- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

Côte d'Ivoire: Gbagbo agoma, Waafrika waandamana

Mada za Habari: Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara, Cote d'Ivoire, Maandamano, Mahusiano ya Kimataifa, Siasa, Uandishi wa Habari za Kiraia, Uhamiaji na Uhamaji, Vita na Migogoro

Makala hii ni miongoni mwa makala zetu maalumu kuhusu Vurugu za mwaka 2011 nchini Ivory Coast [1]

Wakati Rais wa zamani wa Côte d'Ivoire Rais Laurent Gbagbo akiwa bado amejichimbia ndani yahandaki [2] nchini humo, akigoma kukamatwa kwa kuendelea kukataa kushindwa kwenye uchaguzi wa mwaka 2010, ushiriki wa Ufaransa katika harakati za kumng’oa zinasababisha miitikio miongoni mwa wanasiasa na raia wa Ufaransa [3] [fr], pamoja na jamii ya Waafrika waishio Ufaransa. [4].

Pro-Gbagbo protests in Paris, France, March 26, 2011. Image by Flickr user anw.fr (CC BY-NC-SA 2.0). [5]

Maandamano ya wanaomwunga mkono Gbagbo Jijini Paris, Machi 26, 2011. Picha ya mtumiaji wa Flickr anw.fr (CC BY-NC-SA 2.0).

Kuanzia Paris mpaka Douala

Siku ya Aprili 6, 2011, maandamano yaliandaliwa mbele ya Jengo la Bunge la Ufaransa jijini Paris, kama yanavyooneshwa na mfululizo wa video zilizowekwa na mtumiaji wa You tube Mamou922 [6] Katika video hii inayofuata, tunaona umati mkubwa wa watu ukielekea viliko vikosi vya Ufaransa vinavyolinda jengo la umma:

Siku ya April 5, 2011, mjini Douala, mji mkuu wa kibiashara wa Kameruni, Madereva wa Moto Taxi walikusanyika katikati ya mji kwa minajili ya kuonesha wanavyomwuunga mkono Laurent Gbagbo. Video ifuatayo iliwekwa kwenye Wat TV [7] na Gri-Gri International [8], blogu ya habari:

Mmoja wa waliohojiwa kwenye video hiyo anaeleza:

Tatizo la Côte d'Ivoire linawagusa Waafrika wote […] tunaionya jamii ya kimataifa na Ufaransa kusitisha mara moja kile wanachokifanya nchini Côte d'Ivoire […]

Akirejea kile kilichotokea Kameruni wakati wa vita vya kupigania uhuru nchini humo, anaongeza:

Leo tunaelewa kuwa ni ukweli mtupu kwamba Ufaransa iliwaua wazazi wetu miaka 50 iliyopita

Tatizo la Majengo ya Ubalozi

Waziri wa Ulinzi wa Ufaransa Gérard Longuet aliiarifu [12] [fr] Tume ya Mambo ya Nje ya Baraza la Seneti la Ufaransa asubuhi ya Aprili 7, 2011. Aliarifu kwamba vikosi vinavyomlinda Laurent Gbagbo ni kadri ya 1000 na akaeleza kwamba ugumu mkubwa kuhusiana na namna ya kuyavamia makazi ya Rais sehemu ya Cocody (anakojificha Gbagbo) ni uwapo wa ofisin nyingi za kibalozi zinazolizunguka eneo hilo. Maeneo hayo yamekuwa kwa haraka ni mbinu na ujanja wa kujilinda.

Gazeti la Ufaransa JDD liliweka kwenye ukurasa wake wa Facebook uokoaji [15] uliofanywa na vikosi vya majeshi ya UNICORN kwa balozi wa Japani ili kumtoa kwenye makazi yake mjini Abidjan, ambayo yalivamiwa na wanajeshi mamluki usiku wa April 6. Chanzo cha Video hii ni Wizara ya Ulinzi ya Ufaransa:

Kwa mujibu wa Jeune Afrique [16], tjarida kubwa la Kiafrika litokalo katika lugha ya kifaransa, vikosi maalumu 100 vya Angola [17] [fr] vinayaongezea nguvu majeshi ya Gbagbo wanaolilinda handaki ambalo kiongozi huyo wa zamani anaendelea kujifichia humo.

Makala hii ni miongoni mwa makala zetu maalumu kuhusu Vurugu za mwaka 2011 nchini Ivory Coast [1]