Ivory Coast: Mjadala Mkali dhidi ya Chombo cha Habari kilichotumia Picha za Mwanablogu Bila Ruhusa

Sikukuu ya Noeli ya mwaka 2011 nchini Ivory Coast ilikuwa tofauti na zile za miaka iliyopita. Miezi nane tangu kubadilika kwa utawala, serikali ilitaka kuiadhimisha sikukuu hii kwa mapambo mapya kabisa ya Noeli nchini humo na kwa kuandaa maonyesho makubwa ya milipuko ya fataki [fr] [fr] mnamo Desemba 30-31, 2011.

Wananchi wengi wa Ivory Coast walitoka kwenda kushuhudia burudani hizi pamoja na teknolojia inayotumika, na kila mtu aliondoka na picha za ukumbusho. Kama huo ulikuwa ni uzoefu mzuri kwa wapiga picha hawa wasio na utaalamu mkubwa, basi haikuwa hivyo kwa Audrey Carlalie [fr]. Mwanafunzi huyu mdogo wa ki-Ivory Coast, mpiga picha mwenye taaluma hiyo ambaye hukodiwa kwa muda maalumu, aliziona picha zake za milipuko ya fataki zikiwa zimechapishwa na magazeti fulani ya nchi hiyo na hata kwenye mtandao maarufu zaidi wa kukusanya habari nchini humo –pasipo ruhusa yake.

Hakuchelewa kulalamika kwenye ukurasa wake wa Facebook, na muda mfupi baadae zogo zikatapakaa kwenye blogu na mitandao mingine ya kijamii.

Mwanablogu huyo wa Ivory Coast Edith Brou anaanzisha habari hiyo kwenye
blogu yake [fr] na anaeleza:

En effet, les quotidiens ivoiriens tel que le Jour plus, le Nouveau Réveil, Nord-Sud, l’Intelligent d’Abidjan et même le portail Internet historique Abidjan.net, n’ont pas hésité à publier ses photos alors que la moindre des considérations aurait été de lui envoyer un message privé sur Facebook ou Twitter (elle y est toujours connectée) afin d’avoir sa permission.

Kwa kweli, Magazeti yanayotoka kila siku ya nchi hii kama vile le Jour plus, le Nouveau Réveil, Nord-Sud, l’Intelligent d’Abidjan na hata kikusanya habari cha siku nyingi mtandaoniAbidjan.net, vyote havikusita kuchapisha picha zake, wakati kiwango cha chini kabisa cha kuonyesha kujali kingekuwa ni kumtumia ujumbe tu binafsi kupitia Facebook au Twita (binti huyu huwa hewani muda wote) walau hata kupata ruhusa.

Mara tu baada ya posti ya Edith Brou kutoka, ulimwengu wa wanablogu wa nchi hiyo ulisambaziana habari hiyo, kamaYoyo [fr], mwanablogu mwingine ambaye anawaunga mkono waandishi wa habari kwenye mapambano yao ya kudai kutambuliwa na kuheshimiwa kwa kazi zao:

Depuis hier, la déception se lit dans de nombreux commentaires au sujet des journalistes de la presse écrite ivoirienne. Ces professionnels, qui crient au scandale à la moindre atteinte à leur profession, n'hésitent visiblement pas à jouer de raccourcis pour s'accaparer d'une manière bien moins honorable le travail d'autrui.

Tangu jana, maoni mengi yaliyoandikwa yalionyesha namna watu walivyokuwa wamekatishwa tamaa na waandishi wa habari za magazeti wa nchi hiyo. Wataalamu hawa, ambao kupiga kelele kwa hasira pale linapotokea kosa dogo tu dhidi ya fani yao, na kiuwazi huwa hawachelewi kuchukua hatua za haraka kutumia kazi za wengine kwa njia ambayo huwa haina staha.

Ni katika hali inayofanana na hiyo, alama #Carlaliegate ilitengenezwa kwenye Twita kujadili mada hiyo, na miitikio inaongezeka.

