Kenya: Intani walipwe au wasilipwe?

Mwana-Twitter @Robert Alai alianzisha mjadala uliozua hisia nyingi tarehe 14 Mei, 2012 kuhusu umuhimu wa kampuni kuwalipa intani (wanafunzi walio kwenye mafunzo kazini) wao. Aliwahimiza wana-Twitter wengine kuuliza kampuni kama wanawalipa intani wao.

@RobertAlai: Kama wewe ni intani na unahisi kawa unadhulumiwa, tafadhali tuma baruapepe kwa  alai @ techmtaa.com. Hebu tuulize #Je, mnawalipa intani wenu ?

Wana-Twitter walimwunga mkono haraka wakitetea intani:

@madonah12: #PayInterns  ndio mwenendo bora zaidi. Ni muhimu kuwa intani  wapate hela za chakula cha mchana, nauli na pesa kidogo za mfukoni.cc @RobertAlai Kazi njema

Bendera inayowatetea intani. Picha kwa hisani ya: Jeff Howard Flickr account (CC BY-NC-SA 2.0)

@tyrus_: Aye! Mbona hizi kampuni za Kenya zinye anwani ya Twitter ambazo hutuma twiti za “Habari za asubuhi na usiku mwema” na ambazo huuza bidhaa zao kupitia njia hii hawajibu kitu

@RobertAlai: Intani lazima walipwe. Kila mtu asimamie haki zake na mtaona kuwa kampuni zinaweza kuwalipa.

@TheMacharia: Nashindwa kuelewa, ni kampuni ngapi kati ya hizo huwalipa intani? Je, ni ngapi wamewaajiri intani na sio tu kuwachagua?

@mainneli: Intani walipwe kwani wanafanya kazi sawa kama wafanyakazi wengine, tuache kuwanyanyasa #Payinterns

@tkb: @kainvestor @Worldbank kuwaalika watu wiki ni sawa na @Wikipedia ambao hawawalipi intani. Chukueni mifano mizuri ya kimataifa ambapo kila kitu kinafanywa kwa uwazi.

@B_Oyigo: @RobertAlai Jamii Telecom Limited wanalipa intani kati ya shilingi elfu kumi na elfu kumi na tano.

@KenyaPolice: Jeshi la Polisi Kenya haliungi mkono kunyanyaswa kwa  wafanyakazi wa Kenya na wanawalipa intani wao.

Wengine walitetea kampuni ambazo haziwalipi intani wake:

@Kkaaria: Intani, miaka mitano tangu muanze kazi, mtatambua kuwa mlikuwa hamjui mambo mengi. Kuweni na subira.

@TerryanneChebet: maoni yangu ni kuwa wasilipwe lakini wapewe pesa za nauli na chakula cha mchana

@mainaalex: ati intani walipwe, kwa kazi gani? Kama wao wanajua mengi wanafaa waanzishe kampuni zao.

@Kamungah: @MediaMK intani wanasaidia, kampuni inasaidika wakati  ambapo intani  anapata ujuzi wa kazi ambapo kila mtu ananufaika. Waajiri wengine wanawapa hata nafasi ya kufanyiwa mahojiano ili waweze kuwaajiri kabisa.

Wanablogu nao wamejitosa kwenye mdahalo huu. Mwanablogu  Dennis Matara alisema kuwa sheria za kazi zimesisitiza kuwa intani wanafaa kulipwa baada ya kufanya kazi kwa muda wa miezi mitatu.

Lazima tuamke. Umekuwa intani kwa zaidi ya miezi mitatu? Amka. Sheria za kazi zinasema vizuri sana kuwa  kampuni ambayo inakuajiri kama intani haina budi kukutendea kama wafanyakazi wengine, wakulipe na upate siku za likizo kama wengine, miongoni mwa stahili nyingine. Kama hawawezi kufanya hivo, basi siku yako ya mwisho kwenye kampuni hiyo inafaa kuwa siku ya mwisho wa mwezi wa tatu huko.

Ni kweli kuwa intani wengine wanaamua kubaki katika kampuni zaida ya muda wao ili waonekane kuwa wazuri ili kupata nafasi za kazi. Hapo ni sawa, lakini kama kampuni inakuhitaji sana lazima wakuajiri. Waajiri wengi wanajua kuwa wengi wa intani hawa huwa wametoka moja kwa moja toka shuleni, hawana hata nauli lakini bado wanawanyanyasa.

Nairobi Wire iliandika haya:

Kampuni zinazowalipa intani ni chache na  zinawalipa pesa kidogo sana. Kwa kupitia tweets za watu, KCB, EABL, CIC, KPLC,KBC,NMG, RMS na Standard Group wametajwa kuwa wanyanyasaji wakubwa. Equity imesemekana hutumia huduma kwa jamii kama sababu yao ya kuwadhulumu wafanyikazi. KBC ndio mbaya zaidi kwani lazima intani alipe ili apate nafasi huko.
Pia kumekuwa na intani wanaoteta kuwa wanatumiwa kingono.

Hili ni swala moja  la kuvutia ambalo nimeona likiongelewa Twitter kwa muda mrefu. Mara mingi watu huwa wanateta kuhusu Kenya Power.

Suala hili limeibua mjadala mkubwa na kuwa na mvuto wa pekee, ndani ya dakika moja zimetumwa twiti takriban mia moja na hamsini, hili ni tukizingatia kuwa ni Kenya Pekee. Mashirika mengi yamejitetea kuhusu madai kuwa hawawalipi intani. KCB, walisema kuwa hawapati pesa zozote kutoka kwa intani na kuwa intani wanalipwa kiasi kidogo cha fedha lakini ambacho kiko juu ya wastani kulinganisha na sekta nyingine.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.