Misri: Yatambulisha Kipimio cha Morsi


Makala hii ni miongoni mwa makala zetu maalumu kuhusiana na chaguzi za Misri 2011/2012.

Tarehe 24 Juni, raisi mpya wa Misri alitangazwa rasmi na jina lake ni Mohammed Morsi. Morsi wa chama cha Muslim Brotherhood, amekuwa raisi wa kwanza wa Misri kuchaguliwa kwa uchaguzi huru, na kama ilivyo kwa wagombea wengine wote, alikuwa na mikakati yake na ahadi ambazo wapiga kura walizikubali na kuamua kumchagua.

Lakini, watu wa Misri watawezaje kumbana Morsi awajibike katika kutimiza ahadi zake na kufuatilia mienendo ya namna ahadi zitakavyotimizwa? Wael Ghonim alitwiti kuhusu kitumizi kipya kwa ajili ya kuhakikisha Morsi anawajibika kutimiza ahadi zake na kufuatilia kila hatua ya namna ya utimizaji wa ahadi hizo:

@Ghonim: Kinafuatilia utendaji wa Morsi (Raisi mpya mteule wa Misri): http://www.morsimeter.com (via @ezzatkamel)

MorsiMeter, Tracking the performance of Morsi, the newly elected president of Egypt

Kipimio cha Morsi, kinafuatilia utendaji wa Morsi, raisi mpya mteule wa Misri.


Kitumizi hiki kimebuniwa na Zabatak, (@Zabatak),ni mkakati usio wa kimaslahi wenye lengo la kuifanya Misri isiwe na hongo, wala isiwe na rushwa na iwe salama. Na katika ukurasa wa Facebook, wa kipimio cha Morsi,wanaelezea kitumizi hiki kama ifuatavyo[ar]:

هذه محاولة لتوثيق ومراقبة أداء الرئيس المصري المنتخب محمد مرسي وفيها سيتم مراقبة ماتم انجازه وفق ما أقرّه د.محمد مرسي في برنامجه أول مائة يوم.
Huu ni mkakati wa kurekodi na kufuatilia utendaji wa raisi mpya wa Misri, Mohammed Morsi, na tutafuatilia kila litakalotimizwa kwa yale yote aliyoyaahidi katika mpango wake kwa muda wa siku 100 za kwanza akiwa madarakani.

Watumiaji wa mtandao Misri walitoa mitizamo na mawazo yao kuhusiana na kipimio hiki katika Twita kama ifuatavyo:

@MagedBk: kazi nzuri sana! http://Morsimeter.com

@omarkamel: Kipimio cha Morsi si wazo baya. Lakini lazima pia kipime tunawazaje vizuri kwa namna ambavyo mawazo haya yaanze. Mpango wa ulinzi unakera.

@AbdoRepublic: Ni wazo zuri sana la kupima utendaji wa Morsi. Kwa heri udikteta.

Makala hii ni miongoni mwa makala zetu maalumu kuhusiana na chaguzi za Misri 2011/2012.

1 maoni

jiunge na Mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.