- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

Jamaika: Banton Ajitayarisha Kwenda Mahakamani

Mada za Habari: Nchi za Caribiani, Jamaica, Muziki, Sheria, Uandishi wa Habari za Kiraia

YardFlex.com [1] anaifuatilia kesi ya umiliki wa madawa ya kulevya inayomkabili Buju Banton na ambayo itaendeshwa siku ya Jumatatu huko Marekani. Kutokana na taarifa zinazosema kwamba washtakiwa wenzake wawili wameamua kuwa mashahidi wa serikali (upande wa mashtaka) blogu hiyo inasema: “Siku mbili zinazofuata zitakuwa ni za muhimu sana kwani Buju na wanasheria wake wanajipinda na kutayarisha kueleza habari ambazo hazikuelezwa hapo awali.”