- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

Ajentina: Dokumentari Kuhusu Wenyeji wa Mjini Yatafuta Tafsiri ya Maandishi

Mada za Habari: Amerika Kusini, Ajentina, Filamu, Habari za wenyeji, Lugha, Sanaa na Utamaduni, Uandishi wa Habari za Kiraia, Ubaguzi wa Rangi

Makala hii ni sehemu ya Habari zetu maalumu kuhusu Haki za Wenyeji [1].
Dokumentari iitwayo Runa Kuti iliyoshirikishwa katika mradi wa Haki miliki wa “Creative Commons” [2] kuhusu kutambuliwa kwa wananchi waliotokana na uzao wa wenyeji wa zamani walioishi mjini katika jiji la Buenos Aires, inatafuta watu wa kujitolea kusaidia kuiwekea video hiyo tafsiri ya maandishi kwenda katika lugha za asili za Ajentina kama ki-Quechua, ki-Aymara, -kiMapuche na ki-Guaraní pamoja na ki-Kiingereza.

Katika blogu yao, wameweka tangazo lao la kualika watu wanaopenda kujitolea [3]:

Quien quiera, tenga ganas, tiempo, ocio, curiosidad, computadora, internet y otros idiomas para apoyarnos se los agradeceremos añadiendolos a los créditos del documental y mandándoles buenas vibras, donde quiera que estemos y donde quiera que estén.

Todos los idiomas son bienvenidos pero guardamos un especial interés por el quechua, aymara y guaraní.

 

Yeyote anayetaka kushiriki zoezi hilo, anayejisikia kulipenda zoezi hilo, anao muda, na angependa kushiriki zoezi hilo kama sehemu ya vitu avipendavyo, kwa udadisi, ana kompyuta, mtandao wa intaneti na anajua lugha nyinginezo zinazoweza kutusaidia tunatawashukuru kwa kuwaongeza katika orodha ya watu watakaotambuliwa katika shukrani rasmi za videohiyo na kuwatumia zumari nzuri, popote tulipo na popote walipo.

Lugha zote zinakaribishwa ingawa kipaumbele chetu ni ki-Quechua, ki-Aymara na ki-Guaraní.

http://vimeo.com/32219379 [4]

Onyesho la awali (trela) [5] lina maandishi ya tafsiri ya ki-Hispania, ki-Faransa, ki-Kiingereza na ki-Reno, video kamili ya dokumentari hiyo [6] imetafsiwa kikamilifu kwa ki-Faransa.

http://vimeo.com/37754616 [7]

Makala hii ni sehemu ya Habari zetu maalumu kuhusu Haki za Wenyeji [1].