Wakati ambapo taarifa za siku za karibuni kutoka WikiLeaks [EN] zimeweka bayana hamu ya kuanzisha “kanda za kieneo za uhuru wa habari” kwa msaada fulani kutoka Iceland [EN], Serikali ya Italia inaonekana kuelekea upande mwingine tofauti.
Muswada wa Sheria ya Vyombo vya Habari na Usikilizaji Mawasiliano kwa Siri [EN] ambao ulikuwa ukifikiriwa kujadiliwa na Bunge la Italia kwa muda wa miaka miwili sasa (na ambao ulikosolewa vibaya sana na Umoja wa Kimataifa) [soma zaidi kupitia vyanzo mbalimbali kwa lugha ya Kiitaliano hapa] inasemekana ungeanzisha kile kinachoitwa “sheria kabaji” ambayo ingewazuia waandishi wa habari kuchapisha rekodi walizonasa kwa siri za mawasiliano wakati wakifanya uchunguzi, hasa kwa lengo la manufaa ya umma. Hapa tunapongeza juhudi zisizokoma za raia na waandishi wa habari, maana vikwazo hivyo viliondolewa rasmi kutoka kwenye vifungu vya muswada huo mnamo tarehe21 Julai. Hata hivyo, bado toleo jipya ya muswada lina vipengele vinavyolenga kuzuia moja kwa moja uhuru wa kujieleza wa mtandaoni, hiki ndicho kinachoitwa kipengele cha “kuua blogu” (aya. 29 ya Kifungu 1). Kama inavyoeleza blogu ya kikundi ya MAVAFFANCULP:
Una norma introdotta riguarda infatti proprio il mondo del web e non si capisce cosa c'entri con le intercettazioni telefoniche. E’ infatti fatto obbligo a qualsiasi blog e quindi a qualsiasi blogger di rettificare nello spazio di 48 ore una notizia o un articolo che possa contenere una informazione non corretta.
In sostanza, se la norma venisse approvata, tutti i blogger dovrebbero stare all'erta per pubblicare una eventuale rettifica che gli sia richiesta pena una multa di 12.500 euro. Non c'è verso di fare neppure una settimana di vacanza tranquilli! E’ evidente che questo porterà molti siti a una scelta drastica. O si chiude o si smette di occuparci di argomenti su cui i potenti, e i loro agguerriti avvocati, sono particolarmente sensibili.
Kimsingi, endapo sheria itapitishwa kama ilivyo hivi sasa, wanablogu wote watapaswa kurekebisha mara moja masahihisho yoyote yatakayohitajika au wanaweza kutozwa faini ya mpaka Euro 12,500. Hii ina maana kwamba hatuwezi hata kwenda likizo fupi! Ni wazi kwamba jambo hili litalazimisha tovuti nyingi kufanya uamuzi mmoja mkubwa. Au kuzifunga kabisa ama kuacha kushughulika na mambo yanayowagusa watu fulani wazito, hasa ukizingatia kwamba wanasheria wao machachari wako makini kabisa na jambo hili.
Kwa mara nyingine tena, watu wanaeleza kutoridhishwa kwao, wanafanya hivyo kupitia Mtandao na hata mitaani. Jamii ya mtandanoni Valigia Blu iliratibu shughuli nyingi katika majuma yaliyopita, mojawapo ikiwa ni maandamano makubwa yaliyopangwa kufanyika tarehe 29 Julai kuanzia saa 10 jioni,, katika eneo la Piazza Montecitorio, katikati ya jiji la Roma, ili kuadhimisha kuanza kwa majadiliano ya mwisho ya muswada huo wa sheria katika Bunge.
Kwa sasa hivi, watu wanahamasishwa kwenye barua kwa Wabunge ili “Kufungua upya mdahalo na aya ya 29 ya Kipengele cha 1:mpaka sasa barua hiyo imetiwa saini na raia wanaozidi 11,000, hiyo ni pamoja na sahihi nyingine 240,000 zilizokusanywa katika maandamano yaliyopita huko jiji la Roma mnamo tarehe 1 Julai– tazama picha iliyo mkono wa kushoto, inatoka kwenye mkondo wa picha za Flickr katika Valigia Blu.
Kuna video nyingi ambazo watu wametengeneza wenyewe zilizotumwa katika YouTube, mojawapo ikiwa ni hii iliyotumwa na nikilnero.
Taarifa pia inasambazwa kupitia Twitter kwa anwani hashitagi hii #nobavaglio:
- http://nobavaglio.adds.it imeandaa waraka wa kutaka kuungwa mkondo dhidi ya Sheria Kabaji, je, unaweza kunisaidia kupata watu wa kutia saini katika waraka huu?
