- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

Japani: Tsunami yaathiri eneo la pwani, yaacha kila kitu kimeharibiwa

Mada za Habari: Asia Mashariki, Marekani ya Kaskazini, Japan, Marekani, Habari za Hivi Punde, Majanga, Mazingira, Mwitikio wa Kihisani, Uandishi wa Habari za Kiraia

Makala hii ni sehemu ya habari maalumu za Tetemeko la Japani 2011 [1].

Kufuatia tetemeko kubwa kuwahi kutokea nchini [2], Japani imekumbwa na tsumani mbaya zaidi iliyowahi kutokea. Watu wengi nchini kote wameganda kwenye luninga zao wakati vipande vya habari vinavyoonesha tsunami lenye urefu wa zaidi ya mita 7 kwenda juu likisomba magari na majengo. Wakati huo huo, maeneo mengine ya dunia yanajiandaa kwa matukio mabaya zaidi, Hawaii imetoa amri ya kuhama kutoka kwenye maeneo ya pwani [3] na tahadhari zimetolewa katika nchi zisizopungua 20 [4]. Jarida la The Guardian linatoa habari za mpya kadiri zinavyojitokeza [5] kuhusiana na janga hilo.

http://www.youtube.com/watch?v=rWgvX1FGK4I [6]
http://www.youtube.com/watch?v=lSimeWFiuYc [7]

Picha ya wimbi kubwa la bahari mjini Ibaraki [8] (kupitia @gakuranman [9]):

Baadhi ya ujumbe kwenye twita.

Tinystar323 anaandika [10]:

津波は「波」じゃなくて、「コンクリートの壁が猛スピードで突っ込んでくる物」だと思って下さい。人間にどうにか出来る代物じゃないです。絶対に興味本位で見に行ったりしないで下さい。

Tafadhali usifikirie tsunami kama “mawimbi”, lakini (ifikirie) kama “kuta nzito zinazoporomoka kwa kasi ya ajabu kabisa”. Wanadamu hawezi kupambana nayo. Tafadhali usiende nje kuangaia kukidhi dukuduku.

Taarifa isiyothibitishwa kutoka @nishi_0024 [11] ikidai kwamba kituo cha mkutano cha Pacifico Yokohama hakipokei tena watu:

【緊急拡散】パシフィコ横浜は津波の危険があるため、受け入れ中止だそうです!

Pacifico Yokohama [kituo cha mikutano] kimo kwenye hatari ya kukumbwa na tsunami, wamesitisha kupokea watu!

Kutoka @edamamicky [12], mwathirika wa tsunami:

津波被害あり。自宅2階にて母と弟と近所の男性一名と救助を待っています。怪我はありません。1階は浸水して自力では外に出れません。電話も繋がりません。

Mwathirika wa tsunami hapa. Nipo eneo la makazi la 2F pamoja na mama yangu, kaka na majirani tukingoja kuokolewa. Hakuna majeruhi. Eneo la makazi la 1F limegharikishwa na maji na hatuwezi kutoka nje wenyewe. Vilevile mawasiliano ya simu yamekatika.

Kwa habari za hadi dakika iliyopita kuhusiana na hali ya mambo baada ya tetemeko, fuatilia chanzo rasmi cha habari [13] cha NHK.

Makala hii ni sehemu ya habari maalumu za Tetemeko la Japani 2011 [1].