mkuu wa Israeli  Bibi Netanyahu alitoa tamko kwamba “dalili zote zinaelekeza kuwa Irani inahusika na mpango wa shambulio hilo” [4] na kwamba Israeli itajibu kwa ukali.

@ruslantrad:

bTV ikionyesha picha za shambulio dhidi ya watalii wa Israeli huko Bulgaria

Shoshi, raia wa Israeli aliyeshuhudia mlipuko huo alisema [5]:

Tulipita uhamiaji na tukaingia kwenye basi namba 4 nje ya uwanja wa ndege. Tuliweka mizigo yetu, na baada ya dakika mbili basi namba 2 liliripuka na kushika moto. Kwa haraka sisi wengine tulikimbizwa kwenye chumba salama.

Mwanae wa kiume aliongezea:

Watu walionusurika kwenye basi iliwalazimu kuruka miili iliyotawanyika nje ya basi ili wasiikanyage. Tuliliona basi hilo, raia mmoja wa Israeli alipiga picha ya tukio hilo. Tuliona buti lake likilipuka. Tulikimbilia kwa haraka kwenye jengo la abiria.

Katika ukurasa wake wa Facebook [6], Waziri wa Mambo ya Nje Avigdor Liberman aliandika:

Hivi sasa nimezungumza na Waziri wa Mambo ya Nje wa Bulgaria, Nikolay Mladenov  kuhusu mlipuko huo. Mladenov anaelekea eneo la tukio na atanipa taarifa kamili kuhusu yanayoendelea atakapofika hapo.

Twiti kutoka @MokedNews [7] inadai:

Mmoja wa waliouawa katika shambulio hilo nchini Bulgaria, ni mwongozaji wa watalii wa ki-Bulgaria aliyekuwa na watalii hao raia wa Israeli mlipuko ulipotokea. (Chanzo: Televisheni ya Bulgaria)

Habari zaidi za moja kwa moja kwenye blogu ya Haaretz inayoandikwa kwa lugha yaki-Ebrania [5] (habari zaidi za yanayojiri) na kwa lugha yaki-Ingereza [8].

Twiti za kufuatilia habari za moja kwa moja:
@BarakRavid [9] – Mwandishi wa kidiplomasia, gazeti la Haaretz
@ruslantrad [10] –  Mwanablogu wa Syria-Bulgaria na Mchambuzi wa Mashariki ya Kati na Afrika ya Kaskazini
@MokedNews [11] – Kikusanya habari za Israeli