- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

Madagaska: Wajadili Uhalali wa Uwekezaji wa Kigeni wa Moja kwa Moja

Mada za Habari: Madagaska, Afya, Maendeleo, Mahusiano ya Kimataifa, Uandishi wa Habari za Kiraia, Uchumi na Biashara, Utawala

Wakati Madagaska ikijaribu kutafuta suluhisho la matatizo ya muda mrefu ya kiasa, Wanablogu wa ki-Malagasi wanajadili thamani ya Uwekezaji unaofanywa Moja kwa Moja na raia wa Kigeni. Uhalali wa uwekezaji huu wa kigeni uliingia kwenye sura mpya wakati mkataba wa kuuza ardhi uliokuwa ufanywe na mwekezaji wa Kikorea aitwaye Daewoo ulipopata upinzani mkubwa [1] na kwa sehemu kubwa kuchochea mgogoro uliopo.
Wa-Malagarasi wanaamini kwamba Madagaska, kama nchi nyingine za Kiafrika inao utajiri mkubwa wa rasili mali lakini tatizo likiwa ardhi yenyewe kupokonywa kwa sababu ya utawala mbovu na biashara zisizoangalia maslahi ya wananchi. Miaka kumi iliyopita, Jarida la kimataifa la The Economist liliita Afrika “bara lisilo na matumaini”. Katika toleo la hivi karibuni jarida hilo lilionyesha ukuaji wa kasi wa pato la taifa la nchi nyingi za Kiafrika [2] (GDP). Bado hata hivyo, ukuaji huo hauonekani kuwa na uwiano sawa katika nchi za bara hili. Kwa kweli, Madagaska inabashiriwa kuwa nchi yenye kiwango cha kidogo zaidi cha ukuaji [3] barani Afrika.
Kwa kuongeza, mji mkuu wa Antananrivo na majiji mengine yamekuwa yakikabiliwa na ukosefu [4]wa maji na nishati ya umeme mambo yaliyochochea vurugu [3] na ghadhabu miongoni mwa raia wa Malagasi. Hali ilivyo sasa ni moja wapo ya sababu ya jiji la Antananarivo kuwa katika orodha ya moja wapo ya majiji yenye kiwango duni kabisa cha maisha duniani katika Utafiti wa 2011 wa Mercer kuhusu hali ya maisha ya watu [5].

Kwa kule kukabiliwa na historia mbaya ya migogoro isiyoisha ya kisiasa, ulimwengu wa wanablogu wa Kimalagasi unajaribu kuchochea mijadala itakayotoa suluhisho la kisiasa kwa mjadala wa jumla wa namna ya kuukuza upya uchumi ambao umedororora katika miaka mitatu iliyopita.

[6]

Evaratra nchini Madagaska. Picha kwa hisani ya Lalatiana wa blogu ya Madagoravox

Kuufanya Uwekezaji wa Kigeni wa moja kwa moja kuwasaidia watu wa Malagasi

Makubaliano ya matumizi ya ardhi yamejadiliwa kwa kirefu nchini Madagaska kama njia ya kuondokana na umasikini; mkataba uliovunjwa wa Daewoo uliokuwa umetangazwa sana pengine kuliko yote lakini mikataba inayofanana na huo [5] imekuwa ikitekelezwa bila kuchelewa wala miitikio kutoka kwa raia.

Mantiki ya mikataba hiyo inayohusiana na utajiri wa madini wa Madagaska ulijadiliwa hivi karibuni na wataalamu wa Kimalagasi.