Screen shot of reactions to #Carlaliegate on Twitter

Picha ya kioo kuonyesha miitikio kwenye #Carlaliegate kupitia mtandao wa Twita

Kisichoeleweka kuhusu suala hili ni kwamba magazeti yaliyotuhumiwa hata hayakuthubutu kuomba msamaha. Gazeti lililoharibu zaidi ni L'intelligent d'Abidjan [fr], ambalo lilijitetea kwa kusema:

le vendredi (30 décembre 2011) l'IA (Intelligent d’Abidjan) avait des photographes au palais de la culture. Ils n'avaient pas de connexion a cote et il leur fallait traverser le pont pour arriver au bureau. Le maquettiste est alors aller fouiner sur facebook et a trouve cette photo. Desole de n'avoir pas cite l'auteur mais l'image etant dans le domaine public et n'ayant pas ete fait a but lucratif, que faut il payer? Desole de n'avoir pas cite l'auteur de la photo. Nous le ferons prochainement et trouveront les moyens de rendre plus opérationnels nos photographes.

Siku ya Ijumaa (Desemba 30, 2011) Gazeti letu la IA (Intelligent d’Abidjan) lilikuwa na wapiga picha pale kwenye eneo la “Palais de la Culture”. Hawakuwa na usafiri na kwa sababu hiyo iliwabidi kuvuka daraja kufika ofisini. [Baada ya kuchelewa…] ndipo msanifu kurasa aliingia kwenye mtandao wa Facebook na kupata picha hii. Tunasikitika kwamba hatukuonyesha mwenye picha hii ni nani, lakini kwa kuwa picha ilikuwa imewekwa wazi kwa ajili ya matumizi ya yeyote na haikupigwa kwa ajili ya kutengeneza faida, kwa nini tuilipie? Tunasikitika kwamba hatukumtaja aliyeipiga. Tutafanya hivyo sasa hivi na tutatafuta namna bora zaidi ya kuwawezesha wapiga picha wetu kufanya kazi zao.

Kwa mujibu wa Stephane Kouakou, mtumiaji hai mwingine wa mtandao ambaye ni raia wa nchi hiyo, hali hii inachangia kwenye ubovu vya vyombo vya habari [fr] ambao waandishi wa nchi hiyo wanaonekana kudhamiria kendelea kuujenga:

Comme je l’ai déjà souligné dans un de mes articles « Mauvaise presse », la presse en Côte d’ivoire a de bien mauvaises pratiques qui lui font déjà perdre des acheteur-lecteurs. Elle vient d’ajouter une autre corde à son arc qui lui fait perdre un peu plus de la crédibilité qu’elle n’avait pas.

Kama nilivyokwisha kuonyesha kwenye makala yangu ya” “vyombo vibovu vya habari”, ” vyombo vya habari vya nchi hii vinafanya vitendo vingi vya hovyo ambavyo tayari vinasababisha kukosa wasomaji wanaolipa. Sasa vimeongeza unyoyaji mwingine kwenye kikombe chao, kuvifanya vikose hata heshima ndogo ambayo hata hivyo havikuwa nayo.

Hivi sasa, soga kwenye mtandao linaendelea na hatua ziko njiani, kama Yehni Djidji anavyoonyesha kwenye posti yake [fr] kuhusu mada hiyo:

Abidjan.net a purement et simplement retiré les photos de son site.
L'intelligent d'Abidjan a proposé la compensation suivante: reprise de la photo avec son nom, à l'intérieur du journal mais pas en première page, une collaboration pour que les photos soient rémunérées, l'envoi pendant UN MOIS, de la version PDF du journal, à Carlalie. Avant cela, ce journal a fait plusieurs interventions sur le net qui méritent d'être décortiqué, sans doute dans un autre article.
Carlalie, qui a fait appels à des conseillers juridiques ne peut plus s'exprimer sur le sujet, mais la dernière fois que je l'ai eu, les autres organes de presse n'avaient pas réagi à ses tentatives de communication.

Abidjan.net ilichofanya ni kuondoa tu picha hizo kutoka kwenye tovuti yao. L'intelligent d'Abidjan imependekeza fidia ifuatayo: kuziweka kwa mara nyingine picha hizo kwa kutumia jina lake (kwenye kurasa za ndani na sio kwenye ukurasa wake wa mbele), makubaliano ya pamoja ili picha ziweze kulipiwa, na toleo la PDF la gazeti hilo kutumwa kwa Carlalie ndani ya MWEZI MMOJA. Kabla ya hapo, gazeti hili hili lilijaribu mbinu kadhaa nyingine mtandaoni ambazo zinastahili kuchunguzwa, bila shaka kwenye makala nyingine.

Carlalie, ambaye ametafuta ushauri wa kisheria, hawezi tena kuzungumzia suala hilo, lakini mara ya mwisho nilipozungumza naye, mashirika mengine ya habari hayakuwa yamejibu jitihada zake za kuwasiliana nayo.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.