Mkutano wa Global Voices (Sauti za Dunia) wa 2012 umeshafunguliwa muda mfupi uliopita katika jiji la Nairobi, nchini Kenya. Tungetamani sana ungeweza kujumuika nasi pale, lakini kama hilo haliwezekani, waweza pia ukatutazama moja kwa moja kupitia mtandao wa intaneti na pia tukaweza kujadiliana papo kwa hapo.
Ni tukio la wazi linalowajumuisha washiriki 300 kutoka nchi 60 duniani, zaidi wanablogu na waandishi wa vyombo vya habari vya kiraia wenye umri kati ya miaka 18 hadi 76. Lengo la kongamano hili ni kujadili kuhusu upana na umuhimu wa vyombo vya habari za kiraia za mtandaoni ulimwenguni kote.
Tafadhali tembelea Blogu ya Mkutano, ratiba,katika alama ishara ya Twita, #GV2012, na pia kutazama video ifuatayo. Baadhi ya matukio yanaendeshwa kwa namna mbili, hivyo waweza kutembelea ukurasa maalumu wa video wa kongamano na kisha uchague kati ya namna hizo mbili.
Sambaza taarifa hizi na kwa wengine!
Haa! Pia tuna picha nzuri za moja kwa moja katika mtandao wa Flickr.