Blaise Stephen anafanya kazi katika Chemba ya Kimataifa ya Biashara na Viwanda ya Madagaska [5]. Alionyesha kushangazwa kwake na hali inavyoendelea kuwa ilivyo katika mfumo wa kisiasa wa Madagaska kiasi kwamba kwa mujibu wake hicho ni kikwazo kikuu cha kuzuia ubia wa pamoja na wawekezaji wa kigeni [5](fr):

Nous sommes actuellement en cours de création d'une relation commerciale sur le LONG TERME qui sera bénéfique pour les Entreprises de Madagascar entre notre pays Madagascar et le Koweït. L'objectif de cette coopération Étatique serait de mettre en place une ligne de trésorerie (emprunt) de 3 milliards de dollars (voire plus) sur 5 ans avec une mise a disposition immédiate de 1 millard de dollars (encaissement immédiat) que nous pourrions investir dans les activités a forte rentabilité de notre grand pays Madagascar (Activités d'INVESTISSEMENT et non de fonctionnement) [..] .La négociation concernant la mise en place de cette ligne de trésorerie serait la suivante : … 1) Un emprunt de notre État Madagascar a un taux de remboursement a 3,4 %…2) Pret aux Entreprises de Madagascar a un taux de 5,6% ce qui permet de casser le fonctionnement des banques de Madagascar qui prêtent a un taux de 18,20% sur des durées relativement courtes

Tuko katika mchakato wa kujenga ushirikiano wa pamoja wa kibiashara wa muda mrefu kati ya Madagaska na Kuwait ambao utayanufaisha Makampuni ya Kimalagasi. Lengo ni kuweka mikopo ya Dola za kimarekani Bilioni tatu kwa miaka mitano wakati huo huo Bilioni moja ikianza kupatikana mara moja ili kutumika kwa shughuli za uwezekaji wenye faida kubwa (uwekezaji na sio mtaji wa kugharamia kazi). Makubaliano yako katika mtiririko ufuatao: 1) Madagaska itakuwa ikikopa kwa riba ya asilimia 3.4…2) Nchi ingeweza kuyakopesha makampuni ya Kimalagasi kwa riba ya asilimia 5.6 badala ya riba iliyo hivi sasa ya asilimia 18 au 20 inayopendekezwa na mabenki ya kibiashara tena ndani ya muda mfupi sana.

Akijibu makala yake, Ndimby, anauliza katika sehemu ya kuacha maoni [5] [fr]:

Pourriez-vous m'expliquer pourquoi vous rêvez devant un emprunt à 3,4% alors que vous n'arrêtez pas de critiquer les institutions de Bretton Woods qui prêtent pourtant à des “taux concessionnels” de 0,5% ?

Kwa nini unaota ndoto ya riba ya asilimia 3.4 wakati mnazikosoa taasisi za fedha za dunia (Bretton Woods) zinazotoa mikopi kwa tozo la riba ya asilimia 0.5?

Ambapo, Blaise Stephen anajibu [5][fr]:

Pourriez-vous m'expliquer pourquoi vous rêvez devant un emprunt à 3,4% alors que vous n'arrêtez pas de critiquer les institutions de Bretton Woods qui prêtent pourtant à des “taux concessionnels” de 0,5% ?
La question n'est pas d'aimer ou de ne pas aimer les institutions de Bretton Woods mais de juger de leur efficacité dans le processus de développement économique et social pour un pays comme Madagascar…Il faut savoir que ces Institutions ont mis en faillite des pays comme la Russie ou l'Argentine. .et il faut se poser la question : Pourquoi une Institution sensée sortir les pays de la galère, les enfoncent encore un peu plus? [..] Non seulement elles ne te donnent pas la totalité de ton prêt en un seul versement mais se permettent d'apprécier la gestion des affaires courantes des Etats…En règle général, le rôle d'un préteur est de s assurer que son débiteur le rembourse correctement son prêt, il ne va pas s'immiscer dans la vie privée de son client…Ces institutions se permettent d'apprécier la politique générale des Etats et de donner des leçons quant a la gestion de leur affaires publiques avec une arme redoutable la SUPPRESSION DES VERSEMENTS ATTENDUS…Bizarrement cela fini toujours par la suppression des versements attendus : non seulement tu ne peux plus continuer tes travaux de développement, mais tu rembourses pour de l'argent que tu n'as pas reçu…C'est la raison pour laquelle je préfère emprunter a 3,4% en sachant que les liquidités sont directement disponibles

