8 Julai 2012

Habari kutoka 8 Julai 2012

Somalia: Migawanyiko Mikubwa Kuhusu Katiba Mpya

Somalia, ambayo haijawahi kuwa na serikali kuu inayotawala nchi nzima tangu mwaka 1991, inaandika rasimu ya katiba mpya ambayo inatarajiwa kuhitimisha muda wa utawala wa serikali ya mpito iliyopo madarakani na kumchagua rais mpya. Hapa tumekusanya mijadala na mazungumzo ynayoendelea mtandaoni kuhusu rasimu hiyo ya katiba.

Cameroon: Ndoto za Umeme kwa Ajili ya Maendeleo ifikapo 2035

  8 Julai 2012

Cameroon inatarajiwa kufikia hadhi ya soko linalokua kwa kasi ifikapo mwaka 2035 kupitia "mafanikio makubwa" ya hatua kwa hatua katika maendeleo ya miundombinu ya usafiri na nishati. Hata hivyo kufikiwa kwa malengo hayo ndani ya muda uliopangwa hakuonekani kuwashawishi wachambuzi wengi wa masuala ya kisiasa, kwa sababu tu changamoto zilziopo ni nyingi.