- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

Moroko: Mtoto Mwanablogu Asalimia Ulimwengu

Mada za Habari: Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini, Moroko, Elimu, Uandishi wa Habari za Kiraia, Vijana

[1]Wakati Salma alipoanzisha blogu [2] [Ar] mwaka 2008, alikuwa na umri wa miaka 6 tu, inawezekana kuwa ndiye aliyekuwa mwanablogu mdogo kuliko wanablogu wote nchini Morocco. Aliisalimia dunia wakati ule kwa maneno haya:

مرحبا يا أصدقاء بكم في مدونتي
أنا اسمي سلمى
عمري ست سنوات ونصف
أدرس بالقسم الأول بمدرسة الجاحظ
أنشأ لي أبي مدونة هنا
لأكتب فيها اسمي والعنوان وأعرفكم بعمري
وأعرفكم باسم معلمي
وإذا كتبت كتابة ورسمت رسما
سوف أعملهم في المدونة

Hamjambo Rafiki zangu!
Karibuni kwenye blogu yangu.
Jina langu ni Salma.
Ninaumri wa miaka sita na nusu.
Nipo darasa la kwanza katika shule ya “Al Jahed”.
baba yangu ametengeneza blogu hii kwa ajili yangu, Ili niweze kuandika jina langu, umri na anwani, na niweze kukutambulisha wewe kwa mwalimu wangu.
Kama nitaandika au kuchora kitu nitakiweka kwenye hii blogu.

Salma siyo mwanablogu anayeblogu sana japokuwa wakati fulani fulani chini ya usimamaizi wa wazazi wake, huweza kuweka hadithi fupi fupi na picha za shule na walimu wake:

[3]

Salma akipokea tuzo shuleni

Baada ya ukimya (au usumbufu) wa muda mrefu Salma anapata mwamko tena (mwezi April) na kuwaandikia wasomaji wake juu ya mapambano ya kila siku darasani kwake. Anaandika:

زميلتي التي تجلس إلى جانبي في قسم اللغة العربية تحب نفسها كثيرا وتظن أنني ضعيفة وهي قوية لقد أصبحت أكره قسم اللغة العربية بسبب مضايقتها لي وهي تدفعني عند قراءة النص وتلدغني بأظافرها فلا أركز مع أستاذي الذي لايهتم بمشكلتي فأنا أشتكي له وهولا يعاقبها ولم ينقلها من قربي ولهذا قررت إذا لدغتني ألدغها و إذا دفعتني أدفعها ولن أسمح لها بمضايقتي مرة أخرى.

Mwenzangu anayekaa pembeni yangu wakati wa somo la Lugha ya Kiarabu ni mtu wakujiona sana na anafikiri mimi ni dhaifu na yeye anajiona ni mwenye uwezo sana. Nilianza kuichukia kozi hii ya lugha ya Kiarabu kwa sababu huwa ananibugudhi sana. Hunisukuma na kunifinya kila ninaposoma maandishi. Siwezi kutulia na kuwa makini huku mwalimu naye hajali kabisa matatizo yangu. Japokuwa nililalamika kwake, hakumuadhibu wala kumtaka akae sehemu nyingine. Na hiyo ndiyo sababu nimeamua kuwa kuanzia sasa, kama akinifinya nami nitamfinya, akinisukuma nami nitamsukuma na sitamruhusu anibugudhi tena.

Haijulikani wazi kuna wanablogu wangapi watoto katika ulimwengu wa wanablogu wa Morocco na baadhi wanaweza kuwa wanajiuliza je motto anapaswa awe na umri gain kabla ya kuanza kumiliki blog , lakini jambo lililowazi ni kuwa: uandishi wa dhati na wa moja kwa moja wa Salma unaifanya blogu yake iwe ya kipekee sana inayoleta hamasa kuifuatilia. Anapaswa kutiwa moyo na kufuatiliwa.