- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

Urusi: Mlipuko Katika Kiwanja cha Ndege cha Domodedovo

Mada za Habari: Ulaya Mashariki na Kati, Urusi, Habari za Hivi Punde, Safari, Sheria, Uandishi wa Habari za Kiraia, Vita na Migogoro, RuNet Echo

Bomu lililipuka katika kiwanja cha ndege cha Domodedovo mjini Moscow, kwa uchache vifo vya kadri ya watu kumi vimeripotiwa. Mmiminiko wa Twita unapatikana hapa [1] (RUS) na hapa [2] (RUS, ENG). @ann_mint [3], ambaye anafanya kazi Domodedovo, alikuwa ni mmoja wa watumiaji wa kwanza wa Twita kuripoti juu ya mlipuko huo; “Kuna wahanga #domodedovo [4] tuombeeni,” aliandika [5] (ENG) dakika chache zilizopita.