Habari kutoka Juni, 2012
Ethiopia: Ardhi, Historia na Haki katika Eneo la Gambella
Wanaharakati wa masuala ya ardhi wanatumia hati ya malalamiko ya mtandao, mtandao wa facebook na twita kufanya kampeni dhidi ya unyang’anyi wa ardhi nchini Ethiopia. Inaarifiwa kwamba wanakijiji kwenye jimbo msikini zaidi nchini humo, Gambella, wanalazimishwa kuhamia kwenye vijiji vilivyobuniwa na serikali ili kuwapisha wanaoitwa 'wawekezaji' wakubwa.
Misri: Maandamano ya Kukomesha Udhalilishaji wa Kijinsia Yavamiwa
Maandamano kudai kukomeshwa kwa udhalilishaji wa kijinsia yaligeuka kuwa shubiri baada ya wanawake waliokuwa wanahusika nayo kuvamiwa na kundi la wanaume wenye hasira kwenye viwanja vya Tahrir leo(June 8, 2012). Watu walioshuhudia tukio hilo walielezea maoni yao kupitia twita.
Kenya: Intani walipwe au wasilipwe?
Mada hapa ni kuhusu kama inafaaa au haifai kwa intani kulipwa,mjadala ulioanzishwa na @RobertAlai.
Brazili: Jarida Lawapa Nafasi Wasio na Makazi
Jarida la Ocas linalosambazwa katika mitaa ya mjini São Paulo pamoja na Rio de Janeiro tangu 2002, ni jarida ambalo husheheni habari ambazo hulitofautisha na vyombo vikuu vya habari nchini Brazil. Na linakwenda zaidi ya hapo. Aidha huwapa mwanzo mpya na fursa za kazi watu ambao hawana makazi na ambao wamo katika hatari ya kuangamia kijamii.
Zambia Yapanga Bei ya Mahindi kwa Mara Nyingine, Yaikasirisha Benki ya Dunia
Kupanda kwa bei ya mahindi, chakula kikuu nchini Zambia kumesababisha raia kufanya ghasia na hata kusababisha jeshi kuingilia kati. Pamoja na tahadhari iliyotolewa na benki ya dunia kwamba hatua hiyo ingeathiri sekta ya kilimo, watawala wa nchi hiyo wameendelea kupanga bei ya unga wa mahindi.
Kenya: Wanaharakati wapigana vita dhidi ya ufisadi kwa intaneti
I Paid a Bribe ni njia mojawapo inayotumiwa na wanaharakati dhidi ya ufisadi nchini, kwa kutumia teknolojia mpya ili kuwawezesha kupata ripoti za utoaji wa hongo.' I paid a Bribe' imefuatia muundo wa ‘India Anti-Corruption Portal (IPAB)' na ni ushirkiano kati ya IPAB na Wamani Trust ya Kenya ili kuleta IPAB katika Afrika Mashariki na Kati.
Kitabu kipya cha michezo ya watoto kutoka nchi mbalimbali
Blogu changamfu la Kimataifa, PocketCultures limechapisha limechapisha kitabu kuhusu michezo kumi na tano ya watoto kutoka nchi mbalimbali na amabayo inaweza kuchezwa kwa urahisi na msomaji. Kitabu kinaitwa ‘Games for Kids of the World’ na kinaweza kupatikana kwa bure kwenye iPad, Mac au kwenye kompyuta.
Marekani: Kumbukumbu la Walters Art lachapisha Mkusanyiko wa Picha
Jumba la Kumbukumbu la The Walters Art lililoko Baltimore, Maryland limechapisha zaidi ya picha elfu kumi na tisa kwenye mkusanyiko wa Wikimedia Commons na kuziweka chini ya leseni Creative-Commons. Jumba lenyewe lina mkusanyiko wa michoro kutoka Roma na Ulaya.
Uganda: Je, Uganda inageuka kuwa dola ya kifalme?
Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni amekuwa madarakani tangu mwaka 1986. Majuma machache yaliyopita, wananchi walianza kudodosa habari za nani hasa atamrithi kama ataamua kutokugombea kwa awamu ya nne mwaka 2016. Tetesi zinadai kwamba rais anamwunga mkono mkewe, Waziri wa mambo ya Karamoja kurithi kiti cha rais.
Kenya: Habari za Mlipuko Jijini Nairobi Zatawala Mijadala ya Twita
Kufuatia mlipuko mkubwa ulioathiri vibaya mtaa mkubwa wa Nairobi, Moi Avenue, wakenya na marafiki wa Kenya walitumia mtandao wa twita kuhabarishana, na kusambaza taarifa, kushauriana na kujadili tukio hilo baya.