Afrika Kusini: Malema Ameng’oka, Nini Kinafuata?

Mwanasiasa na mtu ambaye husababisha utata zaidi ya wote nchini Afrika Kusini Julius Malema amesimamishwa uanachama wa chama cha ANC kwa miaka mitano. Julius Malema ni rais wa zamani wa Umoja wa Vijana wa Chama cha ANC (African National Congress Youth League).

Mwaka jana, Malema aliongoza wanafunzi kuimba wimbo wa zamani uliotumika katika harakati za kupingana na Ubaguzi wa Rangi ulioitwa “Ua Kaburu” na Jaji wa Afrika Kusini alimtia hatiani kwa matumizi ya hotuba ya kuchochea chuki kwa sababu ya maoni yake aliyoyatoa kuhusu mwanamke aliyemtuhumu Rais Jacob Zuma kwa ubakaji.

Mwezi Mei 2010, Malema alilazimishwa kutoa tamko la kulitaka radhi taifa na kutakiwa kuhudhuria darasa la namna ya kudhiti hasira zake. Akabadili wimbo wa “Ua kaburu”kuwa ‘Mbusu Kaburu‘.

Malema anachukuliwa na mashabiki wake kama sauti ya dhati ya watu masikini wa Afrika Kusini hususani kwa wito wake kuhusu utaifishwaji wa migodi ya Afrika Kusini.

Blogu ya Padri Stephen inaandika kuhusu kusimamishwa kwake:

Former President of the ANC Youth League. Photo released under Creative Commons (CC BY-SA 3.0) by Gary van der Merwe.

Picha: Rais wa zamani wa Umoja wa Vijana wa ANC. Picha imetolewa chini ya Creative Commons (CC VY –SA 3.0) na Gary van der Merwe.

Julius Malema atanyang’anywa uongozi wake wa Umoja wa Vijana wa ANC (ANCYL) baada ya kusimamishwa uanachama kwa miaka mitano.

Malema anazuiwa kujihusisha na shughuli zozote za Umoja wa Vijana (ANCYL) na chama cha ANC katika kipindi alichosimamishwa, uamuzi ulioanza kutekelezwa mara moja leo baada ya Derek Hanekom, mwenyekiti wa kamati ya taifa ya nidhamu katika ANC, kutangaza matokeo ya mchakato wa kinidhamu dhidi ya Malema na kigogo wa juu kabisa wa Umoja huo Jijini Johannesburg leo.

Malema hakuwepo wakati tangazo hilo likitolewa ndani ya Jengo la Luthuli. Alisemekana alikuwa Limpopo akifanya mtihani.

Kamati ilimtia hatiani kwa mashitaka mawili. Moja likihusiana na matamshi aliyoyatoa tarehe 31 Julai –kwamba ANC haikuwa ikijihusiaha tena na masuala yanayohusu maslahi ya Afrika.

….

Aidha, Malema aliamriwa kuachia kiti chake kama rais wa Umoja huo mara moja.

Amepewa siku 14 kukata rufaa…

Makala ya [af] Hardspear juu ya Malema [af] ni udhihirisho ulio wazi wa hofu kwa siku za usoni:

Julius Malema… Ek sidder om te dink watse kak gaan hy nou aanjaag…

Ninatetemeka kufikiri ni ujinga gani atakaoufanya baada ya hapa

Kwa kuangalia matukio yaliyotufikisha katika hatua hii,ni lazima tutazame “Maandamano ya Uhuru wa Kiuchumi” ya hivi majuzi yaliyoongozwa na Malema. Wavuti ya Leaboy inatupa utangulizi murua kuhusu suala hili kwa kutilia msisitizo kikaragosi cha Zapiro kilichoelezea tukio hilo kwa makala yenye kichwa cha habari, “Zapiro ana uchambuzi wa kina juu ya maandamano ya Uhuru wa Kiuchumi”.

Majadiliano makuu katika ulimwengu wa Blogu za Kiafrika Kusini kuhusu maandamano haya ni unafiki bayana wa Julius Malema anayetilia msisitizo mno mateso ya masikini wa Afrika Kusini wakati yeye mwenyewe anaishi kwenye ufahari. Blogu ya One Long Minute inatupa muono wake katika makala yenye kichw acha habari, “Mnaandamana kwa ajili ya kitu gani?”:

Kwanza maandamano kwa ajili ya Uhuru wa Kiuchumi, yaliyoongozwa na Julius Malema, wakati alipokuwa hajachoka sana na akipumzika ndani ya gari lake la kifahari [aina ya BMW]. Kuna kejeli kubwa sana inayonifanya nizidiwe na hisia. Huyu mwanaharamu mchovu bado anaifanya halaiki imfanyie kazi yote huku yeye akichukua sifa zote peke yake.

