7 Julai 2012

Habari kutoka 7 Julai 2012

Misri: Mubarak Afariki Dunia kwa Mara Nyingine

Rais wa zamani wa Misri Hosni Mubarak amewahi kufa angalau mara moja kwa kila baada ya majuma machache tangu kuanza kwa mapinduzi ya Misri, yaliyouangusha utawala wake uliodumu kwa miaka 32. Watumiaji wa mtandao wanaitikia tetesi za hivi karibuni kuhusu afya yake.

7 Julai 2012

Cuba: Maandamano yafanyika Mara Mbili, Wengi Wakamatwa

Kikundi cha wanawake kijiitacho ‘wanawake wavaliao mavazi meupe’ (Ladies in White) kwa mara nyingine wametawala fikra za wanablogu wa Cuba waishio nje ya nchi. Maandamano ya amani ya kikundi hicho ambacho ni moja wapo ya vyombo vya upinzani vinavyoheshimika zaidi katika visiwa hivyo –pamoja na kukamatwa kwao mara kwa mara na vyombo vya dola –yanaendelea kuvuta hisia za watu. Mapambano ya hivi karibuni yalitokea mwishoni mwa juma lililopita wakati wanachama wa kikundi hicho walipojaribu kufanya maandamano mara mbili mjini Havana.

7 Julai 2012

Tazama Picha za Afghanistan Ambazo Huwa Huzioni

Vyombo vingi vya habari vinavyovipoti hali inavyoendelea nchini Afghanistan hubeba taswira mbya. Kupitia miwani yao, Afghanistan huoneshwa kama nchi inayozama kwenye vimbi la mapigano na sura ya kijeshi. Wapiga kura kadhaa wanawasaidia watu kuona nchi hiyo iliyoathiriwa na vita lakini nzuri kwa mtazamo tofauti.

7 Julai 2012