Makala hii ni sehemu ya habari zetu maalum kuhusu Upinzani nchini Syria 2011.
HABARI MPYA: RAZAN YU HURU!
Mwanablogu wa ki-Syria Razan Ghazzawi ameachiwa huru baada ya kuishi gerezani kwa siku 15. Dada yake ametangaza kuachiwa kwake muda mfupi uliopita kupitia twita.
@NadineGhazzawi:Mvua inanyesha familia ya Razan…haleluyah :)))))))) Sasa ni rasmi, dada yetu yuko nje! Natumainini ndivyo itakavyokuwa kwa dada na kaka zetu wengine wote waliokamatwa.
*****
HABARI ZA HIVI PUNDE:
Nadine Ghazzawi, dada yake Razan ametuma ujumbe kwenye twita:
@NadineGhazzawi: Familia ya #FreeRazan ya #Syria iko njiani kwenda kumchukua dada yangu:)))))))
*****
Mazungumzo yanaendelea kuongezeka mtandaoni kwamba Mwanablogu wa ki-Syria Razan Ghazzawi, aliyekamatwa kwenye mpaka wa Syria na Jordan wakati akiwa njiani kuhudhuria warsha iliyohusu uhuru wa vyombo vya habari katika nchi za ki-Arabu mjini Amman Desemba 4, ataachiwa huru.
Siku nane baada ya kukamatwa, Ghazzawi alishtakiwaorodha ndefu ya mashtaka – yaliyopingwa na jumuiya ya wanablogu na kuyaelezea kama mchezo wa kuigiza.
Miongoni mwa mashitaka yake ni, “kuanzisha taasisi ambayo inayokusudia kubadilisha hali ya nchi kijamii na kiuchumi” na “kudhoofisha hisia za utaifa, na kujaribu kuchochea migogoro ya kidini,” liliandika jarida la Lebanese daily Star wakati huo.
Katika ukurasa wake wa Razan Aachiwe Huru kwenye Facebook watu wanaomwuunga mkono walitoa tangazo kwamba Ghazzawi ataachiliwa, wakimnukuu mwanasheria wa Syria na mwanaharakati wa haki za binadamu Razan Zaitouneh. Makala haisemi hata hivyo, ni lini hasa Ghazzawi anatarajiwa kuachiwa huru.
Nadine Ghazzawi, dada yae Razan, aliitikia habari hizo za Facebook hapo juu kwa kusema:
Nitaendelea kuwajulisha nyote, msihofu sitalifanya suala hili kuwa siri :)
Na anafafanua kwenye Twita:
@NadineGhazzawi: #FreeRazan #Syria Razan hajaachiwa bado, tunangoja habari hizi ziwe rasmi, ndiyo sababu sikuandika chochote mpaka sasa.
Mtandaoni, watumiaji wa intanenti na wote wanaomwunga mkono walibaki na matumaini na bado wakiwa wasiwasi na ukweli wa habari hizi. Mohja Khaf anatuma ujumbe wa twita:
@ProfKhaf: RazanZ inaarifu kwamba #FreeRazan Kuachiliwa kwa dhamana kwa Razan Ghazzawi kumethibitishwa, lakini bado taratibu hazijakamilishwa bado.’
Mwanablogu wa Misri Wael Abbas anasema [ar]:
Wakati Msyria Alaa Khangar anatuma ujumbe kwenye twita [ar]:
Dima Khatib anahitimisha hofu yatu sote:
@Dima_Khatib: Ninaendelea kusoma habari za kuachiwa kwa @RedRazan lakini sijapata chanzo halisi cha habari hizi. Ni ujumbe tu wa watumiaji wa twita. Je, kuna mwenye chanzo? #FreeRazan #FreeRazan
Zaidi ya kublogu, Ghazzawi ni mtumiaji mkubwa wa Twita ambaye amechangia sana kama mwandishi kwenye Global Voices Online na Global Voices Advocacy. Yeye pia ni mmoja wa wanablogu wachache nchini Syria wanaoandika habari kwa kutumia majina yao halisi, wakitetea haki za wanablogu na wanaharakati waliowekwa kizuizini na utawala wa Syria, pamoja haki za mashoga na makundi yanayoonewa.
Kwa miitikio na zaidi na habari zinazoendelea kutufikia, tafadhali angalia ukurasa wa Facebook uitwao Free Razan au tumia alama hii kwenye mtandao wa twita #FreeRazan.
Makala hii ni sehemu ya habari zetu maalum kuhusu Upinzani nchini Syria 2011.