- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

Uarabuni: Hongera Tunisia!

Mada za Habari: Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini, Misri, Tunisia, Yemen, Habari za Hivi Punde, Siasa, Uandishi wa Habari za Kiraia, Uchaguzi

Hii ni moja ya makala maalum zianazohusu Mapinduzi ya Tunisia ya 2011 [1].

Mwanaharakati wa haki za binadamu Moncef Marzouki, (66), amechaguliwa hii leo kuwa raisi wa mpito wa Tunisia. Mpinzani aliyewahi kufungwa jela na hata kukimbilia uhamishoni wakati wa utawala wa Rais Zeine El Abidine Ben Ali, atakuwa rais hadi hapo katiba mpya ya nchi itakapo kuwa tayari na uchaguzi wa wabunge na rais utakapofanyika.

Kuteuliwa kwake kulizua maoni mbalimbali kutoka kwa wanamtandao wa Tunisia waligawanyika [2]katika makundi mawili ya wanokosoa na wanaounga mkono. Na kwingineko Uarabuni, uteuzi wa Marzouki, uliofuatiwa na hotuba yake yenye mvuto ya kuukubali, ulipokelewa na raia mtandaoni kwa kuwasifu waTunisia kwa hatua nzuri waliyopiga kuelekea demokrasia, na kuombea iwe hivyo hata kwa nchi zao.

Inaugural address of Mr. Marzouki, the new president of the Republic of Tunisia. Image by hamideddine Bouali, copyright Demotix (13/12/11). [3]

Hotuba siku yakusimikwa kwa Bw. Marzouki, rais mpya wa Jamhuri ya Tunisia. Picha na Hamideddine Bouali, hakinakili Demotix (13/12/11).

Tunisia ndio ilikuwa sehemu iliyoanzisha kasi ya mapinduzi Uarabuni yalioanza katika mji wa Sidi Bouzid ambapo Mohammed Bouazizi aliyekuwa hana ajira wakati huo alipojichoma moto mnamo Desemba 17. Tangu siku hiyo, Mamilioni ya waarabu kote katika ukanda huo waliingia katika mitaa ya majiji, miji na vijiji vyao kuandamana wakidai demokrasia, usawa, haki za kibinadamu, kisiasa, kiuchumi na pia mageuzi ya mfumo wa uwakilishi.

Haya ni maoni ya wanamtandao wa kiarabu katika Twitter.

Noon Arabia wa Yemen anaota:

@NoonArabia [4]: Ninatamani siku moja na sisi hapa Yemen tujisikie fahari na mtu ambaye “sisi” tumekumchagua mtu kuwa kiongozi wetu, kama ilivyo leo Tunisia. #Yemen #Tunisia

MuYemeni mwinguine Abubakr Al Shamahi anatoa kiungo [5] cha hotuba ya Marzouki kwa bunge la Tunisia na ametushirikisha ndoto nyingine:

@abubakrabdullah [6]: Inafurarahisha – hotuba ya Marzouki bungeni Tunisia leo – Natumai kuona siku moja kitu kama hicho kikitokea yemen..

Katika hafla ya kuapishwa kwake, Marzouki alilia wakati alipowataja mashahidi waliouwawa wakati wa mapinduzi ya Tunisia.

Mwanahabari Andrew Hammond anataarifu:

@Hammonda1 [7]: #Tunisia rais wa #Tunisia Marzouki alipata kwikwi ya uchungu alipozungumzia wahanga wa mapinduzi; akitoa mfano wa yanayotokea sasa Palestina, Syria na Yemeni.

Katika hili, Mmisri Menna Alaa anasema [ar]:

مصرمش تونس لأنك مش هتلاقي عندنا مسئوول بيعيط على دم الشهداء و عمر ما مجلس الشعب هيقول:إذا الشعب يوما أراد الحياة فلا بد أن يستجيب القدر

@TheMiinz [8]: Misri sio Tunisia kwasababu kamwe hutomuona afisa yeyote akitokwa chozi kwa uchungu wa mashahidi wanaokufa. Na kamwe hautaona Bunge likinyanyuka na kuimba: “kama watu wanataka kuishi, takidiri itabidi ikubali.”

Wimbo huo ni sehemu ya wimbo wa taifa wa Tunisia. Tafsiri ya wimbo mzima inapatikana hapa [9].

Egyptocracy anakubaliana:

@Egyptocracy [10]: Hotuba nzuri sana ya Al Monsef Al #Marzouki. Hongera #Tunisia. Mnatupa tumaini. #Misri.

Mmisri Abdelrahman Ayyash analalamika:

@3yyash [11]: Watunisia walifanya mapinduzi, yao ni ya kweli na sisi tumeiga tu.. Yetu yameshindwa kabisa! #wivu #Tunisia #Egypt #Jan25

Blogu ya Marzouki inapatikana kupitia www.moncefmarzouki.com [12] na anatwita kama @Moncef_Marzouki [13].

Hii ni moja ya makala maalum zianazohusu Mapinduzi ya Tunisia ya 2011 [1].