Iran: Yu Wapi Mwanafunzi Mwenzangu?

Viti kadhaa vilivyo wazi katika vyuo vikuu vya Iran vilikaliwa rasmi na wanafunzi ambao hivi sasa wametoweka. Wengine wananyimwa elimu kutokana na sababu za kidini, kama vile waumini wa Baha'i dini yenye waumini wachache , wengine wamefungwa jela kwa sababu za kisiasa, wengine wameuawa mitaani, au wamelazimishwa kuondoka Iran. Katika mazingira ya kawaida, kuna wanafunzi ambao wamefukuzwa tu.

Mwaka huu Tahkim Vahdat, kikundi cha upinzani cha wanafunzi kinachoongoza, kiliitisha kampeni ya “viti visivyokaliwa” duniani kote, mnamo desemba 7,siku ya wanafunzi wa Iran,ili kukumbuka wale wote waliokosa tumaini la kupata elimu. Ukurasa wa Facebook ulianzishwa, na filamu nyingi zilipandishwa kwenye YouTube, ili kuonyesha mshikamano kwa wanafunzi waliopoteza na wanaokandamizwa nchini Iran. Hizi ni tatu kati hizo filamu.

Chuo kikuu George Washington, USA

Barcelona, Hispania

http://www.youtube.com/watch?feature=player_embedded&v=4535gGdL-qQ

Ujumbe kutoka Kanada kwa mwanafunzi aliyefungwa jela

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.