- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

Japan: Jijini Tokyo baada ya Tetemeko la Ardhi

Mada za Habari: Japan, Majanga, Uandishi wa Habari za Kiraia

Makala hii ni sehemu ya habari maalumu za Tetemeko la Japani 2011 [1].

Siku ya Ijumaa, Machi 11, 2011 saa 8:46:23 mchana kwa saa za Japani, , tetemeko lenye kipimo cha 8.9 liliikumba Japan [2], hili ni tetemeko kuwahi kutokea katika historia iliyorekodiwa.

(Wakati makala hii inaandikwa kwa mara ya kwanza ilikuwa) imekuwa zaidi ya saa tano tangu tetemeko hilo litokee, na Wajapani wengi bado wanajaribu kurudi nyumbani kwa miguu. Mfumo wa treni umefungwa kwa siku moja.

@Kenji_Hall [3]:

Bado ninatembea kama ilivyo kwa kila mmoja jijini Tokyo. Treni zimesisimama. Teksi zimejaa. Foleni ndefu kwenye vituo vya basi. Ninahitaji kwenda kaskazini lakini nimekwama katikati ya jiji Tokyo. #quake12

Njia za mabasi, na @durf [4]

Mtumiaji wa twita @oohamazaki [5] anakusanya Ramani za Google ili kuonyesha sehemu zilizo salama katika Jiji la Tokyo.


より大きな地図で 東京都内避難場所 [6] を表示

Jua limekuchwa na hoteli, shule, mikahawa, na vinginevyo vinafungua milango yao.

@tsuyoshi_ide [7]:

【拡散希望】 新宿南口の文化服装学院が、非常食と宿泊受け入れ準備中です! #jishin #jisin #shinjyuku

Bunka Fashion College [8] karibu na Lango la kutokea la Shinjuku Kusini wanacho chakula na wanajiandaa kuwapokea watu kwa ajili ya usiku.

@gmsq [9]:

【拡散希望】立教大学は一晩中教室を開放することを決定しました!宿泊可能です! 大学関係者以外の方ももちろん利用可能なので、お困りの方は立教大学までいらして下さい!僕宛にリプライいただければ、なにかお困りの際はお手伝いします! #rikkyo_raise

Tafadhali sambaza ujumbe! Chuo Kikuu cha Rikkyo kinafungua madarasa yote kwa ajili ya usiku huu. Yeyote yuko huru kukesha humo. @jibu kwangu kama unahitaji msaada wowote.

Picha na Mhariri mwenza wa Global Voices katika Kijapani Scilla Alleci

Makala hii ni sehemu ya habari maalumu za Tetemeko la Japani 2011 [1].