Habari kutoka 21 Julai 2012
Ethiopia: Maandamano ya Waislamu Yashika Kasi
Jeshi la Polisi nchini Ethiopia waliamua kutumia nguvu kupambana na wanaharakati wa ki-Islamu, likituhumiwa kufanya vitendo haramu katika maeneo yanayochukuliwa kuwa matakatifu katika misikiti, kwa mujibu wa habari zilizoandikwa na ukurasa wa kikundi cha waislam katika mtandao wa Facebook uitwao Dimtsachin Yisema (Iache Sauti Yetu Isikike). Tangu mwezi Mei, Wa-Islamu wa ki-Ethiopia wamekuwa wakiandamana kupinga serikali kuingilia mambo yao ya kidini.
Paraguai: Kutoka Kutumikishwa Hadi Kuwa Kiongozi Mzawa.

Kutana na Margarita Mbywangi, ambaye katika umri wa miaka mitano, alichukuliwa kutoka kwa wazazi wake na kuuzwa mara kadhaa na kulazimishwa kufanya kazi za nyumbani. Tangu wakati huo amekuwa kiongozi muhimu wa kabila la Aché na hata kuwa Waziri katika nchi yake. Mbywangi sasa anasimulia maisha yake binafsi kupitia Mradi wa Rising Voices.
Afghanistan: Mwanafunzi wa Sekondari Agundua Kanuni ya Hisabati
Mwanafunzi wa Sekondari nchini Afghanistan amegundua kanuni ya kimahesabu inayoweza kutumika kukokotoa milinganyo ya kwadratiki. Watumiaji wa twita wamezipokea habari hizo kama ishara ya maendeleo ya sekta ya elimu nchini humo.
Matangazo ya Mkutano wa Sauti za Dunia (Sehemu ya 1)
Sauti za waliowakilisha GV katika warsha mjini Nairobi, Kenya.