Mnamo Aprili 8 “Anonymous Tunisia” kikundi kisichotambulisha majina ya wanachama wao nchini Tunisia (ambacho kinadai kuwa na uhusiano na kikundi cha watu “wasiojitambulisha” [1]) waingiliao mawasiliano ya watu kiliingilia mawasiliano [2] the ya barua pepe ya waziri mkuu wa Tunisia Hamadi Jebali [3]. Vuguvugu hilo lilipewa jina la utani la (“Achana na Tunisia yangu”) ambayo ni sehemu ya kampeni kuu iitwayo “Operesheni Rejeza Tunisia”.
Katika mkesha wa mapinduzi mwaka 2011 wanachama wa kikundi hicho cha “wasiojitambulisha” waliotawanyika duniani kote walishambulia tovuti kadhaa za serikali katika kile kilichoitwa Operation Tunisia [5]. Mmoja wao hivi2,725 emails [6] wanachama wa chama tawala cha nchi hiyo cha Ennahda mtandaoni [7], ikiwa ni pamoja na mawasiliano ya waziri mkuu.
Namba za simu [8] zinazomilikiwa na maafisa nyeti wa serikali tangu wakati huo zimekuwa zikisambazwa katika kurasa za facebook. Serikali imekamatwa pabaya na mpaka sasa haijaweza kujibu chochote. Wakati huo huo, raia watumiao mtandao wamegawanyika kuhusu ufanisi wa hatua hiyo.
Bassem Meddeb katika hali ya kusisimuka, alituma ujumbe kupitia mtandao wa twita kuhusu kuperuzi maelfu ya barua pepe:
@bmeddeb [9]: Finalement #Anonymous nous a engagé comme détectives! #jbelileaks
Hmida Ben Jemmaa aliandika kwa kejeli:
@HBJtn [10]: Après le #JbeliLeaks, le bureau politique d'Ennahdha décide de correspondre avec des… pigeons voyageurs.
Hata hivyo, baadhi ya watumiaji wa twita walipingana na zoezi hilo la kuingilia mawasiliano ya watu.
Hmida Ben Jemmaa aliandika akipinga mashambulizi hayo, na kuongeza: [12]:
Mwanafunzi wa Utabibu Amine Ghrabi alihoji mantiki ya Zoezi hilo linalofanywa na “watu wasiojitambulisha” na kutuma ujumbe:
@HendrixTN [13]: Petite pensée à tous ceux qui ont gâché leur matinée dominicale à fouiller la boite mail d'un incompétent confirmé ! #JbeliLeaks
Alkimia alituma ujumbe huu:
Na akaongeza:
@alkimia5550 [14]: Anonymous a menacé les Islamistes depuis qq mois.Il ne serait pas malin s'il n'a pas nettoyé
Mwanafunzi Imed Laaridh, anayeunga mkono chama tawala cha Ennahda, alituma ujumbe kwamba angegoma:
@ImedLaaridh [15]: On est peut être parti pour un tour de piratage réciproque. On trouvera de quoi passer le temps.. #TnPolitics #JbeliLeaks
Video ifatayo [Fr] iliwekwa na kikundi hicho. Mwanachama wa kundi hilo anazungumza kuhusu kuvuja kwa barua za waziri mkuu, na makarabrasha yanayotarajiwa zaidi muda mfupi ujao: