- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

Bahraini: Ali Abdulemam, mwanablogu na mchangiaji wa Global Voices akamatwa

Mada za Habari: Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini, Bahrain, Uandishi wa Habari za Kiraia

Ali AbdulEmam


Ali Abdulemam, mwanablogu [1] maarufu wa nchini Bahraini na mwandishi wa Kitengo cha Utetezi cha Global Voices [2], amekamatwa mapema leo na mamlaka ya nchi ya Bahraini kwa kile anachotuhumiwa nacho kwamba anasambaza [3] “habari za uongo” kupitia mtandao wa BahrainOnline.org [4], ambao ni moja ya mitandao maarufu zaidi nchini humo inayopigania kuwepo kwa demokrasi zaidi, huku kukiwa na harakati mbaya zaidi ya zote [5] za Serikali ya nchi hiyo za kuendeleza ubaguzi mbaya wa kiimani kwa miaka mingi sasa [6], pamoja na madai ya kuwepo kwa mtandao wa kigaidi [7] unaowahusisha wanasiasa na wanaharakati wa haki za binadamu [8] kadhaa. Mtandao huu wa BahrainOnline unachujwa sana na serikali ya Bahrain. Alituma barua-pepe mapema leo akieleza kwamba alipigiwa simu na maafisa wa usalama wa taifa wa Bahraini muda mfupi kabla hajakamatwa, na baada ya hapo walimkamata wakisingizia kwamba alikuwa akijaribu kutoroka [9].

Inasemekana kwamba serikali ya Bahraini [10] ina rekodi ndefu ya utesaji wale wanaoonekana kuwa wakorofi, http://bit.ly/9kZyJQ [11] na vipindi vinavyorushwa na Televisheni vinavyochochea chuki na ubaguzi wa kidaraja ili kuhalalisha harakati zake za kukomesha upinzani. [12]

Ali aliwahi kukamatwa hapo kabla kwa ajili ya habari aliyowahi kuchapisha kwenye mtandao wake [13], na amekuwa mchangiaji wa makala katika Kitengo cha Utetezi cha Global Voices [2] na vilevile katika kile cha Lingua ya Kiarabu ya Global Voices [14].

Habari mpya #1:

Kampeni ya kwenye mtandao inayotaka aachiwe huru ipo hai [15] sasa.

Habari mpya #2:

BahrainOnline.org [16] imezimwa.