- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

Korea Kusini: Maombolezo ya Kitaifa ya Mwanamwali wa Kivietnam

Mada za Habari: Asia Mashariki, Korea Kusini, Vietnam, Haki za Binadamu, Uandishi wa Habari za Kiraia, Ubaguzi wa Rangi, Wanawake na Jinsia

Wanablogu wa Korea kusini wanaomboleza kifo cha mwanamwali wa Kivietnamu aliyeuawa na mume wake Mkorea mara tu baada ya kutua nchini Korea. Thach Thi Hoang Ngoc (umri miaka 20) alichomwa kisu na kupigwa hadi kufa na mume wake Jang Du Hyo (umri miaka 47) ambaye ana ugonjwa wa akili. Rais wa Korea Kusini Lee Myung-bak ametuma salamu za rambirambi kwa familia ya mwanamwali huyo kupitia balozi wa Korea nchini Vietnam . Wanablogu wa Korea, wakieleza machungu yao juu ya kifo hicho, waliitaka serikali ya nchi hiyo na polisi kutokuruhusu ndoa za holela kupitia mawakala ambao mara nyingi husababisha ndoa kuwa balaa kwa kuficha hali ya kiakili ya mume mtarajiwa, tabia na wasifu wake.

[1]

Picha ya skrini ya tovuti inavyoonekana baada ya kuingiza neno: wachumba wa Kivietnam.

Unapotafuta neno “wachumba wa Kivietnam” katika katika touvuti ya Naver.com, tovuti ambayo hutumiwa zaidi nchini Korea, karibu ya tisa katika kumi ni tovuti za kukutanisha wachumba, ambazo huwavutia vijana wa Kikorea kwamba wataweza kuijipatia wachumba wa Kivietnam au wa mataifa ya kigeni kwa bei nafuu.

Mwanamwali mdogo aliyeuawa, Ngoc alikuwa kati ya waliokuwa kwenye soko. Aliwasili Korea Julai Mosi, akaolewa na kuuawa tarehe 8. Hakuwa na uwezo wakuzungumza Kikorea na hakujua chochote juu ya udhaifu wa kiakili wa mumewe. Mumewe baadaye aliwajulisha polisi kuwa alikuwa ameagizwa na mzimu kumuuwa mkewe.

Wakorea wengi walichukizwa na habari hizo, wengi walilita tukio hilo kama aibu ya taifa,

Mwanablogu mwanasheria Springlaw aliandika [2] katika makala yake inayoanza kwa sentensi ‘ninaandika hili nikiamini kuwa tukio kama hili halitatokea tena’ na kwamba ndoa hiyo ilikuwa batili tokea mwanzo na iliharibiwa zaidi na kutokuwepo kwa mawasiliano, pia ujinga na uchelewaji katika kuchukua hatua.

신부를 거의 구매하다 싶이하고 서로 말이 통하지 않는 상태에서 폭력과 폭언으로 얼룩진 한국의 결혼생활 그 동안 많은 문제로 곪다 곪다 이제는 터져 버린거 같네요. 이제는 한 가정의 문제가 아닌 국가와 국가의 일로 커질거 같아 정말 걱정인 국제 결혼…이러한 잘못된 결혼 행태는 이미 전부터 사기결혼이라고 불릴만한 결혼들이 성행했었고, 그로 인해 가슴에 상처를 입은 해외 여성들이 많이 생겨났습니다. 이러한 문제를 이미 방송과 같은 언론에서 지적을 했지만 안일한 대처를 지속하던 국가와 국민들에게 베트남 신부의 피살이라는 부끄러운 일이 벌어졌습니다.

Tatizo lilikua na kukua zaidi na hatimaye likalipuka kama inavyoonekana katika kisa hiki. Wanaume wa Kikorea wamefikia kiasi cha ‘kuwanunua’ wenza wao na ndoa yao ikaishia kuwa na ugomvi, na matusi, katika hali ambayo ni vigumu wao kuelewana kutokana na kutoelewana lugha zao. Nina shaka hili litvuka mipaka ya familia na kuwa tatizo kati ya nchi…Vitendo hivi vya ndoa batili, vya kifisadi vimeenea na kukua kwa kuanzia zamani na wanawali wengi wa kutoka nchi za kigeni wameshaumizwa sana. Ni kweli kuwa vyombo vya habari vimeandika kuhusu hili, lakini watu wa Korea na serikali hawakuwajibika hadi kufikia kusababisha kifo cha huyo mke wa Kivietnam.

