- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

Naijeria: Wanablogu wa Ki-Naijeria wanasema nini kuhusu uchaguzi wa mwaka 2011?

Mada za Habari: Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara, Naijeria, Siasa, Uandishi wa Habari za Kiraia, Uchaguzi

Kadiri uchaguzi wa mwaka 2011 nchini Naijeria unavyozidi kukaribia, ulimwengu wa blogu umehamasika na watu wenye sauti zinazosikika. Wanablogu wa Naijeria wanatumia muda wao mwingi kuzungumza ilhali wakitengeneza mjadala wa kitaifa kuhusiana na mustakabali wa nchi yao.

Nze Sylva Ifedigbo [1] anaanza mwaka mpya kwa bandiko linalorusha lawama kwa milipuko ya mabomu iliyowatuma wa-Naijeria kadhaa kukutana na mababu zao kabla ya wakati. Inasikitisha kwamba mapigano yanaendelea kutokea tena katika mlinganyo wa siasa za Naijeria:

Ni siku ya kwanza ya mwaka inayoashiria kuwa utakuwa ni mwaka wa kusisimua. Juu katika orodha kwa wa-Naijeria wengi bila shaka ni uchaguzi mkuu uliopangwa kufanyika mwezi Aprili. Mchakato wa uchaguzi huo unaanzishwa na uandikishwaji wa wapiga kura utakaoanza mwezi huu. Tuko tayari kwa namna gani kuifanya fursa hiyo iwe na maana? Kwa masikitiko hata hivyo, sherehe yetu ilitekwa kwa mara nyingine na wapuuzi wasio na aibu waliolipua bomu katika soko ambalo mara zote hujaza watu sana liitwalo Mogadishu Cantonment Abuja kwenye mkesha wa mwaka mpya.

Felix Okoli [2] lanaweka mzigo kwenye meza ya Tume ya Uchaguzi ya Naijeria (INEC) na hasa mkubwa wa tume hiyo Attahiru Jega:

Jukumu limemwangukia Jega kuhakikisha kwamba Uchaguzi wa Rais wa mwaka 2011 na chaguzi nyinginezo zinakwenda vyema na matokeo yawe nakisi ya matarajio ya kweli ya watu wa maana sana wa Naijeria.

Uandikishwaji wa Wapiga kura ulikuwa ni jaribio la kuthibitisha ukosefu wa maandalizi wa Tume (INEC) katika kufanya uchaguzi unaoheshimika. Mwanablogu Nigerian Curiosity [3] anadai kwamba:

Siku hizi za kwanza pia zinaibua maswali kuhusu Tume ya Uchaguzi (INEC) kukosa maandalizi na uwezo wake si tu wa kuandikisha wapiga kura kwa wakati uliopangwa lakini pia kuandaa uchaguzi huru na haki mwezi Aprili.

Uchaguzi unahusiana na tarakimu. Mawimbi ya mapinduzi yaliyosukumwa na vyombo ya habari vya kijamii katika nchi za Kaskazini mwa Afrika yameamsha uelewa kwa wengi. Haishangazi kwa hivyo kwamba chaguzi za awali ndani ya vyama zilifuatiliwa kwa zaidi ya shauku inayopita. Nnenna [4] anaandika kuwa:

INchini Naijeria, nilifuatilia chaguzi za awali kupitia #PDPprimiraies (chaguzi za mwanzo za wagombea ndani ya vyama)…Wakati wote huu, nilikuwa nasubiri…naandika, nasambaza habari kupitia twita…nikiwa na maelfu ya Wa-Naijeria wengine duniani kote? Kwa nini? Kwa sababu yule atakayeshinda ndani ya chama cha PDP atakuwa na uhakika kwa asilimia nyingi kushinda Urais. Uchaguzi wa PDP ulimalizika baada ya masaa 15. Matokeo ya mwisho yalitangazwa kama saa 1 asubuhi iliyofuata. Hatukulala! Kila hesabu iliyotoka ilikuwa kwenye radio ya mtandaoni, twita, ama Facebook.

Feathers Project [5] anafikiri kwamba uchaguzi wa mwaka 2011 utakuwa wa tofauti kwa sababu ya waangalizi wengi wa kujitegemea wa uchaguzi walioko nchini.

.uchaguzi wa mwaka 2011 unaonekana kuwa ni wa muhimu sana kiasi cha kutokuachiwa wanasiasa pekeyao. Majina maarufu kama vile Piga kura ama Ridhika tu, JCPL (Jiandikishe, Chagua, Piga kura na Linda kura), If Naija Votes (kama Naija itapiga kura) yamegeuka mjadala.

[6]

ReVoDa, programu-tumizi ya kwenye simu za kiganjani unaowapa raia wasio na mafunzo nyenzo ya kushirikishana uzoefu wa uchaguzi. Chanzo: blogu ya ‘Gbenga Sesana.


Gbenga Sessan [7] anathibitisha nguvu ya vyombo vya habari vya kiraia katika uchaguzi huu hasa baada ya kupatikana kwa programu-tumizi mpya –ReVoDa ambayo:

…utawafanya wa-Naijeria 87,297,789 wenye simu za kiganjani, 43,982,200 waliounganishwa na mtandao wa intaneti na 2,985,680 walio kwenye mtandao wa Facebook kuwa waangalizi wa uchaguzi wasio rasmi.

Eurukanaija [8] ana ushauri kwa Mke wa Rais, ambaye matusi yake ya Kiingereza yamegeuka kuwa kivutio cha taifa:

D tin consan the campaign wey you dey helep our Presido, Uncle Jo and all im ‘umblerra’ friends do. Auntie, you try. Even though you no too sabi English, you dey make effort…

Jambo linaloigusa kampeni ni wewe kumsaidia Rais wetu, Mjomba Jo[Goodluck Jonathan] na ndivyo marafiki wake wote vivuli wanavyofanya . Shangazi, umejaribu. Hata kama hujui kusema kimombo, unaonyesha bidii…

Inaonekana kuwa si tu wanablogu wanaoongea bali wanamuziki pia wanaimba. Kampeni ya elimu ya uraia kwa ajili ya uchaguzi huu iliyoshika kasi mtandaoni imepewa sauti. Trading Places [9] anaielezea kwamba:

Kupitia twita, Eldeethedon, mmoja wa wanamuziki kadhaa, amewasihi watu “kuwa mabadiliko” na Kujiandikisha Kuchagua, Kupiga na Kulinda kura [10].