Umuhimu wa Kongamano La Sauti za Dunia (Global Voices Summit) hapa Nairobi

 Kuanzia tarehe mbili mwezi wa Julai hadi tarehe nne mwezi huo huo, familia ya Sauti za Ulimwengu (Global Voices, GV) pamoja na washiriki wao wa kimataifa, raia wapendao vyombo vya habari na watazamaji watakusanyika pamoja katika hoteli ya Pride-Inn mjini Nairobi kwa kongamano la GV ambalo hufanyika baada ya kila miaka miwili. Mkutano uliopita ulifanyika nchini Chile. Bila shaka:tukio hili ni la kusisimua na ambalo limekuwa likitarajiwa na wengi kwa shauku kuu!

Hii itakuwa mara ya kwanza kwa Kongamano hili kufanyika Afrika Mashariki na wengi wetu kutoka eneo hili tunataka kuwakaribisha wageni wetu.

Lazima niseme kuwa nimesisimka sana, hasa kwa kuwa sijatimiza hata mwaka mmoja kama mwanachama wa kikudi hiki lakini nimefaidika kwa njia nyingi kama mwandishi kutokea Kenya. Nina hamu ya kukutana na waandishi na wahariri wengine ambao nimefanya kazi nao kupitia intaneti.

Kwa kuwa washiriki watatoka mabara mbalimbali, wenye tamaduni na asili mbalimbali nina uhakika kuwa washiriki wote watajifunza mengi. Pia sina shaka kuwa majadiliano tutakayo kuwa nayo, wakati tutakapokuwa pamoja yote yatakuwa ya thamani kwa wote. Kuwa miongoni mwa watu wenye vipaji tofauti, werevu, usanii kutakuwa ni kilele cha marupurupu yatokanayo!

Kwa nini Nairobi?
Swali hilo kwa ukweli limenitatiza, sikuwa mmoja kati ya waandalizi, hivyo basi siwezi kudhania sababu zao za kuchagua Nairobi. Katika makala hii hata hivyo, nitajaribu kuwaonyesha masuala yanayoifanya, Nairobi Kenya kuwa chaguo.

Kenya kama nchi inajulikana kwa sababu tofauti. Inajulikana sana hasa kwa sababu ya wanariadha ambao hutawala katika mashindano mbalimbali ya mbio ndefu kote duniani.

Kenya pia inajulikana kwa wanyamapori na mizunguko ya kitalii na ndio sehemu zilipo mbuga Maasai Mara pamoja na maeneo mengine mashuhuri ya kitalii (kwa maelezo zaidi angalia MagicalKenya tovuti ya Shirika la Kitalii la Kenya). Mji mkuu wa Nairobi unajivunia kwa kuwa mmoja wa miji ya aina ya kipekee duniani, kwa kuwa hifadhi ya wanyama ya Nairobi iko dakika 15 kutoka eneo la katikati la biashara.

Labda jambo ambalo linalojulikana sana kuhusu nchi hii ni kuwa, rais wa kwanza wa Marekani mwenye asili ya ki-Afrika, Barack Obama, anaweza kufuata mizizi ya mababu zake kutokea pahala panapo julikana kama Kogelo, wilaya ya Siaya, sehemu ya Magaharibi mwa Kenya. Wenyeji wa eneo hilo ambao wengi wao ni Wajaluo wanawekuongeza msemo huu “lakini miye sisemi” kwa majivuno kwa kuwa wanatambua hili. Nimeandika hili nikiwa na madhumuni maalum.

Katika kampeni yake ya kuwania uraisi na katika kitabu chake-Ndoto za Babangu(Dreams of My Father), Obama alitaja kuwa alitiwa motisha na namna na urahisi wa maisha wanayoishi watu wa Kenya. Sauti yake, ilikuwa ya kutia motisha na iliwafanya wengi kuamini naye kwa mabadiliko-change you can believe in. Ni wazi, mkakati wa kampeni yake ambao ulitumia vyombo vya habari vya kijamii ulimsaidia kuingia ikulu ya Marekani. Sauti yake na hadithi yake inatuonyesha kuwa wakati mwingine ili kutatua masuala magumu, ufumbuzi rahisi unahitajika.

Kwa kutoa ufumbuzi rahisi kwa masuala magumu, Kenya inaongoza na kwa mawasiliano ya intaneti na kiteknoljia tunajivunia mafanikio kadhaa:

  1. Kenya ndio iliongoza kwa huduma za kutuma pesa kwa kutumia simu, huduma inayojulikana kama M-pesa. Malipo kwa Mpesa na programu ya kutuma pesa kote kwenye mtandao na nje ya mtandao imetupatia njia muwafaka ya biashara na inajihidhihirishia umuhimu wake kwenye soko la kimataifa kama suluhisho la shughuli za malipo.
  2. Pia Kenya ndiyo asili ya programu ya Ushahidi ambayo ni programu huria ya kuorodhesha migogoro ambayo imekuwa ikutimiwa duniani kote katika migogoro na majanga mbalimbali kama vile tetemeko la ardhi nchini Haiti na Tsunami nchini Japan.
  3. Aidha Kenya ndiyo makazi ya i-Hub na asasi dada ya M-Labs, ambayo ni sehemu huru ya kukuza uvumbuzi na teknolojia.

Washiriki katika mkutano watarajie kupata nini kutoka kwenye mkutano?

Mandhari ya Kenya ni nzuri, zaidi ya mvuto wa muonekano wake wa nyanda za juu za bonde la ufa, miji ya pwani, ziwa Victoria, vichaka vya mau na mengineyo.

Wakenya ni watu ambao wanawapenda marafiki. Wana uhusiano mzuri na watu wengine. Labda hili linaonekana kwa kuwa Wakenya wengi wanaongea kiingereza cha malkia kwa ufasaha. Pia katika maeneo ya kitalii usishtuke kumpata dereva wa gari la kukodi ambaye anaweza kuongea kwa ufasaha lugha zingine kama Kijapani, Kichina, Kijerumani au hata Kifaransa, huo ndio utofauti na pengine ishara kubwa ya ukarimu na kuvutiwa kwa masuala ya kijamii wanayoonyesha watu wa Kenya.

Mwandishi na mwanae wakiburudika na ngoma ya ki-Maasai kwenye kijiji cha utamaduni

La muhimu kama nilivyoeleza katika aya zilizopita ni kuwa Kenya ina mazingira mazuri ya kutia mtu motisha na ya uvumbuzi.

Serikali ya Kenya inaongoza kwenye eneo hili kwa miundombinu inayofaa na kuwezesha utamaduni wa ubunifu. Wananchi pia wana uhuru wa kujieleza kwenye intaneti na pia katika mawasiliano mengine.

Uzuri wa nchi na wananchi utasaidia kufanya Kongamano liwe na ufumbuzi wa maana na maamuzi yatakayofikiwa yatasaidia familia ya GV kuendelea kutimiza majukumu yake ya kuwaonyesha watu sauti ambazo haazijasikika tena hapo awali katika dunia ya leo, ambayo leo inapatana zaidi kijamii na kwa njia zinazofaa zaidi kama vile hakujaonekana tena.

3 maoni

jiunge na Mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.