Habari kutoka 17 Aprili 2011
Naijeria Yapiga Kura 2011: Maoni kutoka kwenye Uchaguzi
Wanaijeria walipiga kura jana katika uchaguzi wa tatu wa rais tangu taifa hilo lilipoingia kwenye utawala wa kiraia mwaka 1999. Mpaka sasa, uchaguzi huo umeelezwa na wengi kuwa ulikuwa wa mafanikio, huku kukiwa na taarifa za ghasia za hapa na pale pamoja na hitilafu za upigaji kura. Vyanzo vya habari vimeripoti kuwa watu wengi walijitokeza, foleni zenye kufuata utaratibu, na wapiga kura kusubiri hadi uchaguzi utakapomalizika ili kuhakikisha kwamba kura zao zimehesabiwa. Wanablogu wanajadili.
Attahiru Jega: Kiongozi wa Tume ya Uchaguzi ya Naijeria au Mtekaji?
Watumiaji wa mtandao wa Intaneti wa Naijeria wanadai kwamba utando usio na mwangaza wa siasa za Naijeria unahitaji mwamuzi mwenye uwezo wakati wa Uchaguzi wa 2011. Attahiru Jega, bosi wa tume ya uchaguzi itabidi adhihirishe katika majuma yajayo kuwa uchaguzi utakuwa mwepesi kama A, B, C.