19 Disemba 2011

Habari kutoka 19 Disemba 2011

Syria: Mwanablogu Razan Ghazzawi Ameachiwa HURU!

Habari zinasambaa mtandaoni kwamba mwanablogu wa Syria aliyekuwa gerezani anaweza kuachiwa huru wakati wowote kuanzia sasa. Ghazzawi, anayeblogu akiwa Syria kwa kutumia jina lake halisi, aliwekwa kizuizini akiwa njiani kuhudhuria warsha ya uhuru wa Vyombo vya habari iliyokuwa ikifanyika mjini Amman. Kuwekwa kwake kizuizini kulikosolewa na watumiaji wa mtandao, ambao sasa wanasubiri kwa hamu kuachiwa kwake. Amekuwa ndani kwa siku 15 sasa.

Mexico: Wanafunzi Wawili Wauawa Kwenye Maandamano Huko Ayotzinapa

  19 Disemba 2011

Wanafunzi wawili, Jorge Alexis Herrera Pino na Gabriel Echeverría de Jesús, waliuawa tarehe 12 Desemba 2011, wakati wa maandamano ya wanafunzi wa shule ya vijijini ya Raúl Isidro huko Ayotzinapa, mji mkuu wa Guerrero, Chilpancingo, nchini Mexico. Mitazamo yenye utata kuhusu yalioyotokea imechapishwa mtandanoni.