Sudani: “Polisi Yakanusha Kutumia Risasi; Majeruhi wote ni Wakufikirika

Maafisa wa serikali ya Sudani wanaendelea kurudia ‘uongo’ uliozoeleka ambao watawala wa ki-Arabu wamekuwa wakiutumia tangu kuanza kwa yale yanayoitwa Mapinduzi ya Uarabuni yaliyoanza mwezi Desemba 2010. Imekuwa kawaida kusikia kauli kama, ‘waandamanaji wamedhibitiwa wakati wakiwashambulia polisi, ambao nao walijihami kwa kushambulia’ na kuendelea.

Sudani ni nchi iliyojiunga hivi karibuni kwenye vuguvugu kubwa la maandamano ya wananchi wanaotaka mabadiliko yaliyosababisha kuanguka kwa watawala wa muda mrefu kama Zine Al Abedine Ben Ali wa Tunisia mapema mwezi Januari 2011 na mwanzake Hosni Mubarak wa Misri mwezi uliofuata. Muammar Gaddafi wa Libya naye alikamatwa na baadae kuuawa na kundi la wananchi wenye hasira mwezi Oktoba 2011. Serikali za ki-Arabu zimekuwa na jitihada ya kuhakikisha idadi ya madikteta waliong’olewa haizidi hao watatu, kwa kufanya ukandamizaji mkubwa dhidi ya upinzani wa kisiasa na vile vile kuendesha vitendo vya mauaji yasiyokubalika ya watu wao wenyewe wanaoonekana ‘kuwaasi’. Maafisa wa Sudani sasa wanarudia yale yale tuliyoyasikia kwa watawala wote wa nchi za ki-Arabu ambao nchi zao zinasumbuliwa na wananchi wenye hasira ambao wamekuwa wakitawaliwa kidhalimu na kwa kukandamizwa kwa miongo kadhaa.

Maandamano yalianzia katika Chuo Kikuu cha Khartoum mnamo Juni 17, pale mamia ya wanafunzi walipopinga mpango wa serikali wa kubana matumizi. Waandamanaji walikumbana na kipigo cha polisi na wengine wao waliwekwa kizuizini, hali ambayo iliamsha hasira zaidi na maandamano katika siku zilizofuata.

Mimz anaonyesha hisia zake juu ya jinsi ambavyo Shirika la Habari la Sudani (SUNA) lilitangaza habari hizo. Anatwiti:

@MimzicalMimz: Shirika la habari SUNA linasema jana waandamanaji “walizuiwa’. ukweli kwamba shirika hilo limeandika kuhusu habari hiyo jambo hilo pekee ni ujumbe mahsusi kuhusu ukubwa wa maandamano hayo.

Mwandishi wa habari wa ki-Misri Salma Elwardany, ambaye yuko Khartoum, anatoa muhtasari wa yanayotokea nchini humo. Anatwiti[ar]:

ملخص تغطية وكالة الانباء الرسمية لمظاهرات امس: مواطنين اعتدوا على الشرطة فاضطروها لاستخدام الغاز المسيل للدموع ‎http://suna-sd.net/suna/showNews/-fJi7HGycvs26Azq7aG4mmjptp-NQZ_WndSuVb1-KMY/1‏ ‎‫#الخراء‬‏
@S_Elwardany: Ufupisho wa habari zilizotangazwa na Shirika la SUNA jana: raia waliwavamia polisi, ambao ilibidi walazimike kutumia mabomu ya machozi

Ananukuu habari hiyo inayosema:

وتهيب الشرطة بالمواطنين “عدم الالتفات للشائعات التي تؤدى لزعزعة الامن وتعريض الممتلكات للخطر والتعاون مع الشرطة في أداء واجباتها” ‎‫#السودان‬‏
@S_Elwardany: Polisi wametoa wito kwa wananchi kupuuza tetesi zinazotishia usalama wa nchi na uharibifu wa vitu. Polisi pia imewataka wananchi kushirikiana na polisi katika kutekeleza majukumu yao.

Na anaongeza

لشرطة تنفي في بيانها ليلة امس استخدام الرصاص المطاطي او الحي, صح الاصابات امبارح كانت من وحي خيال المواطن ‎‫#السودان_ينتفض‬‏
@S_Elwardany: Katika tamko la jana usiku, polisi wamekanusha kutumia risasi za mpira au zile za moto. Sawa! Kwa hiyo majeruhi tuliowaona jana wametokana na hisia zetu

Yousif Elmahdi anathibitisha:

@Usiful_ME: Kwa hiyo, itakuwa nilifikiri tu kwamba nilikuwa karibu na mtu aliyepigwa risasi ya mpira mguuni na mwingine aliyetupwa kwenye gari dogo la wazi lililokuwa kwenye mwendo

Watumiaji wa mtandao wanafuatilia yanayoendelea nchini Sudani kwa karibu, kufuatia tetesi kwamba serikali ya Sudani inakusudia kukata mtandao wa Intaneto – tishio linalokumbushia jaribio la Misri kuwanyamazisha wanaharakati na kudhibiti mapinduzi yaliyotokea Januari 25 wakati serikali ilipoondoa uwezekano wa wananchi kutumia mtandao mnamo Januari 27.

Anuani ya mtandao wa twita ya Ubalozi wa Marekani mjini Khartoum leo imetoa tamko:

@USembassykrt: Upatikanaji wa intanenti na pengine simu za mkononi zinaweza kuwa na matatizo ya upatikanaji au kutokupatikana kabisa nchini humu kufuatia upinzani wa umma dhidi ya serikali na maandamano yanayoendelea katika mji mkuu wa nchi hii.

Inavyoonekana, kufuatia hali inayoendelea katika nchi za kiarabu, ni intaneti na ongezeko la matumizi ya vyombo vya habari vya kiraia, ndivyo vinavyobeba lawama kwa kuchochea mapinduzi yanayoendelea katika nchi za Kiarabu na wala sio udikteta, udhalimu na uvunjifu wa haki za binadamu unaoendelea katika nchi hizo.

Wakati huo huo, tawala za ki-Arabu zinaonekana kuwa na kinga ya kifunza kutokana na yaliyowakumba majirani zao.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.