India: Kipindi cha Runinga cha Aamir Khan Chaweka Wazi Masuala ya Kijamii

Kipindi kipya cha mazungumzo ya  runinga ya India Kwa jina  Satyamev Jayate (Ukweli pekee utatawala) kilicho peperushwa tarehe 6,Mei, 2012 kiliiacha nchi hiyo kwenye hali ya mshangao. Mtanganzaji wake ambaye ni muigizaji na mtengeneza filamu wa Bollywood, Aamir Khan anaweka wazi miiko na maswala mengine motomoto ya kijamii ambayo yanawavutia na kuwanasa WaHindi wengi. Mamilioni ya watanzamaji wa kusini mwa Asia huganda kwenye runinga zao kila jumapili wakati kipindi hicho kinapoenda hewani kupitia mitandao kadhaa ya binafsi na pia ile ya umma kwa pamoja.

Amreekan Desi alitizama sehemu ya kwanza iliyozungumzia “mauaji ya watoto wa kike ambao bado hawajazaliwa” [yaani vichanga vilivyo tumboni mwa mama] na hizi ndizo hisia zake:

Maisha ya kila siku yanatupa nafasi kufunga macho yetu na kujifanya kana kwamba hakuna shida.Kipindi hiki kinatuletea [masuala nyeti] moja kwa moja kwenye sebule zetu kikiwa na maelezo ya kweli pamoja na tarakimu zake. Hatuwezi kuendelea kujifanya kwamba hizi ni tatizo la mtu mwingine. Ni tatizo letu

Maisha na Nyakati za Mwenye Nyumba wa KiHindi(The Life and Times of an Indian Homemaker)inaleta sehemu ya barua pepe ya shujaa aliyeponea mateso ya ngono utotoni ambaye pia alitizama sehemu ya pili ya Swala hilo:

Satyamev Jayate alitonesha kidonda ndugu. Ukisikiliza simulizi za walioponea mateso hayo kumbukumbu za kitambo zinarejea. Siri mbaya iliyofichwa ndani ya moyo, jambo ambalo limebadilisha utu wangu katika maisha na kunifanya jinsi nilivyo sasa. Ninapozungumza na  mwanangu wa kiume nagundua kuwa haidhuru ni kwa jinsi gani mazingira ya nyumbani yalivyo, kuna mambo mengine yanadumaza  maendeleo na afya ya mtoto. Mateso kwa mtoto si ati kunatokea tu kwenye nyumba ambazo zimefungwa  na hisia za kijamii na kadhalika, mateso hayo hufanywa mahala ambapo mtoto yupo kwenye mazingara mabayo hawezi kujitetea. Hao wanaotesa [kingono] huwalenga watoto ambao ni shabaha rahisi, huku wakijua kila kitu kuhusu wanapotokea na namna wwanavyofikiri, na kukonga imani ya watoto hao na kuwapa mazingira ya kuwafariji ambayo mara nyingine watoto hao hawanayo. Mimi ni shujaa niliyeponea.

Na baada ya miaka karibu 30, nimeamua kujitokeza na kusema wazi.

Kuna hisia nyingi kwenye ulimwengu wa blogu. Kikombe nusu cha chai anaelezea simulizi yake ya kutendewa vibaya kwenye hospitali, iliyohamasishwa na kipindi cha  Aamir juu ya “Ufisadi kwenye mfumo wa afya nchini India”; Ugich Konitari anaeleza kuwa mfanyakazi wake wa ndani wake anaweza kuhusisha hadithi ya binti zake na kesi ya kwenye onyesho la Satyamev Jayate kuhusu” Mahari”. Mahesh Murthy anaombea Satyamev Jayate ingelikuwa kundi la harakati za kijamii linaloungwa mkono na runinga. Kuna majadiliano mengi kwenye mtandao wa Twita kuhusu kipindi hiki:

priyasaha1: nilitizama sehemu ya kwanza ya Satyamev Jayate jana, kwa kifupi kilikuwa safi sana. Sasa najua kwanini watu wanakipenda kipindi hiki .

Aamir Khan. Picha na mtumiaji wa Flickr gdcgraphics. CC BY-SA

Kipindi hiki hakijakosa utata. Baada ya onyesho kuhusu vitendo potofu vya Madaktari, Jumuiya ya Madaktari wa India walilalamika kwamba walichafuliwa jina na kutaka waombwe msamaha lakini Aamir alitetea hatua yakeakisisitixa kuwa hataomba msamaha.Ilidaiwa kuwa Aamir Khan upokea malipo ya juu ya  Rs. 3 crore (Dola za Kimarekani 600,000) kwa kila onyesho la kipindi kwani utengenezaji wa kipindi hiki unagharimu sana. Hata hivyo Astitwa  alitetea Satyamev Jayate na kuwapa jibu wanao mkosoa Aamir Khan:

Hata kama asilimia ni 1% ya taifa la watu laki 121 inaweza kubadili mienendo yake, nafikiri  harakati za Aamir Khan (za ujenzi wa maadili) na vituko vyake vya kuvutia biashara vitaendelea kutuvutia. Mwasemaje, India?

Debolina Raja Gupta  anaorodhesha ratiba ya mada zilizoangazwa kwenye kipindi cha Satyamev Jayate kufikia tarehe 10 ,Juni, 2012:

1. Sehemu ya 1 – mauaji ya vitoto vichanga vya kike vingali kwenye matumbo ya mama zao
2 Sehemu ya. 2 -Mateso ya Kingono kwa Watoto
3. Sehemu ya 3 -Mahari
4. Sehemu ya 4 – Ufisadi Kwenye Sekta ya Afya India
5.Sehemu ya 5 – Mauaji kwa Ajili ya Kutunza Heshima
6.Sehemu ya 6 – Matatizo Yanayowakabili Walemavu kwa katika Jamii Yetu

Anafikiri kipindi kinafaa kupewa sifa, sio lawama:

Nalithamini wazo kwamba hatimaye, watazamaji runinga wa India wanatinzama vipindi viingine zaidi ya mifululizo ya saas-bahu (Mama Mkwe na mkwe), au mifululizo mingine kwa ujumla, ambayo ni sawa na mafurushi ya vinyesi.

Indi.ca Kutoka Sri Lanka anakisifu Kipindi:

Pamoja na matatizo mengi ya kijamii, aibu yote hubebwa na muadhiriwa ambaye hunyanyasika na ukimya [uliopo juu ya masuala hayo].Kuuvunja ukimya huo kunaweza kuleta mabadiliko, na ni vyema kwamba Khan anatumia umaarufu wake vyema. Kadhalika ni kipindi cha runinga chenye ushawishi wa papo hapo.

Debolina Anamalizia:

Aamir ameweza kutuchangamsha na kututetemesha sisi wote, lakini ni kwa kiasi gani masuala hayo yanatugusa na tunafanya nini juu yake ni mambo ambayo bado tunasubiri kuyaona.

2 maoni

jiunge na Mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.