Mwanahabari Bladimir Sanchez ameshapata vitisho kwa maisha yake kwa kutengeneza video [en] inayoonyesha kufukuzwa kwa lazima kwa wakulima na wavuvi wanaopinga kutengenezwa kwa bwawa la kuzalisha umeme katika eneo la Huila, nchini Colombia mnamo tarehe 14 na 15 Februari. Takriban baada ya siku tatu, video hiyo imetazamwa na watu zaidi ya laki sita.
Katika Publimetro [es], Camilo Andrés García Cortés anasema kuwa video hii yaweza kuwa inafanya historia kwa kuwa video iliyotazamwa mara mengi zaidi nchini Colombia, kwa sababu ishapata kutazamwa mara laki tano baada ya masiku mawili tu. Video ambayo Serikali ya Colombia Haitaki Tuone [es] yaonyesha fujo inayotumiwa dhidi ya jamii mbili zilizoko ukingoni wa mto, ambazo zimetumia njia za amani kupinga kujengwa kwa bwawa hilo. Video hiyo pia inakusanya maoni na ushuhuda ya waliokumbana na vurugu hizo, pamoja na waliojeruhiwa.
Jamii zitakazoathiriwa zimepinga kujengwa kwa bwawa hili, kwani litawaacha bila jinsi ya kupata riziki yao kama mto utaelekezwa kwingine. Wakieleza jinsi waandamanaji walivyojeruhiwa, wanajamii na wanahabari waliopo katika eneo hilo wanaeleza kwamba hapakuwa na fujo dhidi ya wenye mamlaka, ilhali ya uwepo na vurugu, na polisi waliwazuia wanahabari, waangalizi wa amani na shirika za kupigania haki za kibinadamu kufika sehemu ambako maandamano yalikuwa yakiendelea.
La acción violenta se cumplió coordinadamente entre el Gobierno Nacional y Emgesa contra campesinos y pescadores inermes cuya única respuesta fue cogerse solidariamente de las manos para abrazar el río Magdalena o lanzarse al mismo, mientras recibían cargas de gases lacrimógenos y granadas de aturdimiento, ocasionando varios heridos, entre ellos, el obrero de construcción Luis Carlos Trujillo Obregón quien perdió su ojo derecho.
Katika mahojiano na Publimetro [es] Bladimir alizungumza kuhusu vitisho alivyopokea:
Recibí una llamada No aparece el número de la persona en el identificador (…) Me han enviado mensajes a mi correo. Me dicen que soy de las Farc, del ELN, que estoy atacando a la fuerza pública. Yo no soy nada de eso. Simplemente soy un realizador audiovisual que quiere mostrar la realidad de lo que pasa en el departamento del Huila.
Katika Ukurasa wake katika Facebook unaojulikana kama Zeitgeist Huila [es], Bladimir aliandika tarehe 23 Februari [es] kuwa amepokea simu kadhaa za kutisha, zingine zikiwa na vitisho kwa maisha yake.