- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

Misri: Mubarak awekwa Kizuizini

Mada za Habari: Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini, Misri, Harakati za Mtandaoni, Maandamano, Sheria, Siasa, Uandishi wa Habari za Kiraia

Makala hii ni sehemu ya habari maalumu tunazowaletea kuhusu Mapinduzi ya Misri ya Mwaka 2011 [1].

Miezi michache tu iliyopita, raia wengi wa Misri walitamani sana kumwona aliyekuwa rais wa nchi hiyo, Rais Mubarak, akitupwa jela, hata hivyo, pengine ni wachache miongoni mwao waliofikiri kwa uhakika kabisa kwamba siku moja jambo hili lingetimia.

Hata hivyo, mnamo Jumatano ya tarehe 13 Aprili, 2011, raia wa Misri waliamka na mapema asubuhi ya siku hiyohiyo kukutana na habari zinazohusu Mubaraka kutupwa kizuizini. Hapa chini tunawaletea jinsi habari hizi zilivyopokelewa katika ulimwengu wa uandishi wa habari wa Kijmii miongoni mwa Wamisri.

Kusherehekea kutiwa nguvuni kwa dikteta

Mwandishi wa Misri, Ibrahim Farghali, alilinganisha wakati huo [2] [ar] na wakati ule kulipokuwa na habari za mtu wa kwanza kufika katika anga za juu:

احتفلت روسيا امس بذكرى خروج اول رائد فضاء روسي للفضاء الخارجي يوري جاجارين، واليوم تحتفل مصر بسجن الرئيس المخلوع حسني مبارك

نتمنى أن نرى مصر قريبا تحتفل بإنجازات شبيهة بمنجزات دول العالم المتقدم
والثورة لا تزال في الشارع
Jana, Urusi ilisherehekea kumbukumbu za binadamu wa kwanza kwenda katika anga za juu, Yuri Gagarin [3]. Na leo, Misri inasherehekea tukio la aliyekuwa rais, Hosni Mubarak, kuanza safari ya kwenda gerezani.

Tuna matumaini kwamba siku moja Misri isherehekee mafanikio kama hayo ya ulimwengu uliondelea, na tunatumaini kwamba hata wakati huo ule moyo wa mapinduzi utaendelea kuwepo mitaani.

Zeinobia naye aliandika makala mpya ya blogu kuhusiana na wasaa huo, aliupa jina rahisi tu, “A Historical Moment [4]” yaani “Wakati wa Kihistoria”. Kisha alieleza jinsi watoto wa rais huyo wa zamani nao walivyokamatwa na kutiwa kizuizini:

Rais aliyetimuliwa madarakani Mohamed Hosni Mubarak na watoto wake Alaa na Gamal El-din wametiwa nguvuni na watakuwa gerezani kwa siku 15.

Kisha Zeinobia aliendelea kueleza kwamba Mubarak anakabiliwa na mashtaka ya kuua waandamanaji na kuiba fedha za umma; hata hivyo, hadi wakati huu Mubarak bado yupo hospitalini kwa sababu ya matatizo ya kiafya. Alaa na Gamal Mubarak wanakabiliwa na mashtaka kama hayo ya baba yao.

Jinsi watu waliyopokea

Mchora katuni wa Brazil Carlos Latuff [5] aliweka kumbukumbu ya wasaa huo kwa namna yake,alichora mifululizo ya series [6] katuni [7] .

Mubarak Before and After Jan25 Revolution [7]

Michoro ya kumwonyesha Mubarak Kabla na Baada ya Mapinduzi ya Januari 25, imechorwa na Carlos Latuff

Nyingi ya Twita za hivi punde zilizotumwa katika siku mbili zilizopita nazo zilihusu kukamatwa kwa Mubarak na kutiwa kizuizini.

@engmtm [8]: Natamani ningeweza kumhoji #Mubarak mimi mwenyewe :D

Ujumbe wa sauti iliyorekodiwa [9] wa Mubarak[ar], ambao aliutuma Al-Arabiya (Kituo cha Habari za Televisheni) [10] ambaoulitokea kuwa kumbe uliandikwa [11] na mwanasheria maarufu wa Misri, Fareed El-Deeb, unasemekana kuwa ni msumari wa mwisho kwenye jeneza la Mubarak:

@Eslam_Foad [12]: شكرا للراجل اللي بيكتب خطابات مبارك من غيرك الثورة ماكنتش هتنجح
@Eslam_Foad [12]: Asante kwa mtu anayeandika hotuba za Mubarak, bila wewe pengine mapinduzi yasingalipata mafanikio kama haya.

Katika majuma machache yaliyopita, Gereza la Torah liligeuka siyo tu kuwa makazi ya watoto wa Mubarak, lakini pia limekuwa makazi ya nguzo (watu) wengi tu waliokuwa katika utawala wa Mubarak. Kupitia Twita, watu hawakuiachia fursa ya kufanyia mzaha jambo hili:

@MAkhnoukh [13]: عاجل تم تغيير سجن طرة لدولة طرة ويطالب سكانها بالاستقلال فهى دولة متكاملة لها رئيس وحكومة ومش عايزين شعب خالص
@MAkhnoukh [13]: Habari za hivi punde: Gereza la Torah hivi sasa linaitwa Jamhuri ya Torah na raia wake wanadai uhuru. Lina rais wake, serikali yake na kwa hakika hawataki kuwa na watawaliwa pale.
@Aessameldin [14]: جمال هيمثل فى السيزون الجديد من بريزون بريك و خديجة فى ديسبيريت هاوس وايفز
@Aessameldin [14]: Gamal Mubarak atakuwa nyota katika (filamu ya) Kujaribu Kutoroka Gerezani, na mkewe Khadija atajiunga na timu ya wapiga picha wa (filamu ya) Wake Wasio na Matumaini.

Akaunti za uongo kadhaa za Twita za Mubarak [15], familia yake (Suzanne Mubarak [16], Alaa Mubarak [17], Gamal Mubarak [18] na mkewe Khadija [19]), na za watu katika utawala wake (Fathi Sorour [20], Safwat El-Sharif [21] na Ahmed Nazif [22]) zimetengenezwa ili kuwakebehi.

Car carrying banners in celebration of the detention of Mubarak, posted on Yfrog. [23]

Picha ya gari likiwa limebandikwa matangazo ya kusherehekea kutiwa kizuizini kwa Mubarak, na kutumwa katika posted on Yfrog.

Hatimaye, pamoja na yote haya, na licha ya orodha ya upingaji wa mafanikio ya Mubarak [24] kama ilivyoandikwa na Ahmed Hayman, bado kuna wanaomwonea huruma rais huyo wa zamani:

@MontuEssam [25]: اقسم بالله انا بقيت حزين انى مصرى لما اشوف كميه الغل والحقد والتشفى اللى فى شعب مص هو ايه اللى بيحصل هو احنا وحشين من جوانا اوى كدا؟
@MontuEssam [25]: Ninaapa kwa Mungu, hivi sasa ninajisikia mwenye huzuni kwa kuwa raia wa Misri, hasa kwa sababu ya yale ninayoyashuhudia sasa. Inakuwaje kwamba watu wa Misri wamebeba chuki nyingi kiasi hiki, na wanataka kulipiza kisasi! Kuna nini? Je, sisi kweli ni wabaya kiasi hicho?

Makala hii ni sehemu ya habari maalumu tunazowaletea kuhusu Mapinduzi ya Misri ya Mwaka 2011 [1].