Ndoa za kimataifa zinaongezeka kwa kasi sana nchini Korea. Takribani asilimia 11 (matukio kama 35 elfu ) ya ndoa zote ni za kimataifa kwa mujibu wa ofisi ya takwimu ya Korea. Lakini wengi huzichukulia kama ni ndoa za masharti kati ya Wakorea wasio na vigezo vya kuoa na wanawali wa kutoka nchi za kigeni ambao hununuliwa kwa dola elfu 7 hadi elfu 10. Katika karibu kila ndoa wanandoa huwa hawawezi kuongea lugha ya mwingine, na ndoa hiyo yenye mapungufu hushindwa kuendelea na mume humpiga mke hatimaye mke hukimbia. Pale hali inapoweza kuvumilika, wake hutuma pesa nyumbani kwao. Napesa zinazotumwa na wanawali hao wadogo hubadilishwa na kuwa kiasi kikubwa kutokana na tofauti iliyopo kiuchumi.

Mwanablogu wa Kikorea Trustme77 anayeishi Vietnam aliyaweka haya pamoja [3]Wavietnam wametoa maoni kuhusu habari hii. Wengine walielezea simulizi zao za kusikitisha na wengine hawakuzuia hasira zao kwa wakala wa ndoa husika na serikali.

슬프다. 많은 베트남 여성들이 돈 때문에 그들 스스로의 존엄성을 상관하지 않는다. 더 슬픈 것은 베트남 법이 너무 느슨하다는 것이다. (Bui Tan Man)
도박같은 삶. 젊은 여성들은 외국 생활을 이해하지 못한다. 대부분 천국일 것이라고 생각한다. 그것은 순진한 여성들이 실수일 뿐이다. (Ta Duc Thong)
당신이 깨달았을 때 행복은 없다. 나는 한국 남성과 결혼하여 한국에서 살고 있다. 나는 브로커를 통해서 결혼했고 수백명의 여성들 사이에서 선택되었을 때 울었다…몇 달 간의 서류 절차를 거처 한국에 갔을 때 나의 꿈은 완전히 무너졌다. 그는 직업이 없었고 간질병 환자였다. 속았다는 것을 알았을 때 고향을 그리워하며 많이 울었다. (Nguyen Thi Hong)
국제 결혼 브로커들은 처벌되야 한다. 왜 당국은 나서지 않는가? (Anh Minh)

Hii inahuzunisha: wanawake wengi wa Vietnam hawajali kabisa juu ya utu wao na huuzwa kwa pesa, cha kusikitisha zaidi ni kwamba sheria za Vietnam ni dhaifu sana. (Bui Tan Man)
Maisha ya Kamari: wengi wa wanawake vijana hawafahamu jinsi maisha yanavyoweza kuwa huko ughaibuni. Wengi wanafikiri kuwa yanaweza kuwa kama peponi. Lakini hilo ni kosa kwa hawa wanawake wanaoamini kiurahisi. (Ta Duc Thong)
Kamwe hakuna furaha ukigundua kuwa: Nimeolewa na mwanaume wa Kikorea na sasa ninaishi Korea. Niliolewa kwa kupitia wakala na nililia (kwa furaha ) nilipochaguliwa kuolewa kati ya maelfu ya wanawake wengine… Baada ya miezi kadhaa nilipata karatasi, nikawasili nchini Korea na ndoto yangu ikapigwa chini. Mume wangu hakuwa na kazi na pia ana kifafa. Nilipogundua kuwa nimechezewa, Nililia sana nikifikiria kuhusu kwetu. (Nguyen Thi Hong)
hawa wakala wa ndoa wa kimataifa wanapaswa kuadhibiwa. Kwa nini serikali haipo makini katika hili? (Anh Minh)

Kutojali kwa Wakorea hakuisaidii, aliasa mwanablogu Danbee 928, [4] akiwataka Wakorea kukumbuka wakati wa unyenyekevu wa ile miaka ya 1960 hadi 70, wakati wakorea wengi walipoenda kwenye nchi za magharibi au vitani ili kupata pesa za kutuma nyumbani.

우리에게도 과거 가난을 탈출하겠다고 서독 광부로, 간호사로, 그리고 월남전으로 떠난 일이 있습니다. 낯설고 물설은 이역만리에서 가난을 이겨 나가겠다고 그리고 되물림 하지 않겠다고 얼마나 힘들게 지냈는지. 왜 개구리 올챙이적 생각을 하지 못할까요?

Na sisi pia tuliwahi kwenda nchi za watu kusaka pesa, baadhi kama wachima madini huko Ujerumani Magharibi, wengine kama wauguzi na wengine kama (askari au wafanyakazi) wakati wa vita ya Vietnam. Mnakumbuka jinsi tulivyohangaika huko kwenye nchi za mbali, ambako hakuna ulichokuwa unakifahamu, ili kupiga vita umasikini na kuwaepusha na njaa watoto wetu. Kwanini tusiukumbuke wakati huo wa unyenyekevu?

Polisi wa Korea Kusini waliahidi kufanya uchunguzi wa nchi nzima ili kujua mtandao wa hawa wakala wa ndoa, ili kujua ndoa zilizosajiliwa na zisizosajiliwa. Wanablogu wanatumaini kuwa uchunguzi huo utakuwa wa uhakika na wenye hitimisho zuri ili kufuta doa hili katika jina la taifa.