Habari kutoka 2 Mei 2011
Naijeria: Gavana wa Kinaijeria Kwenye Twita
Gavana wa Kinaijeria Kayode Fayemi yumo kwenye Twita, mwanablogu wa Naijeria Lord Banks anaripoti.
Uganda: Wananchi Wakasirishwa na Kukamatwa Kikatili kwa Kiongozi wa Upinzani
Kiongozi wa upinzani nchini Uganda Dk.Kiiza Besigye alikamatwa tena katika mji mkuu wa Kampala kutokana na kushiriki kwake katika Kampeni ya Kutembea Kwenda Kazini usiku mmoja baada ya kuachiwa huru kwa dhamana. Besigye alipewa dhamana kwa sharti kuwa asijihusishe na kampeni ambayo imeuweka utawala wa Uganda kwenye vichwa vya habari kwa majuma matatu sasa.
Msumbiji: Polisi Washambulia Waandamanaji
Siku ya tarehe 6 Aprili, maofisa wa tawi la Polisi wa jamhuri ya msumbiji (PRM) – Kikosi cha Askari Maalum wa Dharura (FIR) – walitumia nguvukusitisha maandamano ya wafanyakazi wa shirika binafsi la ulinzi Group Four Security (G4S). Kwenye Facebook, wanamtandao walionesha kuchukizwa kwao kutokana na vitendo hivyo vya kikatili na kuhoji wajibu wa polisi, sheria na haki za binadamu.