Dunia ya Uarabu: “Acheni Kulia Juu Sudani”

Kura ya maoni kwa ajili ya uhuru wa Sudani ya Kusini leo imeiweka nchi hiyo kwenye uangalizi wa karibu miongoni mwa watumiaji wa twita wa Kiarabu. Kuanzia Saudia mpaka Palestina, watumiaji Twita wa Kiarabu wanajadiliana kuhusu mshikamano, kugawanyika na rasili mali za Sudani.

Kura hii ya maoni ni sehemu ya Makubaliano ya Naivasha yaliyofanyika mwaka 2005 baina ya serikali kuu ya Khartoum na Chama cha SPLA (Sudan People’s Liberation Army) na inaweza kusababisha kumeguka kwa Sudani ya Kusini kutoka kwenye nchi ya Sudani ya leo.

Kutoka Saudi Arabia, Omar ALattas anauliza:

متي ستظهر نتايج انتخابات السودان
Matokeo ya kura ya maoni ya Sudani yatatangazwa lini?

Na anahitimisha:


اليوم ستصبح الجزائر أكبر دولة عربية عوضا عن السودان بلد المليون ميل
Leo nchi ya Aljeria itachukua nafasi ya Sudani kama nchi kubwa zaidi ya Kiarabu

Bader Aujan, kutoka Saudi Arabia pia, ana mtazamo chanya kuhusu mustakabali (wa Sudani):

ألمانيا اتحدت بعد أنقسام وهونغ كونغ عادت للصين بعد أقتطاع وستعود السودان إن شاء الله وسيكون الأنفصال دافعاً قوياً للتنمية

Ujerumani iliungana tena baada ya kugawanyika; Hong Kong ilirudi China baada ya kujitenga; na ninategemea vilevile kwamba Sudani itakuwa hivyo hivyo. Ninatumaini utengano huu utakuwa kichocheo muhimu kwa ajili ya maendeleo.

Halafu anaongeza:

Ujerumani ni mfano mzuri wa namna nchi zilizowahi kujitenga siku moja zilikuja kuungana tena kwa amani. haiwezi kuwa tofauti katika hili!

Na Mohamed Osman, ambaye pia anatuma habari kwa njia ya Twita kutoka Saudi Arabia,, anawasihi wasomaji wake:

نرجوا من الأخوة العرب الأعزاء عدم النياحة والردح في موضوع السودان، 26 سنة من الحرب وأنتم صامتون فأكملوا صمتكم
Wapendwa ndugu zangu wa Kiarabu, tafadhali acheni kulia na kutengeneza mizengwe kwa yanayotokea Sudani. Kulikuwa na mapigano ya miaka 26 ambapo ninyi mlinyamaza. Tafadhali endelezeni kimya chenu leo.

Mpalestina Bahaa AlKayyali anaombea umoja wa Sudani

الوحدة للسودان… الوحدة
Umoja kwa Sudani…umoja

Wakati kutoka Jordani, Ali Dahmash anaonesha Rasilimali zenye utajiri za Sudani:

Hivi mnafahamu kwamba asilimia 70 ya uzalishaji wa Mafuta ya Sudani yako kusini? Si ajabu John Kerry & wanasiasa wa Kimarekani wanaunga mkono utengano!

Na huko huko Saudi Arabia, Bandar Bin Naif, anajiuliza:

قمر صناعي أنشىئ خصيصا لمراقبه الاستفتاء والأحداث في السودان، هل هو حبا في السودان أم مباركة للإنفصال
Chombo cha kurekodi mawasiliano angani (Setilaiti) kilirushwa mahususi kwa ajili ya kufuatilia kura ya maoni na maendeleo ya nchi ya Sudani. Je, hili linafanyika kwa kuipenda Sudani ama ni baraka kwa ajili ya kujitenga

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.