Pakistani: Buriani Mehdi Hassan; Mfano wa kuigwa wa Ghazal.

Mehdi Hassan Khan ambaye alijulikana kama ‘Mfalme Ghazal’ alifariki jumatano ya tarehe 13, Juni, 2012 baada ya kuugua kwa muda mrefu katika hospitali ya jiji la Karachi nchini Pakistan. Mwimbaji huyo wa Ghazal, aliyekuwa na umri wa miaka 84, alikuwa akiugua kwa takribani miaka 12.

Baada ya kifo chake, ‘MehdiHassan’, amekuwa akitawala sana katika mtandao wa Twita katika nchi za Pakistan na India. Mamia ya mashabiki wake, wakiwemo waimbaji, watu maarufu, na wanasiasa waliotoa salamu za rambirambi na heshima zao kwa mwimbaji huyo maarufu. Mashabiki wake pia wamekuwa wakiweka katika mitandao mbalimbali ya kijamii nyimbo zake za Ghazal zilizowahi kuwa maarufu.

Waziri mkuu wa India Manmohan Singh ameandika katika ukurasa wake wa Twita akionesha huzuni yake::

@PMOIndia: “ushawishi wa mapenzi yake kwa ushairi wa Urdu na kutayarishwa kwake mapema katika utamaduni wa Dhrupad umemzawadia nafasi muhimu sana katika ulimwengu wa muziki”

Muigizaji maarufu wa Kihindi Shahrukh Khan katika ukurasa wake wa Twita anaeleza ni kwa namna gani anavyomkumbuka mwimbaji mashuhuri Ghazal:

@imsrk: “Ninakumbuka kipindi ambacho mama yangu alikuwa akipika katika jiko lililojaa masizi huku mvua ikinyesha, sauti ya Mehdi Hassan ilikuwa ikitumbuiza kupitia redio kaseti”.

Mehdi Hassan Khan

Screenshot from the video : Roz kehta hoon bhool jaon by KhurramDBG

Mwimbaji Lata Mangeshkar alitoa salamu za rambirambi kwa familia ya Mehdi Hassan alipoongea na vyombo vya habari na alisema kuwa kifo chake ni pigo kubwa katika tasnia ya muziki.

Asif Noorani katika blogu ya Dawn anasema:

Mehdi Hassan amefariki, lakini sihuzuniki. Usinilaani kwa kuwa ninasema nimepata tulizo, kifo chake kimekuwa ni mwisho wa mateso aliyoyapata kwa miaka 10. kumshuhudia akiwa amelala, asiyejiweza wala kuongea, akiteseka kwa maumivu, achilia mbali ngozi yake iliyo na vidonda, ilikuwa ni hali isiyozoeleka

Adil Omar (@Adil_Omar) katika ukurasa wake wa Twita anasema:

@Adil_Omar:Siwezi kudanganya kuwa nilikuwa nausikiliza muziki wake, lakini nilikuwa nafahamu fika thamani na mchango wake. Pumzika kwa amani Mehdi Hassan.

Mwimbaji Talat Aziz, anaelezea hisia zake:

Ninajisikia mwenye huzuni kupita kiasi. Nilikuwa mwanafunzi wake, mara nyingi nilikuwa naye. Kwangu mimi alikuwa ni nyota. Ninakosa cha kusema kufuatia kifo chake. Alikuwa hazina kubwa kwa ulimwengu wa Ghazal. Pamaja na kuwa ni muda mrefu ulipita bila yeye kuimba, lakini atakumbukwa. Hapatatokea tena Mehdi Hassan mwingine.

Ipitie tanzia ya Fawad kwa Mehdi Hassan, ambaye anamchukulia kama mwimbaji wa enzi asiye na mfano katika Asia ya kusini.

1 maoni

jiunge na Mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.