Haiti: Video Inayookoa Maisha

Mganga nayeishi jijini Fransisco ambaye pia ni mwanablogu Dkt. Jan Gurley amezuru Haiti mara mbili tangu lilipotokea tememeko la ardhi la Januari 12 ili kuwahudumia watu kwa kujitolea. Ziara yake ya pili ilikutana na tukio la maambukizi ya kipindupindu ambalo limetwaa maelfu ya maisha na kusababisha maelfu wengine kulazwa hospitali tokea kesi ya kwanza ilipotokea mnamo Oktoba 19, 2010.“Kipindupindu ni ugonjwa mbaya ulio katika kiwango cha kimbunga kikubwa,” anaandikaDkt Gurley (Doc Gurley, kama anavyojulikana katika ulimwengu wa blogu):

Unaweza kufariki ndani ya masaa 3, huku maji yote mwilini yakitoka kwa njia ya choo. Kijamii, nchini Haiti, nilibaini mnamo mwezi Februari kuwa tayari kulikwishakuwa na unyanyapaa mkubwa unaoambatana na ugonjwa wa kuharisha. Haistaajabishi, kwa kweli, kama ukifikiria ukweli wa kuishi kwenye maegesho ya magari bila ya maliwato huku ukiwa umezungukwa na mamia ya watu. Na hivi sasa kuna wasiwasi kuwa huenda kipindupindu kililetwa nchini Haiti na wafanyakazi wa kimataifa waliokuja kusaidia..Ukiachilia mbali idadi kubwa ya vifo (taarifa zinasema idadi ya vifo vilivyotokana na kipindupindu ni 200 mpaka 500 kwa mujibu wa ripoti za Urusi), je kwa kiasi gani imani iliyopo, na ile inayotarajiwa inaweza kuvunjwa na tukio kama hili?

Doc Gurley alitafuta kwenye mtandao video ya maelekezo ya jinsi ya kujiongezea maji mwilini kwa njia ya kinywa (ORT) ambayo angeliwaachia wafanyakazi wenzake pamoja na wagonjwa. Ufahamu wa jinsi jinsi ya kujiongezea maji mwilini (ORT) unaweza kuokoa maisha, kwani vifo vingi vinavyotokana na kipindupindu hutokana na kupoteza maji mwilini. Doc Gurley anawakumbusha wasomaji wake kwamba hata nchini Haiti video inaweza kuwa zana yenye ufanisi mkubwa katika kueneza habari: “Huko watu wanazo simu za mkononi zenye uwezo wa kutuma ujumbe wa maandishi, na kila mmoja ana anwani ya barua pepe. Wafanyakazi wa mashirika ya misaada wanazo simu zenye akili (simu za kisasa zaidi) ambazo zinaweza kuonyesha video, na watu huko Haiti, kama ilivyo hapa, wanapenda kukusanyika na kuangalia skrini ndogo.”

Wakati utafiti wake wa kwwenye mtandao uliposhindwa kuambulia chochote bali video moja tu kwa lugha ya KiHausa pamoja na nyingine za matangazo ya biashara yaliyojificha yanayotangaza vinywaji vya aina ya Getorade, Doc Gurley aliwakusanya marafiki wachache pamoja na kutengeneza video inayoonekana hapo chini. Kwa kiasi kikubwa haina maneno, na hivyo kuifanya kuwa sawia kwa matumizi katika nchi yoyote, na inaonyesha jinsi ya kutengeza chumvi za kurejesha maji mwilini “kwa kutumia vifaa ambavyo mtu anayeishi katika jiji la bati anaweza kuvipata”, pamoja na chupa za maji na vifuniko vyake:

vifuniko 4 vya sukari, kifuniko 1 cha chumvi, maji safi ml 500 = uzima

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.