Ni msimu wa uchaguzi nchini Naijeria. Lakini ratiba ya uchaguzi huo imesogezwa mbele kwa juma moja zaidi [1]kwa sababu ya matatizo ya kiuratibu. Uchaguzi wa Rais [2] ulipangwa kufanyika tarehe 9 Aprilli 2011. Hii ni orodha yetu ya watumiaji wa twita unaweza kufuatilia kazi zao wakati wa uchaguzi wa Naijeria 2011 na miitikio yao kuhusiana na suala la kuahirishwa uchaguzi huo.
@MrFixNigeria [3] ni Balozi wa Microsoft wa Usalama wa Mtandaoni na ndiye meneja wa kampeni za Urais mwenye umri mdogo kuliko wote katika Naijeria.
@EiENigeria [4] (Imetosha sasa basi Naijeria [5]) ni muungano wa Wa-Naijeria vijana wanaofanya kazi ya kuhamasisha ushiriki wa vijana katika uchaguzi wa mwaka 2011.
Kutokana na kuahirishwa kwa uchaguzi [6], tutakuwa tukizindua kura yetu ya mwisho ya maoni (“Nani utampa kura yako tarehe 9 Aprili”) siku ya Jumanne, Aprili 5. #NigeriaDecides
@toluogunlesi [7] ni mwanasafu katika gazeti la Naijeria, liitwalo NEXT, mwanafunzi wa Uandishi wa Ubunifu katika Chuo Kikuu cha East Anglia (UEA).
Siku ya huzuni kiasi gani [8]kwa Naijeria:
Siku ya huzuni kwa Naijeria: uchaguzi umeahirishwa, Ibori ameachiwa, na tena moja ya mpishiwyake smahiri anaunguza yai linalochemka WTF http://twitpic.com/4gb7yb
@feathersproject [9] ni mwandishi wa ki-Naijeria, mchapishaji, na mwandishi [10]wa Global Voices Online.
UCHAGUZI WA BUNGE: AFADHALI UMEAHIRISHWA KULIKO UNGEVURUGWA [11] http://wp.me/pfoBI-jq
@TechLoy [12] ni blogu inayoongoza katika masuala ya kiteknolojia, inayoleta habari mpya mpya za teknolojia, inayotoa tathmini za kampuni an kiradi inayozinduliwa pamoja na tathmini za bidhaa mpya.
Alama ya #Jega inaongoza kwenye Twita [13]:
Inafurahisha kumwona “Jega” [Attahiru Jega, kiongozi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC)] akiongoza kwa Twita duniani kote kama #Jega ataamua mustakabali wa Naijeria
@COOL2VOTE [14]:
#BREAKINGNEWS (HABARI MPYA KABISA): UCHAGUZI UMEAHIRISHWA MPAKA APRILI 4. [15]. IMETHIBITISHWA NA MWENYEKITI WA TUME YA UCHAGUZI. #Cool2Vote #NigeriaDecides
@Africanelection [16] ni mradi unaokuza uwezo wa waandishi wa habari, waandishi wa kiraia kutumia vyombo vipya vya habari kwa minajili ya kufanya uangalizi na kuripoti uchaguzi barani Afrika.
Naijeria:Harakati zimesitishwa mpaka saa 12 jioni [17]. http://ow.ly/4rHrB #naijavotes2011
@delemomodu2011 [18] ni mgombea wa urais kupitia chama cha National Conscience Party (NCP).
Tulichokishuhudia leo ni udhihirisho wa wazi wa kushindwa kazi na [19]kukosa mipango kwa hali ya juu. #INEC
@DamiOyedele [20]:
Posti mpya: ‘Tarehe mpya ya uchaguzi haiwezekani’ [21]anasema Dele Momodu http://bit.ly/ewGfNh cc @mrfixnigeria
@gbengasesan ni mjasiriamali wa kijamii wa Naijeria mwenye kuvutiwa sana matumizi ya TEKNOHAMA katika maendeleo; kuelekea kwenye kuzalisha fursa zilizo bora na zenye uhakika. Unaweza kusoma zadi kumhusu ‘Gbenga Sesan hapa [22].
Leo isingepaswa kutokea [23]… soma blogu yangu ya hivi karibuni, “Wakati wa-Naijeria wakiamua (sehemu ya 6)”, kwa kwenda hapa http://gbengasesan.com #ReVoDa #NigeriaDecides
@forakin [24] ni mtu asiye na ukinega katika tarakilishi, mwanablogu, na m-Naijeria azungumzaye Kifaransa anayeishi Amsterdam.
@reclaimnaija [25] ni jukwaa pana linalojihusisha na ushirikishwaji maarufu wa wananchi wa chini katika kunadi uwazi wakati wa uchaguzi na serikali ya kidemokrasia.
Taarifa zetu zinathibitisha [26] kauli ya kijasiri ya Prof. Jega kwamba majimbo mengi hayana vifaa vya upigaji kura. #reclaimnaija #NigeriaDecides
Watumiaji wengine zaidi wa twita unaoweza kufuatilia kazi zao wanaweza kupatikana hapa [27].