Zambia 2011: Matukio Mawili Yaliyotikisa Taifa

Bila ya shaka, matukio mawili nchini Zambia yatatambuliwa kama matukio yaliyoitikisa nchi kama vile tetemeko la ardhi linavyotikisa. Tukio la kwanza lilikuwa ni kifo cha Rais wa pili wa Jamhuri , Frederick Chiluba, mmpigania haki za wafanyakazi ngangari, aliyegeuka kuwa mwanasiasa na ambaye alimshinda rais wa kwanza wa Zambia Dk Kenneth Kaunda ambaye alikuwa madarakani kwa miaka 27 na kuondolewa katika wadhifa huo kwenye uchaguzi wea kwanza wa vyama vingi baada ya miaka 17 ya ‘demokrasia’ ya chama kimoja.

Hivi ndivyo mwanablogu mmoja wa Zambia, Munshya, alivyomkumbuka Chiluba:

Huyu ni mtu asiyekuwa na elimu ya juu ya sekondari aliyefanya kazi kwa bidii ili kuweza kusoma kozi chache za cha daraja A ambazo baadaye alikubali kuwa aliziacha kando. Na zaidi, ili kwamba asishindwe na changamoto zilizomkabili, Chiluba alikwenda hata Tanzania kutafuta fursa. Na aliporudi nchini Zambia akiwa na umri kwenye miaka ya ishirini, alitafsiri ujuzi ujuzi alioupata alipokuwa akifanya kazi kwenye nyanja mkonge nchini Tanzania kwa manufaa. Alitumia ujasiri na kutokuwa na hofu kwake kuwa mlinzi wa wa wafanyakazi wenzake. Kwa kupitia chama cha wafanyakazi, Chiluba ambaye alikuwa na umbile dogo alipata nafasi ya kuongea na kutembea kama mtu mrefu kupita wote.

@ictjournalist aliandika ujumbe wa twita:

@ictjournalist: @GNdhlovu namkumbuka kama mtu ambaye alianzisha mapinduzi barani Afrika ambayo yameenea kila sehemu

Afriwoman alikuwa na huzuni kidogo:

@afriwoman: Nasikiliza stesheni za redio za Zambia, napitia picha za mazishi ya #Chiluba kwa hisani ya @QfmZambia . Sikumpenda lakini nina masikitiko kiasi

Tukio la pili lilikuwa ni kushindwa kwa chama tawala cha MMD baada ya kutimiza miaka 20 madarakani na miaka mitatu tu katika ofisi rais aliyekuwepo Rupiah Banda ambaye alishindwa na Michael Sata wa PF ambaye alikuwa katika jaribio lake la nne kugombea urais.

Baada ya kuchaguliwa, rais Sata, katika taktiki yake yake nyingine kabambe kisiasa, aliistua dunia pale alipomteua swahiba wake wa siku nyingi na makamu wa rais wa chama chake, Dk Guy Scott, mZambia mweupe ambaye amekuwa kwenye ulingo wa siasa nchini humo kwa zaidi ya miaka 20.

Akitoa maoni juu ya uteuzi wa Guy Scott, mtumiaji wa twita na mwanablogu wa Zambia @missbwalya alibaini:

@missbwalya: Zambia ndiyo nchi pekee ya kiAfrika yenye makamu wa rais Mzungu, Najiuliza hili litapokewa vipi na wale waAfrika wenye siasa kali “dhidi ya watu weupe”.

Makamu mpya wa rais wa Zambia Guy Scott. Picha kutoka tovuti ya chama tawala cha Patriotic Front.


Kifo cha Chiluba ambacho wananchi walikisikia kwanza kwa kupitia Twita, kililishtua taifa ambalo miaka mitatu tu kabla, lilimzika rais aliyekuwa madarakani, Levy Mwanawasa ambaye alifariki nchini Ufaransa baada ya kuzimia akiwa katika ziara ya kimataifa ya kikazi nchini Misri. Kifo cha Chiluba kiliondokea kuwa suala moto katika kampeni kwa chama cha MMD ambacho wanachama wake walitishia kumpiga Sata ikiwa angehudhuria mazishi ya aliyewahi kuwa kiongozi wake ambaye chini yake alitumikia siyo tu kama waziri bali pia kama katibu mkuu wa MMD.

