Global Voices: Changia Leo

2011 umekuwa mwaka usio wa kawaida katika maudhui ya mtandaoni. Global Voices imekuwepo pale wakati mapinduzi yalipotokea, wakati tawala za kidikteta zikianguka, na matokeo ya matumizi ya mtandao yaliposambaa katika miji na mitaa ya wachangiaji wetu wanaoripoti kutoka duniani kote.

Global Voices poster

Ili kuusherehekea mwaka ambao umekuwa wa kusisimua sana kwetu, sisi, pamoja na marafiki zetu wa Morningside Analytics,tumetengeneza nakala chache za toleo la bango ambalo ambalo linaonyesha “makundi makini” ya wanablogu ambao hutumia kiungo cha Global Voices ambao pia hunukuu maudhui yanayofanana mtandaoni. Picha inayotokana na kazi hiyo inaonyehsa wigo wa jumuiya ya Global Voices, na kuifanya iwe kazi ya sanaa inayoadhimisha mwaka muhimu katika historia na nguvu ya vyombo vya habari vya kiraia. Bango hili linapatikana kwa yeyote anayechangia Dola za Kimarekani 25 au zaidi. Agiza moja kwa ajili yako leo kupitia kiungo hiki. Tutakuwa tukiyatuma mabango hayo mwezi Januari 2012.


Hata kama hautapenda kutumiwa bango, tutakushukuru kwa mchango wako. Michango ya mara kwa mara haitozwi kodi nchini Marekani, na inaweza kufanyika kupitia ukurasa wetu wa Kuchagia. Tafadhali hakikisha unasambaza habari hizi kupitia mitandao yako!

Global Voices ni jumuiya ya watu wanaojitolea inayoundwa na waandishi, wafasiri, na wanaharakati wa mtandaoni zaidi ya 500 wanaokuletea habari pamoja na mazungumzo yasiyopewa kipaumbele katika vyombo vikuu vya habari duniani. Tazama video yetu mpya inayoonyesha picha na nukuu kutoka kwa baadhi ya wanaotuunga mkono:

Global Voices iko katika kiini cha mazungumzo halisi ya kidunia, na mchango wako utatusaidia kutufanya tuendelee kuwa tulipo. Asante sana!


Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.