Swali si ikiwa tunazipenda au hatuzipendi taasisi za kifedha za Bretton Woods, bali kuusaili uafanisi wake katika mchakato wa maendeleo ya kiuchumi na kijamii kwa nchi kama Madagaska….Kumbuka kwamba taasisi hizi zimezifanya nchi kama Urusi au Agentina kuelekea kwenye kufilisika…kwa hivyo mtu unapaswa kujiuliza: Kwa taasisi ambayo ilipaswa kuzisaidia nchi kuondokana na matatizo ya kiuchumi inafanya kinyume chake kabisa kwa kuzisaidia kuzama zaidi? […] Si tu (taasisi hizi) hazikupi mkopo wako wote kwa mkupuo lakini wanathubutu kutathmini namna tunavyoshughulikia masuala yetu ya ndani ya nchi…Kama kanuni ya jumla, wajibu wa mkoposhaji ni kuhakikisha kwamba mkopaji anarejesha mkopo wake kikamilifu na sio (mkopeshaji) kuingilia masuala binafsi ya mteja wake….Taasisi hizi si tu kwamba zinatathmini sera kuu za nchi husika lakini pia zinatoa elimu kuhusu namna ya kuendesha masuala ya ndani ya nchi kwa kutumia silaha yao kubwa: tishio la kufuta mkopo…Katika hali ya kushangaza mara nyingi mambo huishia kwa KUFUTWA KWA MKOPO ULIOTARAJIWA: kwa hiyo si tu kwmaba nchi husika itashindwa kuendelea na miradi yake ya kimaendeleo, lakini pia itakubidi ulipe fedha ambazo haukuzipokea…Hii ni sababu inayoeleza kwa nini ninakubaliana na riba ya asilimia 3.4 nikijua kwamba fedha taslimu tayari ipo

Ndimby anahitimisha majadiliano hayo kwa kuhoji zinakotoka fedha hizo [7][fr]:

Ce que vous dites à la fin de votre démonstration me semble être résumable en un point : l'argent n'a pas d'odeur. Peu importe d'où il vient, à quoi il sert et le contexte dans lequel vous l'utilisez, pourvu que “vous le remboursiez en temps et en heure” [..] sans conditionnalités apparentes telles que vous le souhaitez. Mais je doute que finalement ces prêts soient innocents et effectués pour “l'amour de l'humanité”

Unachokisema kinaweza kufupishwa kwamba: fedha haina harufu. Nani anajali wapi inakotoka, kwa lengo gani au ni kwa mukhtadha gani inatumika almuradi tu unairejesha “kwa wakati” bila masharti yaliyo wazi unayoonekana kuyaogopa. Hata hivyo, bado nina mashaka ikiwa ni kweli mikopo hiyo inatolewa kwa kusukumwa na upendo wa utu na kwamba haina agenda ya siri.

Nchi yenye utajiri wa mali asili na iliyokubuhu kwa ufisadi

Kile anachokigusia Ndimby ndicho hasa hatari ya mikopo isiyo na masharti au isiyo na uwazi wa kutosha katika namna inavyotumika katika uwekezaji.
Perspectives economiques en Afrique anafupisha hali ya kiuchumi ilivyo [8] [fr]:

L’environnement politique demeure instable. Dans ce contexte, les partenaires émergents représentent une opportunité pour Madagascar. La Chine n’a pas reconnu le gouvernement malgache actuel, mais plusieurs de ses entreprises continuent de signer des contrats avec lui. En 2010, le groupe chinois Wuhan Iron and Steel Co (WISCO) a versé une avance de 100 millions USD pour une concession portant sur l’extraction de minerai de fer. Si les gisements se révèlent aussi vastes qu’il l’espère, il pourrait y investir 8 milliards USD, ce qui serait, de loin, le plus gros investissement direct étranger (IDE) effectué à ce jour à Madagascar. Ce pays, où la corruption est omniprésente, devra réussir à transformer cette opportunité en développement.

