Habari kutoka 18 Mei 2011
Uganda: Polisi Wawanyunyizia Waandamanaji Rangi ya Waridi
Polisi wa Uganda wameikabili kampeni inayoendelea kwa mwezi mmoja sasa ya Kutembea Kwenda Kazini kwa kuwanyunyuzia waandamanaji moshi wa machozi na risasi sa moto. Wakati wa maandamano siku ya Jumanne, walitumia mbinu mpya, ya kuwashambula waandamanaji waliokuwa wakijaribu kuandamana kuelekea viwanja vya katiba katikati ya jiji la Kampala kwa maji yaliyochanganywa na uji wa rangi ya waridi.