Tunisia: Anonymous Dhidi ya Ammar – Nani Atashinda Vita ya Kuchuja Habari?

Bango la Anonymous, likitoa wito kwa wanaharakati kushambulia mitandao yaa serikali ya Tunisia

Kichuja habari cha Tunisia, ambacho kwa kawaida hujulikana kama Ammar, kinaeendelea kutishia kuziharibu na kuzifunga anuani za wanaharakati wa mtandaoni, katika nchi hiyo ambayo imekuwa ikishuhudia wimbi la maandamano tangu katikati ya mwezi Desemba. Ni leo tu, wanaharakati wamedai kwamba serikali imeingilia anuani zao za barua pepe,na kuziingilia blogu na mitandao yao ya kijamii, na kuzizuia zisifanye kazi. Hatua hii inaonekana kuja kama kulipiza kisasi kwa shambulio lililofanywa na kikundi cha wanaharakati wa mtandaoni wanaojulikana kama Anonymous, ambalo lililenga njia na mitandao ya muhimu ya Serikali ya Tunisia.

Shambulio hilo kwa anuani za wanaharakati si jambo geni kwa Tunisia na wanaharakati wa mtandaoni. Nchi hiyo inaelezewa kama nchi ya kipolisi na adui wa mtandao wa Intaneti na pia mkandamizaji wa vyombo vikuu vya habari kwani hata Orodha ya Uhuru wa Vyombo vya Habari  iliipatia alama -10 mwaka 2010, ambapo iliporomoka kutoka nafasi ya 154 mpaka nafasi ya 164 kidunia.

“Nchi hiyo inaendelea kuporomoka kwenda kwenye nafasi za chini zaidi za Orodha kwa sababu ya sera zake za kigandamizaji zinazotekelezwa na watawala wa serikali mjini Tunis dhidi ya mtu yeyote anayetoa wazo kinyume na lile la utawala ulioko madarakani,” inasema taarifa hiyo.

Kwa mujibu wa Gawker, Anonymous, kundi lenye muundo-huru la wanaharakati wenye utaalamu wa kuingilia mawasiliano binafsi ya mtandaoni pamoja na walinzi sungusungu, walishambulia tovuti za serikali, pamoja na ile ya Rais, Waziri Mkuu, soko la hisa na wizara kadhaa, wakipinga kitendo cha Tunisia kuingilia utumiaji wa mtandao maarufu wa kutoa taarifa za siri za serikali duniani uitwao Wikileaks, kufuatia sakata la kuingiliwa kwa mawasiliano ya siri, na dhidi ya uingiliaji wa mitandao binafsi wenye ukandamizaji unaofanywa na nchi hiyo.

Katika AnonNews.org, , jukwaa la mtandaoni kwa “wanaharakati wa kupinga kuingiliwa kwa mawasiliano,” tangazo lifuatalo katika kile kinachojulikana sasa kama Operesheni: Tunisia, lilitolewa:


Wakati kwa ajili ya ukweli umefika. Wakati kwa watu kujieleza kwa
uhuru na kusikilizwa kutoka kokote duniani. Serikali ya Tunisia
inataka kutawala wakati uliopo kwa kutumia uongo
na taarifa za kupotosha ili kulazimisha mustakabali wanaoujua wao kwa kuwaficha ukweli
wananchi. Hatutabaki kimya haya yanapotokea.
Anonymous imesikia dai la uhuru wa watu wa Tunisia.
Anonymous ina nia ya kuwasaidia watu wa Tunisia katika vita hii dhidi
ya ukandamizaji. Itafanyika.
 Itafanyika.
Hili ni onyo kwa
serikali ya Tunisia: mashambulizi dhidi ya uhuru wa kujieleza na wa habari
kwa watu wake havitavumiliwa. Taasisi yoyote inayohusishwa na kuingilia mawasiliano binafsi
ya watu italengwa na haitaachiwa mpaka serikali ya Tunisia
isikilize dai la uhuru wa watu wake. Hiyo iko mikononi mwa
serikali kusimamisha hali hii. Achia huru mtandao na mashambulizi
yatakoma, endeleza nia hiyo na hatua hii itakuwa mwanzo tu.

Orodha ya mitandao ya serikali iliyokwisha kushambuliwa inaweza kupatikana hapa.

Na kwa mujibu wa wanaharakati waliopo nchini humo, serikali ilijibu mashambulizi kwa ‘kuziteka’ anuani za barua pepe za wanaharakati, ikiwa ni pamoja na zile za wanasheria na za waandishi, na kuweza kuzitumia blogu zao na mitandao ya kijamii, kama vile Facebook,na kuzizuia zisiweze kufanya kazi.

Mwanablogu wa Tunisia Astrubal, mhariri mwenza wa Nawaat.org, anasema dalili nyingi zinaelekeza kwenye shambulizi linaloratibiwa na serikali ya Tunisia katika jaribio la kuharibu mawasiliano binafsi ya wanaharakati. Anaandika [Fr] :

Il s’agit vraisemblablement d’une campagne destinée surtout à subtiliser les log et mot de passe des utilisateurs afin de fouiner dans leurs messages privés. Par ce moyen, la police, en quête de renseignements, chercherait à s’infiltrer dans les comptes des utilisateurs pour savoir qui communique avec qui et sur quel sujet. Il s’agirait en somme de chercher à démanteler ces réseaux de journalisme citoyen qui se sont constitués spontanément suite aux mouvements de contestation de Sidi-Bouzid.