Mazingira ya kisiasa bado hayajatengemaa. Katika mukhtadha huu, nchi zinazoibukia kiuchumi zinatoa fursa kwa Madagaska. China bado haijaitambua rasmi serikali iliyopo madarakani lakini makampuni mengi ya Kichina yana mikataba ya kibiashara na nchi yetu. Mwaka 2010, kampuni ya Kichina ya chuma iitwayo Wuhan Iron and Steel Co (WISCO) ilipata mkopo wa Dola za Kimarekani milioni 100 kwa ajili ya kuchimba madini ya chuma. Kama itatokea machimbo haya yakawa mengi kama inavyobashiriwa, (makampuni haya) yatawekeza zaidi ya Dola za Kimarekani bilioni 8 ambazo zingeweza kuwa kiasi kikubwa zaidi cha uwekezaji kuwahi kutokea nchini Madagaska. Katika nchi inayosongwa na ufisadi, wanahitaji kuonyesha kwamba wanaweza kuigeuza fursa hii kuwa maendeleo halisi.

Kama ilivyotajwa awali, kukosekana kwa kanuni na miundo iliyowazi kipindi hiki cha mpito tayari kinaweka mazingira murua kwa kila aina ya ufisadi. Katika makala hii, Franck R anabainisha matukio ya ufisadi ya hivi karibuni [9][fr]:

A Madagascar, notamment sous ce régime transitoire, on aime trop prendre son temps. Et on aime aussi s’enrichir… rapidement. [..] ces véhicules de l’UNICEF confisqués par des politiques, la scandaleuse richesse, en l’espace de quelques mois, d’un célèbre affairiste de la place qui a acquis un immeuble sis à Antanimena, un gros paquet d’actions de Madarail,[..] Il n’est pas le seul à profiter de la transition pour se faire du fric. Ainsi va la transition.

Nchini Madagaska, hususani chini ya serikali ya serikali ya mpito iliyopo, tungependa kushika hamsini zetu linapokuja suala la kupata utajiri […] magari ya UNICEF yalitwaliwa na serikali, utajiri wa kufuru na wa ghafla wa mfanyabiashara ambaye ndani ya miezi michache amelichukua jengo la Antanimena, ambao ni chaguo kubwa la hisa mjini Madarail […] na wala si yeye tu anayetengeneza pesa kwa biashara. Na ndivyo mpito unavyokwenda.

Ndimby anahitimisha kwa kuonyesha uhusiano kati ya ufisadi na hali tete ya kisiasa [10] [fr]:

C’est ce genre de mentalité, qui tente systématiquement de cacher la réalité et de détourner l’attention des insuffisances du clapier en matière de gestion publique qui fait que la crise perdure. A force de se complaire dans le subterfuge et la superficialité ; à force de prétendre qu’un coup d’État est une oeuvre de salut public ; à force d’insinuer qu’un régime qui ne tient que par la répression et la corruption est soutenu par l’ensemble du peuple ; il ne faut pas s’étonner que la reconnaissance internationale ait patiné pendant plus de deux ans et que la réconciliation nationale dérape périodiquement.

Ni kwa sababu ya mitizamo ya aina hii inayojaribu kwa ufundi mkubwa kuficha uhalisia na kuwapotezea watu uelekeo wasione udhaifu mkubwa wa matumizi ya fedha za umma, ndio maana migogoro tete haiishi. Ni kwa sababu siku zote wanatufanya tuyatizame mambo kijuu juu na matangazo yanayovutia, kwa sababu mara zote wanajaribu kushawishi kwamba jeshi lipo kwa maendeleo ya watu walio wengi, na kwa sababu wanajaribu kuwashawishi wengine kwamba serikali inaungwa mkono na watu wakati inapokuwa madarakani basi kujikita tu kwenye ukandamizaji na ufisadi. Tusishangazwe kwamba kutambuliwa kimataifa hakuwezekani kirahisi baada ya miaka miwili katika hali ambayo umoja wa kitaifa bado ungali ukishindikana.

Wanablogu wa Ki-Malagasi wanaonekana kuafikiana kwamba uwekezaji wa moja kwa moja wa kigeni unaweza kuwa mzuri kama ulivyo uwazi unapoambatana na utekelezaji. Vinginevyo, itakuwa hadithi nyingine iliyozoeleka ya fedha zilizopotea ambazo zitawanufaisha watawala mafisadi wa Kiafrika.