Venezuela: Ziara ya Mahmoud Ahmadinejad Yaibua Utata

Rais wa Iran, Mahmud Ahmadinejad, aliwasili nchini Venezuela siku ya Jumapili, tarehe 8 Januari, katika siku yake ya kwanza ya ziara itakayoendelea kwenye nchi za Nicaragua, Cuba na Ecuador. Ziara yake imechochea miitikio mikali kwenye mitandao ya kijamii, ambapo watumiaji wanahoji ikiwa uwepo wake huko unaweza kuwa na faida yoyote kwa taifa hilo.

Kwenye Twita, baadhi wanakosoa kuwepo kwa Ahmadinejad na mapokezi aliyopewa na serikali ya Venezuela. Luis Carlos Díaz (@LuisCarlos) [es] anaandika:

Dice mucho del Ministerio de la Mujer su no-pronunciamiento sobre la visita de Ahmadineyad

Kutotangaza kwake ziara hiyo ya Ahmadinejad kunaeleza mengi kuhusu Wizara ya wanawake

Mwanablogu Carlos Bauza (@CarlosBauza) [es] anapendekeza kwamba ziara ya Ahmadinejad inaweza kuathiri uchaguzi ujao wa Urais nchini Venezuela, wakati Garcilaso Pumar (@garcilasop) [es] anaandika kwenye twita:

Mahmud Ahmadinejad es un tirano retrogrado, asesino y misógino. Chávez es un imbécil que le ilusiona ser todo eso. #Coneldebidorespeto

Mahmud Ahmadinejad ni mtawala katili wa kizamani, mwuaji na mtu mwenye chuki kwa wanawake. Chavez ni mjinga anayeona sifa kuwa na tabia zote hizo #withallduerespect

Mahmoud Ahmadinejad, picha ya mtumiaji wa mtandao wa Flick Parmida Rahimi (CC BY 2.0)

Wengine wanatumia alama ya #FueraAhmadinejadDeVzlakumtaka Rais huyo wa Iran aondoke nchini humo. Mtumiaji @PericoRipeado24, kwa mfano, anakosoa mtazamo wa Ahmadinejad kuhusu haki:

#FueraAhmadinejadDeVzla Porque tu justicia se ve en la horca, cuando tu pueblo roba es para comer

#OndokaAhmedinejadVzla Kwa sababu haki kwako hufanyika kwa kunyonga, wakati watu wako huiba tu ili kupata mlo wao.

Wakati huo huo, watumiaji wa mtandao wanaomwunga mkono Rais Chavez walituma ujumbe kwenye twita kumpokea Ahmadinejad:

Basem Tajeldine (@BasemTajeldine): Merece un reconocimiento la valentía d Ahmadineyad al visitar Vzla, Cuba, Nicarg y Ecu, antes “patio trasero” d USA, hoy paises soberanos

Ujasiri wa Ahmadinejad kufanya ziara kwenye nchi za Venezuela, Cuba, Niacaragua na Ecuador unastahili kutambuliwa, jana [nchi hizi zilikuwa] “nchi za uani” za Marekani, leo [zimekuwa] nchi huru.

Justo Bustamante Ch. (@JustoBustamante): BIENVENIDO MAHMUD AHMADINEJAD PRESIDENTE REPÚBLICA ISLAMICA DE IRÁN Lider de la Revolución Iraní. LOS REVOLUCIONARIOS VENEZOLANOS te saludan

Karibu Mahmud Ahmadinejad Rais wa Jamuhuri ya Kiislamu ya Iran, kiongozi wa mapinduzi ya Iran. Wanamapinduzi wa ki-Venezuela wanakuheshimu.

Carlos R. Franco (@CarlosRFrancoM): Camarada Mahmud Ahmadinejad bienvenido a la tierra de Bolívar, patria libre, soberana y socialista… ¡Que chillen los escuálidos!

Komredi Mahmud Ahmadinejad karibu kwenye kwenye nchi ya Bolivar, nchi huru, yenye maamuzi yake na ya kijamaa…Hebu na wapinzani wapige kelele!

Hii ni ziara ya tano ya Ahmadinejad nchini Caracas. Baada ya kutania kuhusu “mabomu ya atomiki“, ziara yake iliisha siku ya Jumatatu, Januari 9 kwa kutia saini mfululizo wa makubaliano mengi ya pamoja, ikijumuisha Mkataba wa Makubaliano ya ushirikiano wa kiteknolojia kwa kuwafunza wataalamu katika elimu ya tabia za chembechembe ndogondogo na utengenezaji wa vifaa vinavyotokana na chembechembe hizo na kubadilishana walimu katika fani hii.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.