Brazili: Jarida Lawapa Nafasi Wasio na Makazi

Inajulikana wazi bila hata kutamka kwamba watu wengi wanapendelea kupata habari kutoka vyanzo vingine zaidi ya televisheni au magazeti makuu.Huko Marekani ya Latini, Ulaya, Asia – na kote duniani, kwa kweli- mambo yamekuwa hivi tangu mwanzo wa Milenia: habari bora zaidi, maoni yaliyo na msingi bora na ufafanuzi husika vinapatikana kwenye blogu na kwenye mitandao ya kijamii, na pia katika magazeti ya vyuo vikuu na mitandao ya wanaharakati.

Revista Ocas [pt] ni mojawapo ya majarida hayo, linalosheheni habari ambazo zinalitenga na vyombo vikuu vya habari nchini Brazili. Kwa kweli, inaenda zaidi ya hapo. Ufupisho wa Organização Civil de Ação Social (Asasi ya Harakati za Kiraia), jarida hilo ni mradi wa kujitolea uliotiwa motisha na magazeti ya mitaani toka kote duniani, hasa lile la The Big Issue, ambalo limekuwa likisambazwa jijini London tokea miaka ya 1990.

Waanzilishi wa Revista Ocas walifuata mfano huo nchini Brazili kwa kuunda nafasi za kazi kwa watu walio katika hali ya hatari kijamii. Zaidi ya hivyo, kutokana na kuelewa umuhimu wa watu wanaojitolea nchini humo, International Network Street Pappers (INSP) ilisaidia juhudi za  kuchapisha jarida ambalo linasambazwa kwa watu wasio na makazi. Naam umesoma vyema -watu wasio na makazi. Revista Ocas limesambazwa katika barabara za São Paulo na Rio de Janeiro tangu mwaka 2002.

Revista Ocas issue 61: the subheading reads 'Invest in a human being'. Illustration by Alex Senna, shared on Flickr (CC BY-NC-SA 2.0)

Revista Ocas toleo la 61: kichwa cha habari kinasomeka reads 'Wekeza kwa Mwanadamu'. Mchoro na Alex Senna, uliowekwa kwenye Flickr (CC BY-NC-SA 2.0)

Wahariri wa toleo wanaeleza [pt]:

Lengo ni kuwapa wauzaji nafasi ya kurejesha kujiamini kwao, na hivyo kuwasaidia watu binafsi kuwa wakala wao wenyewe wa mabadiliko, hivyo basi Revista ni ngazi tu katika njia hiyo, na si mwisho wa safari hiyo.

André Maleronka, ambaye anahusika na kutangaza jarida katika blogu ya Overmundo [pt] anaongeza:

Katika toleo la kuchapisha, Jarida hilo linawatumia waandishi wazito na mchanganyiko wa hadithi na taalam za utamaduni, ripoti za watu wasio na makazi, waliokuwa wakiishi mitaani pamoja na uchambuzi wa sera za mitaani.
 Video [pt] iliyotengenzwa na shirika hilo inaelezea Revista Ocas inamaanisha nini kwa wale wanaoliandika na kuliuza:

Jarida linagharimu reais 4 [takriban dola mbili za Marekani], reais 3 [dola na senti tano za Kimarekani] ambazo huwaendea wauzaji moja kwa moja, zinazosalia real 1 [dola 0.5] hupelekwa kwa Ocas na wauzaji wenyewe – uhusiano wa imani ambao wengine hawajawahi kuupata kutoka kwa waajiri wengine.  Marisa Suraci, ambaye ameuza Ocas tangu lizinduliwe aligundua tena utayari wake kufanya kazi:

Ni ubaguzi wa namna gani ambao waajiri wanaufanya ikiwa hawatupatii fursa za kazi? Wale ambao wana uhitaji wanaweza kuwa wamesoma na kufanya kazi kadri walivyoweza huko nyuma. Ocas, si kama waajiri wengine. Zaidi ya kunisaidia kukimu mahitaji ya kifedha, pia ilinisaidia kiafya. Nilizidi kujiboresha kadri nilivyoongea na  watu, nikiuza jarida, na nilipokelewa vyema…

Blogu ya Retinas Urbanas [pt] inaeleza jinsi Ocas inavyopata fedha zake na umuhimu wa mradi huu:

Chanzo pekee cha mapato ya Ocas ni pesa inazopewa na wauzaji wa jarida, kadhalika kupitia kwa matangazo na michango. Pia wanafanya warsha za kibunifu kwa watu wasio na makazi na mara kwa mara hugundua wachoraji au waandishi wapya. Kwa juhudi hizi wanaruhusu mahitaji ya kila mtu kueleweka, kama ni kukosa nyaraka, au matibabu ya uzoefu wa dawa za kulevya, na kuwasaidia  kujiboresha kupitia  mtandao wa washirika wa sekta ya tatu.

Kivuli cha ugumu wa kupata hela umegubika matoleo ya hivi karibuni ya jarida hilo, na mjini São Paulo na Rio de Janeiro, miji mikubwa ya  Brazili ambako linasambazwa, tayari kuna upungufu wa wauzaji. Toleo la mwisho la 80, lilichapishwa shukrani kwa mradi wa michango wa kijamii Catarse [pt], ulioiwezesha Ocas kupata reais 8,880 [takriban dola  elfu nne na mia nne za marekani] kupitia michango ya watu themanini na tisa na mashirika kwa siku 60.Ocas, 80th edition: 'Nine years. 79 editions. 330,000 copies sold on the streets. Hundreds of people helped.'

Ocas, 80th edition:

Jarida lina  blogu [pt] na ukurasa wa Facebook, na linatafuta watu watakaojitolea [pt] na wachangiaji [pt].

Ombi la kwenye mtandao [pt] linaeleza umuhimu wa jarida hili na linatafuta njia ya kuhakikisha kuwa linaendelea. Mchakato huo (wa ombi la kwenye mtandao) unaipatia Ocas mamlaka ya kuendelea kuongea na mashirika mengine, na wauzaji wanafurahia idadi iliyoongezeka ya watu wanaolitambua jarida hilo mitaani. Wabrazili wanaojulikana na haiba ya kimataifa wanapamba kurasa za mbele za jarida,  na jarida linaongelea  mada muhimu huku likiwa limesimama katika jukwaa linaloamini kuwa habari ndio mikono ya kila mwananchi.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.