Depuis les événements de Sidi-Bouzid qui ont montré, en effet, l’importance des réseaux sociaux quant à la circulation de l’information, des perturbations récurrentes du réseau ont été constatées. Pour le cas de Facebook, les connexions en HTTPS notamment pour se logger sont souvent impossibles à établir. Le pouvoir tunisien n’a pas osé, comme il l’a fait par le passé, bloquer les services du réseau social le plus utilisé par les Tunisiens. Cette fois-ci, il semble qu’il chercherait plutôt à atteindre directement ceux qui l’utilisent pour faire circuler l’information, plutôt que de s’attirer les foudres de tous les utilisateurs par un blocage total de Facebook.

En tout état de cause, nous rappelons à tous les utilisateurs de Facebook et, a fortiori, s’ils se connectent à partir de la Tunisie : NE VOUS CONNECTEZ JAMAIS à partir d’une page non sécurisée. Même si vous n’avez rien à cacher, n’oubliez jamais que vous êtes également dépositaire de la confiance des personnes qui vous envoient des messages privés. Même si, vous, ça vous est égal que l’on puisse fouiner dans vos messages privés, on se doit, tout un chacun, d’honorer la confidentialité des messages privés que nous recevons.

Inaelekea kampeni hii inalenga kwenye kuiba nywila na majina yanayotumiwa na watumiaji mitandaoni ili kupitia jumbe zao binafsi. Polisi inatafuta namna ya kuingia katika akaunti za watumiaji na kujua nani huwasiliana na nani na huongelea nini. Huku wakiwana lengo kuu la kuvunja mitandao wa waandishi wa kiraia iliyoanza kwa nguvu kubwa kufuatia maandamano ya Sidi Bouzid.

Matukio ya Sidi Bouzid, yamethibitisha umuhimu wa mitandao ya kijamii katika kuruhusu msambao endelevu wa habari. Lakini tangu kuanza kwa matukio hayo, kuharibiwa mara kwa mara kwa mitandao hiyo kumeonekana. Katika kisa cha Facebook, viunganisho, ikijumuisha matumizi ya HTTP (viungo salama) kuingia mtandaoni, haikuwa rahisi kuiunganisha. Utawala wa Tunisia haujathubutu, kwa wakati huu, kufunga huduma nzima ya Facebook, ambao ni mtandao maarufu zaidi nchini Tunisia. Wakati huu, serikali inaonekana kuwalenga bayana wale wanaoutumia mtandao huo kusambaza habari.

Kwa sababu yoyote, tunawakumbusha watumiaji wote wa Facebook, hasa kama wanaunganishwa kutokea Tunisia: USIJIUNGE kutokea kwenye ukurasa usio salama. Hata kama huna cha kuficha, usisahau kwamba uliaminiwa na watu wanaokutumia jumbe binafsi. Hata kama wazo kuwa mtu fulani anaweza kuingilia anuani yako ya barua pepe na kusoma jumbe zako halikusumbui, ni lazima uheshimu faragha ya jumbe binafsi unazozipokea.

Habari za shambulizi dhidi ya anuani za wanaharakati punde tu zilipata upenyo wa kusambaa kwenye mitandao ya kijamii.

@SBZ_news anataarifu:

Wanablogu wanapokea shambulio kutoka kwa polisi wa mtandaoni, wanaojaribu kuingilia mawasiliano ya kila aliyeunga mkono au

Mwanaharakati wa Kimauritania Naser Weddady anaandika kwenye twita:

Kwa kutumia mwitikio kutoka kwa watu walio mwelekeo wa mambo unajitokeza: Anuani za Facebook zilizoingiliwa zinahusiana na anuani ya Yahoo

Na anaongeza:

Mwanaharakati wa

@ & mwandishi wa habari @ wanalengwa kwa sababu ya kuongea na chombo cha habari cha kigeni

Wakati @spiralis1337 anaonya:

Polisi ya Tunisia inaingilia anuani za Facbook kukusanya taarifa Jilinde

And Seifeddine Ferjani anaongeza:

uingiliaji wa barua pepe na anuani za Facebook, imethibitisha serikali ya Benali ni kampuni ya kihalifu

Na kama hiyo haitoshi, katika mwendelezo zaidi, @nayzek anaandika kwenye twita:

RT @ haha Sasa maafisa (?) wanaonekana kuwaita watu mmoja mmoja kuwaomba kuacha kutumiana video za kwennye mtandao wa FB :)

Kwa twita za Operesheni: Tunisia, angalia kwenye alama hii #optunisia
Na kwa twita zaidi kuhusu Sidi Bouzid na Tunisia, angalia alama #SidiBouzid na #Tunisia, ambazo huhuishwa mara kwa mara na miendelezo ya karibuni zaidi inayoendelea mahali husika.

Fasiri kutoka Kifaransa imetolewa na Hisham.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.