- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

Peru: Kampeni ya Kuzuia Kufungwa kwa Maktaba ya Amazon

Mada za Habari: Amerika Kusini, Peru, Fasihi, Habari za wenyeji, Harakati za Mtandaoni, Sanaa na Utamaduni, Uandishi wa Habari za Kiraia

Juan Arellano wa Globalizado [1] [es] anaripoti juu ya kampeni ya kuzuia kufungwa kwa maktaba huko Iquitos, Peru [2], maktaba ambayo inatilia mkazo vitabu na masuala yanayohusu Amazon. Maktaba hiyo ni ya pili kwa umuhimu katika masuala ya Amazon huko Marekani ya Latini.