Habari kutoka 14 Novemba 2010
Ivory Coast: Wimbo Mpya Kwa Ajili Ya Uchaguzi wa Rais
Museke imeweka video ya wimbo mpya “Mpiga Kura” ulioandikwa maalum kwa ajili ya uchaguzi wa rais nchini Ivory coast. Wimbo huo unachezwa na Le Griot-Guére, Jackivoire, Soro Solo, na gitaa la kuongoza linapigwa na mpiga gitaa gwiji kutoka Kongo, Huit-kilos.
Mexico: Mwanamke wa Miaka 20 ni Mkuu Mpya wa Polisi katika Mji wa Kaskazini mwa Mexico
Valles García ni mwanamke aliyeolewa mwenye umri wa miaka 20 anayesoma masomo ya makosa ya jinai na uhalifu; vile vile ni mkuu mpya wa polisi wa Práxedis, Chihuahua, mji uliopo umbali wa kilometa 100 (maili 62) kutoka Ciudad Juárez, mji wenye uhalifu zaidi nchini Mexico.