- Tovuti za TV za hapa ziko hatarini kufungwa, sheria hii kandamizi inatishia uhai wa TV zaidi ya 350
- hapa hali ya kuchanganyikiwa ndiyo inayotawala, kama ilivyo katika dola lililo nyuma kabisa, lililosahauliwa, lisilo na jina …
Kundi la Facebook la No Legge Bavaglio limepitisha wanachama 6,500 (kufikia 11,000 kama wakijumlishwa na waungaji mkono wa mtandaoni) na linaendelea kutoa taarifa na habari mpya kila saa:
Vyombo vya habari vikongwe navyo vinapinga sheria hiyo iliyopendekezwa, vikieleza kwamba yeyote anayetuma habari kwenye mtandao (zikiwemo tovutiza redio na TV) atawajibika na “Takwa hilo la kufanya masahihisho”. Katika tovuti ya gazeti la kila siku la Il Fatto Quotidiano ina taarifa hii:
Tutte le web tv ed i video blogger italiani, in forza degli emanandi regolamenti, dovranno chiedere all’Agcom un’autorizzazione – o almeno indirizzarle una dichiarazione di inizio attività -, versare 3000 euro per il rimborso delle spese di istruttoria (quali?) e, soprattutto, finiranno assoggettati, tra gli altri al solito obbligo di rettifica, sempre entro 48 ore e sempre sotto la minaccia di una sanzione fino a 12 mila e 500 euro .
L’obiettivo dell’ultimo scellerato progetto di Palazzo sembra evidente: ora che il Cavaliere si accinge a sbarcare in Rete avendone forse, almeno, subodorato le enormi potenzialità, la vuole tutta per lui, per i suoi amici e per i soli suoi nemici che ha, comunque, la garanzia di poter controllare almeno in termini economici.
Lengo la sheria hii inayopigwa vita sana ya Berlusconi sasa lipo bayana. Sasa kwa vile anajiandaa kuanza kujishughulisha Mtandao, labda baada ya kuona jinsi anavyoweza kunufaika sana, anataka mtandao mzima uwe wa kwake yeye peke yake, pengine na marafiki zake na maadui wachache ambao anaweza kuwadhibiti kwa njia za kiuchumi.
Maoni mengine ya mtandaoni yanaeleza madhara hasi ya “sheria hii kabaji” kwenye shughuli za biashara za mtandaoni, , kama alivyoeleza Enrico Giubertoni kupitia Buzzes:
È immorale poiché impedisce de facto ogni forma di critica, è antieconomico poiché impedirà di affermare un principio cardine del Social Media Marketing ovvero il giudizio su un prodotto. Se scriverò che il prodotto A non è bene mentre B è meglio, il produttore di A potrà obbligarmi a rettificare. Come faremo a fare InfoCommerce con l’Ammazza Blog?
Baadhi ya marekebisho mahususi ya kufutilia mbali kifungu “kinachoua blogu” tayari yametangazwa, lakini kwa kutazama muktadha mpana zaidi kuna wingu zito la mgogoro wa serikali mpya, na kusudio linaloendelea la kuweka kwa lazima vikwazo kwenye uhuru wa kidemokrasia wa kujieleza wa raia. Hata hivyo, kule Bungeni kila mmoja amekuwa bubu. Hakuna anayejua kifungu hicho kidogo kiliingiaje kwenye muswada wa sheria ya usikilizaji wa mawasiliano kwa siri.
Katika makala moja ya blogu iliyopewa jina la “Il legislatore fantasma” (Mtunga Sheria wa Kimzimu), Massimo Melica anasema:
Ho provato in ogni stanza, corridoio, stanzino ministeriale…nessuno conosce o ricorda chi ha redatto il testo inserito nel “ddl intercettazioni”, nella parte che riguarda Internet.
Ho sfidato il Sig. Nessuno e nessuno ha accettato la mia sfida.
Quindi ci ritroveremo una norma (comma 29 art.1 ddl intercettazioni) pensata da Nessuno, voluta da Nessuno e scritta da Nessuno ma alla fine approvata dal Parlamento italiano.
Inutile gridare al complotto perchè non c’è, si tratta della burocrazia e della politica incapace di tener traccia dei suoi movimenti.
Nilimtupia changamoto Bw. Hakuna Mtu na hakuna mtu amekabiliana na changamoto yangu hiyo.
Kwa hiyo, hatimaye tutakuwa na sheria (aya ya 29 ya kipengele cha 1) ambayo imetungwa na Hakuna Mtu, inayotakiwa na Hakuna Mtu na Kuandaliwa na Hakuna Mtu, lakini ambayo hatimaye ilipitishwa na Bungela Italia.
Hakuna sababu ya kubishana kuhusu njama ambazo hazipo, labda kwa makosa urasimu na siasa zimeshindwa kutunza kumbukumbu za jambo ambalo wenyewe wamelianzisha.
NYONGEZA YA KARIBUNI (tarehe 30 Julai): Hatimaye Bunge limeamua kuahirisha majadiliano kuhusu muswada huo mpaka mwezi Septemba.