Sata hakukanyaga katika eneo la mazishi kufuatia vitisho vya kumpiga vilivyotolewa na makada wa MMD lakini bila kutarajiwa alitokea katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Mulungushi ambapo mwili wa Chiluba ulilazwa na kutoa heshima zake za mwisho, huku akiutazama pamoja na raia wa kawaida, na kuwachukiza maafisa wa usalama ambao hawakujua cha kufanya na mtu huyu ambaye wakati huo alikuwa ni kiongozi wa upinzani ambaye ni wazi alikuwa katika uhusiano mbaya na Rais Banda.

Hadi wakati ambapo makada wanazi wa MMD walipofika ili kumshughulikia Sata, alikuwa amekwishaondoka Mulungushi. Taktiki hii pengine ni moja ambayo ilimuongezea ukubwa Sata katika fikra za wapiga kura watarajiwa. Jambo la kejeli, hata hivyo, ni kuwa Chiluba, kabla ya kifo chake, alijitangaza kuwa mshauri wa kisiasa wa Rais Banda na aliyeapa kuwa atazileta ngome za Sata vijijini kwenye kambi ya MMD.

Mashabiki katika lori wakisherehekea ushindi wa kiongozi wa upinzani Michael Sata wakati alipoapishwa kama rais wa tano wa Zambia. Picha na Owen Mayiza, haki miliki ya Demotix (23/12/2011).


Linalohusiana na kifo cha Chiluba lilikuwa ni uchaguzi wa rais ambao MMD ilikuwa na uhakika wa kushinda kutokana na kampeni yake iliyokuwa na fedha za kutosha dhidi ya mkakati wa kampeni yenye hali mbaya kifedha na ya chini chini ya PF ambayo ilitumia kauli mbiu ya “Donchi kubeba”, donchi ni neno lililopotoshwa la Kiingereza, don’t na kubeba ni kusema.

Serikali ya MMD ilijaribu kuzuia tmatokeo ya kura pale ilipokwa wazi kuwa mambo yalikuwa hayaendi njia yao lakini watumiaji wa mtandao waliokuwa hatua moja mbele walitoa matokeo kwa njia ya twita, Facebook na mitandao ya kijamii.

Rais Sata ameanzisha uchunguzi mkubwa wa matukio ya kifisadi yaliyofanywa katika utawala uliopita na ndani ya wiki chache baada ya uchunguzi kuanza, vitengo cya usama vilichimbua mabilioni ya Kwacha za Zambia kutoka katika shamba la waziri wa zamani. Mawaziri wengine kadhaa wamekamatwa ama mali zao ambazo zinashukiwa kupatikana isivyo halali zimechukuliwa. Pale upeo wa ufisadi ulipojulikana wazi, wananchi walianza kudai iondolewe kinga inayomlinda rais Banda asishitakiwe. .

Wanamtandao pia walijiuliza ikiwa rais aliyepita alijishtaki mwenyewe katika hotuba yake ya kuaga. Kwenye Facebook, Ghong Jhala aliuliza:

Unafikiri RB na wanawe watashitakiwa kwa jinai? Niliona ni jambo la ajabu pale aliposema kuwa “hawakutumia vibaya rasilimali za taifa huku wakiwa na ufahamu huo” je, ina maana kuwa walitumia vibaya rasilimali za taifa lakini hawakujua kuwa walikuwa wanafanya hivyo?

Wanamtandao wengi walichangia juu ya vita dhidi ya ufisadi:

@lwangamwilu: Baadhi ya watu kwa miujiza walipata utajiri katika miaka miaka 3 waliyokuwa madarakani, hebu waache wachunguzwe – Milupi #Zambia

@stevenputter: #Zambia, baiskeli 1000 “kwa matumizi binafsi” nilidhani ni Mungu peke yake ambaye anaweza kuwa sehemu zaidi ya moja kwa wakati mmoja, si ajabu wanachunguzwa

Pengine tugusie mdahalo wa Makubaliano ya Barotseland, ambao ulipamba moto mwaka 2011. Kwa muda mrefu ulichukuliwa kama suala lisilo na maana wakati wa miongo ya utawala wa chama kimoja, Barotseland iligeuka suala tata kisiasa mwaka 2011.

Watu wawili waliuwawa mwezi Januari 2011 baada kuzuka machafuko hukoMongu, mji mkuu wa jimbo la Magharibi baada ya kusimikwa tena kwa Mkataba wa Barotseland wa mwaka 1964. Baadhi ya wanaharakati wanadai kwamba Mkataba wa Barotseland unaruhusu kujitenga kutoka Zambia.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.