Blogu ya Vuilblog anatumia dhihaka dhidi ya wafuasi wa Malema kwa kutumia picha ya Malema, ikiwa na maandishi yafuatayo:

Hauna maji, unaishi kwenyebanda, unasafiri kwa taksi. Ninanunua magari ya kifahari, ninanua nyumba za bei mbaya, ninakunywa Johnnie Walker pekee. Bado mnanipenda. Asanteni kwa kuwa wajinga.

Makala nyingine zinajadili taswira na tabia anayoionyesha Julius Malema. Akielezea jinsi Malema anavyojifikiria kwa mtindo wa ubeuzi ni 2OceansVibe:

Katika hotuba yake ya hivi karibuni katika Chuo Kikuu cha Walter Sisulu huko Mthatha, Malema alisema ilikuwa ni kazi ya vijana kupenyeza hoja za kiradikali, lakini akalalamika kwamba siku hizi, mtu anawekwa kiti moto mbele ya kamati ya nidhamu kwa ajili ya “kusema ukweli”.

Hii ni kutoka kwa mtu ambaye alikuwa kwenye vyombo vya habari asubuhi ya leo kwa kutumia maneno ya kibaguzi dhidi ya Wahindi. Masikini Juju. Kwa kweli anajisikia tu kutokueleweka na kutokuugwa mkono.

Bibliopolit anamfananisha Malema na Lady Gaga:

Ndivyo ilivyo, hapa Afrika Kusini, tunaye mtu anayefanana na Lady Gaga naye ni Julius Malema! Ni kwa kuwa tu yupo kwenye majukwaa ya Kisiasa. Tumwite Julius Gaga, or Lady Malema? Kama isingekuwa kwa sababu ya matamshi na madai yaliyojaa chuki ya Malema, asingepata hata chembe ya kusikika kama anavyosikika hivi sasa. Kwa Malema, chochote kama hakitaleta mkanganyiko wa fikra, hakina faida ya kukisema, kwa mujibu wa namna Lady Malema anavyowaza.

Malema anastawi kutokana na umaarufu, na kwa maoni yangu, anaangukia kwenye kundi moja na Lady Gaga. Ingawa kwa umbo anaonekana ni mtu mzima, bado hajakomaa kiakili au kijamii ili kuwa mtu mzima, na anaondelea kuusaka umaarufu kama msichana wa miaka 10. Na njia pekee anayoweza kuitumia kupata umaarufu huo anaoutaka kwa udi na uvumba, anafanya na kusema mambo yatakayowachanganya watu.

Blogu ya The fire in My Eyes inakwenda moja kwa moja kwenye hoja:

Julius Malema ana chembechembe za dikteta.
Anawataka raia wa Afrika Kusini walio wengi kuzaana na inaonekana anaota ndoto za nchi ambayo raia weupe hawapo tena.
Namna anavyoongea inamfanya mtu afikiri Ubaguzi wa rangi uliogeuzwa na kila mara anawazungumza watu weupe kama maadui.
Ana vijana wengi wanaomfuata nchi Afrika Kusini hata kama ana mashitaka ya ufisadi.
Sifa mbaya aliyopata kwenye vyombo vya habari inaelekea kuwasha moto kwa wafuasi wake na amekuwa kana kwamba ‘mwokozi’ kwa wengi.

Property Mag inaweka mhutasari wa hali ya kisiasa ilivyo sasa Afrika Kusinikwa kuyatizama matukio ya hivi karibuni:

Kutimuliwa kazi Mawaziri wawili, kufukuzwa kwa Mkuu wa Polisi, Upelelezi wa njama za silaha pamoja na ukweli kwamba kwa matokeo yoyote, Julius Malema atayakabili mashitaka yake, vyote hivyo vimetuma ujumbe chanya kwamba Afrika Kusini haitaruhusiwa kugeuka kuwa nchi ya Ulimwengu wa Tatu. Hatua hizi zilizochukuliwa na Rais pamoja na bajeti mpya ndogo ya Waziri wa Fedha, vimerudisha imani kwa kiasi kikubwa katika utawala ulioonekana kuanza kukosa nguvu.

Kwa hivyo tunajua mahali tuliko sasa, bado hatujajua mustakabali wa Malema na Afrika Kusini.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.